Zanzibar: Mbunge wa jimbo la wawi Mohammed Juma Ngwali (CUF) ajivua uanachama wake na kujiunga na CCM

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,909
14,413
Mbunge wa Wawi (CUF) Mkoa wa Kusini Pemba, Ahmed Juma Ngwali amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia CCM

Tutaheshimiana tu,CCM for 2020-2025
1583159715282.png

=======

TAARIFA YA HIVI PUNDE

02 March 2020

NG'OME YA MAALIMU SEIF YASAMBARATISHWA - PEMBA

Mbunge wa Jimbo la Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba kwa tiketi ya CUF Ndugu Mohammed Juma Ngwali amejivua vyeo vyake vyote ndani ya Chama hicho na kuomba kujiunga na CCM leo.

Mbunge huyo ambaye alikuwa Kundi la Maalimu Seif amepokelewa na Ndugu Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM Taifa akiwa pamoja na Wanachama wa CUF na ACT 1854.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Upinzani umemalizika rasmi. Pemba ilikuwa tegemeo la mwisho!

Una mtazamo tofauti kabisa, Pemba na Zanzibar hali ni mbaya zaidi kwa watawala kila uchao kwa taarifa tu ni kwamba huyu Ahmed Ngwali alikuwa ndumila kuwili tokea siku ya kwanza na kabla uchaguzi wa 95 alitaka kuwekwa pembeni lakini maalim seif alimpigia kifua baadae ndio akaja kumsapoti Lipumba kwa kila hali lakini la kushangaza zaidi ata huyo Lipumba naye amemsaliti ameendazake ccm.

Huyu Ahmed alidhani Lipumba atakuwa na impact Zanzibar lakini hesabu zake zikamcheza leo ndio ameangukia ccm ambayo kwa kule pemba ccm kushinda ata jimbo 1 la uchaguzi ni 0%. Ndo mana tunasema huyu Ahmed amekwisha tena safari yake ya kisiasa.

Kule Pemba labda usikie ACT wamesusia uchaguzi mkuu otherwise ni kilio kile kile, wananchi wa pemba na zanzibar hawana bei hawanunuliki siasa bado ni mbichi kwa Zanzibar.
 
TAARIFA YA HIVI PUNDE

02 March 2020

NG'OME YA MAALIMU SEIF YASAMBARATISHWA - PEMBA

Mbunge wa Jimbo la Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba kwa tiketi ya CUF Ndugu Mohammed Juma Ngwali amejivua vyeo vyake vyote ndani ya Chama hicho na kuomba kujiunga na CCM leo.

Mbunge huyo ambaye alikuwa Kundi la Maalimu Seif amepokelewa na Ndugu Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM Taifa akiwa pamoja na Wanachama wa CUF na ACT 1854.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI

b0f28575-7fcb-49ab-9440-7e557b2dd1ca.jpg
0ed59b9a-5785-48e4-8682-f56168a26228.jpg
d7d9cc62-78ab-4e87-9111-5f21caf018a1.jpg
 
Sasa hivi kuna pesa zinatembezwa kwa wabunge wale walio tayari kwenda kuunga juhudi, kuna tetesi kuwa wanalipwa Tsh. 600 million halafu na kuhakikishiwa kuwa mafao yao ya ubunge pia yanabaki "Intact".

Ni wale wenye roho ngumu sana ndio wataukataa huu mradi. Ktk dili hii ambayo madiwani desperate hununuliwa kwa hadi Tsh. 60,000,000/- depending on the intensity of the bargain, inawafanya walengwa waamue kuchukua mlungula bila kujali majaaliwa ya uchaguzi ujao kwani hawajui kama vyama vingine vinaweza vikaugomea au la hivyo wanaona wavune tu kwani hawajui ya kesho.

Wakati haya yakiendelea kuna maelfu ya watoto wa kitanzania wenye sifa za kusoma vyuoo vikuu wamenyimwa mikopo. Inatia uchungu sana hii. Kwa hali hii Magufuli hana namna lazima tu awe refa ktk mechi ambayo pia yeye ni mchezaji kusudi ushindi upatikane, vinginevyo wanaona watatema kombe.
 
Back
Top Bottom