Zanzibar kuna lockdown ?

Marco Polo

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
13,208
Reaction score
20,954
Niko mtaani mara nashtukia mkwaju wa mgongo nageuka niulize kulikoni nakula mtama nikanyanyuka na kutoka mbio, nimefika huko mbele nawauliza watu naambiwa kuanzia saa 12 haruhusiwi mtu kuzurura barabaran kisa tishio la korona,

Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kama tv's, redio na magazeti na sijaona wala kusikia tamko rasmi la Serikali ya SMZ kuhusu watu kutotoka nje, kwanini wasitutangazie kuliko kuvamia na kusumbua watu?
 
Hahahaha nimecheka kifala

Sent from my vivo X21 using Tapatalk
Usicheke mkuu!!

hivi vikosi vyetu vya ulinzi na usalama ni bure kabisa, sijui huwa wanatumia vigezo gan kuwaajir hawa watu, sasa mm najiuliza wangekuja wakanifahamisha vizur kwamba natakiwa kuondoka kwenda nyumbani mm ningewabishia? Si ningeondoka zangu kwa amani tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole jombaa

Sent from my vivo X21 using Tapatalk
 
Sorry bro nacheka vile umeelezea mkasa wako kicomedy lakini nimesikitika kwa ulivyofanyiwa,
Kesho utakua ndani saa 10 tu.
Lol


The best Medicine of Corona is to Stay Home.
 
Acha kutudanganya inamaana hilo eneo ulikuwa peke yako au kulikuwa na raia wengine,na je Kama hakukuwa na watu wengine wewe hukushangaa kuwa kwanini siku hiyo uko peke yako hilo eneo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungewamwagia hata mchanga haiwezekani upigwe bure bure.
 
Niko mtaani mara nashtukia mkwaju wa mgongo nageuka niulize kulikoni nakula mtama nikanyanyuka na kutoka mbio,


Haha pole sana mkuu kwa matatizo yalokukuta.
 
Mkuu ni kweli wanapiga haswa mkikaa vikundi mnakung'utwa! Ni upuuzi sijui serikali za kipolisi zinawaza kutumia nini..?
Hii ni aibu kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…