Zanzibar Isaidiwe??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Isaidiwe???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Dec 20, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  HALI ya maisha visiwani Zanzibar ni ngumu kwani gharama za maisha zimepanda baada ya kupanda kwa bei ya mafuta pamoja na kutokuwapo umeme.

  Zanzibar imekumbwa na tatizo la umeme baada ya njia inayopitisha umeme kutoka bara kuharibika na tatizo hilo linatarajiwa kumalizika Januari mwakani.

  Kwa mtu aliye mbali na Zanzibar ni vigumu kupata picha halisi ya hali ya maisha visiwani humo kwa sasa, lakini ukweli ni kwamba ndugu zetu wa Zanzibar wako katika wakati mgumu na wanahitaji kusaidiwa kuondoka katika hali hii.

  Kwa mujibu wa moja ya habari za leo kwenye gazeti hili, wafanyabiashara wengi wameathirika kutokana na tatizo la umeme na baadhi wamefunga biashara zao.

  Kibaya zaidi hata televisheni ya taifa visiwani humo imesitisha matangazo yake kutokana na kutokuwepo kwa umeme.

  Biashara zilizoathirika zaidi na tatizo hilo ni pamoja na saluni za kiume na kike; vibanda vinavyotoa huduma mbalimbali, vikiwamo vya vinywaji baridi; wauzaji wa samaki na baa; kumbi za starehe; na nyumba za kulala wageni, huku biashara ya teksi na daladala zikiwa ngumu kutokana na ukosefu wa mafuta.

  Nyumba za kulala wageni zilizobahatika kuwa na jenereta huwashwa kwa muda fulani hasa usiku na kuzimwa mchana hali inayosababisha kuwapo kwa joto ndani ya nyumba hizo kwani hazitumii viyoyozi.

  Kila kona ya mji wa Zanzibar, imetawaliwa na miungurumo ya jenereta kiasi cha kuwa kero kwa wageni hasa watalii, huku gharama ya kuchaji simu za mkononi ikiwa sh 1,000.

  Bila kusahau kuwa vibaka nao wamechukua nafasi yao, uporaji wa simu na ukabaji ni jambo la kawaida.

  Biashara inayoshamiri na kuingiza pesa kwa haraka ni ya jenereta; biashara ambayo inafanywa na wafanyabiashara wenye mtaji mkubwa.

  Zaidi ya jenereta 100 huingizwa visiwani Zanzibar kila siku kutoka Bara na kuuzwa kwa wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani au biashara.

  Hata hivyo baadhi ya jenereta hizo si imara kwani baadhi hulipuka kutokana na kutumiwa kwa muda mrefu.

  Kwa kifupi, hali ya maisha imekuwa ngumu kwa wananchi wa Zanzibar na pato lao kwa mwezi lazima liporomoke kutokana na vyanzo vya kodi kupungua.

  Tunachukua nafasi hii kuwapa pole Watanzania wenzetu kwa tatizo hili la kukatika kwa umeme kwani si tu kwamba linaleta kero kwa wananchi wa visiwa hivyo, bali pia litarudisha nyuma harakati za kukuza uchumi.

  Sisi tunaamini kuwa matatizo ya Zanzibar ni yetu sote hata kama Wizara ya Nishati na Madini si sehemu ya wizara za Muungano, lakini tunaamini katika hili Zanzibar inahitaji msaada si tu wa kifedha bali pia wa mawazo ya jinsi ya kuondokana na tatizo hili.

  Taarifa za awali zinaonyesha kuwa hali ya umeme katika visiwa hivyo inaweza kurejea mwakani baada ya wataalamu kuwasili na pengine ikachukua muda zaidi kuweza kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida.

  Tunaitaka Serikali ya Muungano kwa kushirikana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuangalia namna ya kuondoa tatizo la umeme visiwani humo, vinginevyo athari zake zitatuangukia sote.


  Source: Tanzania Daima

  "Kusema ukweli haya yaliyozungumzwa ni kweli kabisa na hali inasikitisha zanzibar. Lakini swali linakuja wale wanaotishia muungano ufe wanaliona hilo au wanataka kuwazungusha maskini ya watu waamini wanawatetea kumbe wanataka wachaguliwe na waendelee kukaa madarakani milele!!!!"
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Poor leadership, ni kilio cha wengi miongoni mwa ngozi nyeusi.

  Inasikitisha kuona visiwani pamoja na kuwa kusifika duniani pote kwenye utalii lakini wanahit the dog level kwa namna tunayoishuhudia sasa kiasi hata cha kukosa umeme.

  Ktk larger picture muungano unakwamisha mambo in terms of who has final say kwenye ishu nyeti.
   
 3. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,042
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  eehhhh eeeh yamekuwa hayo!!!!!mwenye final say NI RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR na BARAZA LAKE LA WAWAKILISHI.......mnataka kuhamisha matatizo yenu kwa BARA au SMT?????acha kila nchi ibebe mzigo wake yenyewe.
   
 4. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nanyie nanyi jambo likitokea makurupuka na huo Mungano ,tatizo la zanzibar ni hizo fitna zilizoletwa na kuwafanya viongozi wetu kushindwa kukaa pamoja na kuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo ya wananchi wa zanzibar .
   
 5. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,795
  Likes Received: 2,569
  Trophy Points: 280
  Zanzibar inahitaji emergency power plant .Nakumbuka zanzibar demand ni about 40 megawatts ,easily supplied by 2 to 3 diesel fired power plants.True diesel power plants are expensive to run however opportunity cost of one month plus power blackout should be much greater.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Buraza una matatizo ya msingi ya uelewa. Pole.
   
 7. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Una maanisha TBC? Mbona wanabroadcast kutokea Dar na wapo ktk satellite? Au kuna Television nyingi za Taifa hapa JMT?
   
 8. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145

  Ana maanisha television ya zanzibar TvZ!!
   
 9. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Unahitaji uwe na roho ngumu kuishauri SMZ, si mmesikia karume anavyoskip vikao vya baraza la mawaziri bila hata taarifa!!

  Waache kina yakheee wapambane na matatizo yao!!
   
 10. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,389
  Likes Received: 3,707
  Trophy Points: 280
  Hapana unahitaji uwe na roho kama ya mwendawazimu...............
   
 11. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kweli .....zanzibar hali ya uchumi inaenda kuwa mbaya sana...
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Pengine tungefuatilia yanayotokea ulaya sasa kutokana na Baridi. Maafa hutokea popote!
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Leo hii unafahamu hilo? Sisi Bwana! ni vigugumizi.
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Baraza la Mawaziri la Zanzibar?
   
 15. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndiyo part ya utalii wenyewe!!!!
   
Loading...