Zanzibar is gone | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar is gone

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Jun 12, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna habari za kutatanisha kuwa tayari baraza la wawakilishi la Zanzibar au tunaweza pia kuliita Bunge la Zanzibar wanavutana kuhusu kuvunja Muungano na kundi linaloelekea kushinda ni lile linalotaka iitishwe kura ya maoni kuhusu hatma ya Muungano ,likidai wananchi waliowatuma wanahitaji kura ya maoni kuhusu Muungano ,ili ipatikane ridhaa yao.
  Wengine walifika kuhoji mbona Tanzania haijatia saini kuhusu muungano wa East Africa hadi leo ? Wanaogopa kitu gani ?

  Pia kuna tetesi kuwa umoja wa serikali ya kitaifa huenda ukavunjika muda si mrefu ,kuna upande utawasilisha na kuanzisha mvutano huo wa kura ya maoni na hapo ndipo tishio la kuvunjika kwa Muungano huo wa GNU.

  Kwa kweli WaZanzibari wengi wamechoshwa na Muungano, kwani kuna wastaafu wengi wa kutoka JWTZ ambao nao wameonekana kupanda kwenye viriri wakisema hawalipwi mafao yao na hawana pa kuyadai ,serikali ya Muungano imewatelekeza na kuwatupa.

  Kuna tetesi zingine zinasema Maalim Seif atamshauri Dr Shein na pia kuishauri serikali kuitisha kutangaza mgogoro wa Muungano na kuitaka kuitisha kura ya maoni ,ikiwa hoja yake itakataliwa basi atakuwa hana faida ya kubakia hapo alipo kama makamo wa Raisi kwani ni kuwasaliti wananchi.

  Wananchi walio wengi wanasikika wakiitajataja hoja ya G55 wakidai kama wao wana makosa basi wale wa G55 nao wafikishwe mahakamani la si hivyo hoja ile itaendelezwa hadi kieleweke ,wengine walihoji kwa nini wabara(TZ) wanaona hayana aibu kuidai au kuishi kama Tanganyika, kwa nini wanaidharau Nchi yao.

  Hivi ni WaZanzibari tu ndio wanahamu na kuwa na Taifa lao na kutunza itikadi na silka zao ukichanganyishwa na utamaduni wao ,hawa WaTanganyika wao vipi ? Mbona wanaing'ang'ania Zanzibar na wengine wanafika hata kufurahi unapowaita kuwa wao ni WaZanzibari na kunakuwa na mbinde ukimwita kuwa ni m'bongo ,huku ni kupotoka kwa mtu kudharau chake.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanza Zanzibar hawana Utamaduni wao; Utamaduni wao ni kwa kiarabu toka Oman

  Wengi waliokwenda huko kama Watumwa na kubaki kama wananchi Walipochukua Dini ya kiislamu; na Tamaduni zao

  Zilipotea; Wakautwaa Uislamu... Maalim Seif alikuwa kilioni ana nyumba Bara, Wanadhani Wakivunja huo Muungano bado

  Watakuja Bara kama kwao? Waache Wafanye watakavyo... Ni wakati Mzuri... Rais wa Muungano ni Muislamu. Waziri wa

  Ulinzi Muislamu.

  * Na hapo hao Wanajeshi wa Zanzibar kutolipwa Waziri wa Ulinzi kwa Miaka 10 ni Mzanzibari; Mtoto wa Mwinyi kwanini wasipeleke

  Matatizo yao kwake; Haya Sasa Hivi Waziri wa Ulinzi ni Mzanzibari tena, kwanini wasiende kumuona? au ni Uvivu na kupenda kukaa

  barazani na kulalama?
   
 3. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ...mpira miguuni 'kwao', golini hakuna kipa, wafunge tu....
   
 4. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Source plse
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Niliweka topic kama hii toka Zanzibar Daima; kuhusu Wawakilishi wa Zanzibar Wanavyovutana kuhusu Muungano

  Na wanasema wakikutana baadaye July wana kura ya kutaka kura ya Maoni ya Wananchi
   
 6. NDAMANDOO

  NDAMANDOO JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 250
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Waacheni, ya NYERERE yatatimia, leo wao watanganyika kesho wao wapemba. hakuna kambi ya wakimbizi itakayoanzishwa kwa ajili yao baada ya wao wenyewe kurumbana.
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Waafrika bwana ndivyo walivyo kufikiria kutengana nyakati hizi duh haya yetu macho tutaona mwisho wake
   
 8. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Si muende?
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ushauri wangu tujitenge nao then am sure akina Boko Halam,Alcaeda na Alshababy watafanya makao kule.
  Then baada ya hapo tunaitwaa zanzibar kijeshi kama sehemu ya Tz bse machafuko hayatakoma uko.
   
 10. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu sio tetesi ni habari za uhakika kabisa,

  Mgogoro uliopo sasa ni kuwa hata watetezi wa muungano zanzibar wanaogopa kujitokeza, wenye nguvu sasa ni wale wanaopinga. Mungu ibariki Jamuhuri ya watu wa zanzibar.

  Sera za muungano za CCM huenda zitapelekea kushindwa vibaya znz kwa chaguzi zijazo!
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwani lini waliwahi kushinda?
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,734
  Trophy Points: 280
  Wazanzibari chukuane kanchi kenu.
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wazanzibar wana hoja ya msingi, japo hawaathiriki kivile kwakuwa wao tayari wana serikali kamili ya umoja wa kitaifa.
  Tatizo kubwa lipo upande wa Tanganyika. Kwa kweli ni aibu na fedheha kwa wazanzibari kuwasaidia watanganyika kudai serikali ya Taganyika, bila kuwa na reaction yoyote kutoka Tanganyika. Ni vizuri watanganyika wakaelezwa hasa na serikali ya Muungano huu uliokaa kushoto kuwa kuna siri gani tofauti na usia wa nyerere kuulinda muungano. Lazima nikiri kuwa Nyerere alifanya mengi mazuri kwa maslahi ya Tanganyika, na Karume alifanya vivyo hivyo kwa maslahi ya wazanzibari. Lakini pia lazima tukumbuke kuwa Nyerere hakuwa malaika, hivyo inawezekana labda alikosea, either kwa kutojua ama alijua.
  Hivyo watanganyika tunatakiwa tuamke, badala ya kuutetea muungano tunatakiwa tuujadili muungano huu, tuangalie maslahi ya pande zote mbili, na kama hakuna faida yoyote, na unatia hasara kwanini tuendelee kuwa na muungano huu kisa tu kwa ajili ya usia wa Nyerere ambaye pia ni mwanadamu?


  Otherways, I stand to be corrected!

  Mungu Ibariki Tanganyika wa watu wanyenyekevu, wastaarabu, wapole na wakarimu kwa wenzao wa upande ule.

  Mungu tunaomba uwang'ate sikio magamba waamke sasa watusaidie kuifufua Tanganyika yetu, au kama vipi, Tenda Miujiza bwana Mungu wa Majeshi, kazi hiyo waachie CDM na uamsho wakaitekeleze within a second!

  Still stand to be corrected!
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Baraza la wawakilishi halina nguvu ya kuvunja muungano.Bunge la JMT ndiyo chombo pekee chenye mamlaka na nguvu za kuvunja muungano.

  WaZanzibar kama kweli wamepania kuvunja muungano hawapaswi kupiga kelele kwenye baraza la wawakilishi watatakiwa kufanya yafuatayo.

  [1] Wamwagize makamu wa Rais Dr Gharib Bilal ajiondoe katika serekali ya muungano.

  [2] Mawaziri wote kutoka Zanzibar wajiondoe katika serekali ya muungano.

  [3] Wabunge wote toka Zanzibar wajiondoe katika vikao vya bunge la JMT.

  [4] WaZanzibar wote walioko Tanzania bara au Tanganyika warejee Zanzibar au waombe passport ya kuishi Tanganyika.

  [5] WaTanganyika wote wanaoishi Zanzibar warejeshwe Tanganyika watakao penda kubaia lazima wapatiwe passport ya Tanganyika mara moja.
   
 15. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,365
  Likes Received: 8,351
  Trophy Points: 280
  mbona wanachelewa kuuvunja
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Unajua nngu007 huwa tunasahau kuwa kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi. Let them go....kelele hizi zinachosha na naamini watu wenye vision wamesema sana umuhimu wa muungano huu. Ila huwezi kulazimisha mambo kila wakati
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Mkuu umefikiria kama vile unashauriana na Putin...hiyo strategy mbona kiboko
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Utamaduni na Mila za Muislaam popote alipo ni Uislaam. Kumbuka hilo. Uislaam umekuja kuondosha mila na tamaduni za "kishenzi" na kuifanya dunia iwe na mila na tamaduni moja nayo ni UISLAAM.

  Wanachosema Wazanzibari ni kweli kabisa, Jee, sisi hatuitaki nchi yetu ya Tanganyika?

  Ikiwa wao watakuja kama wageni na sisi tutakwenda kama wageni kama ilivyo kwa mataifa mengine wanayoishi hapa na Zanzibar.

  Naona ni wakati muafaka kila mmoja awe na nchi na Serikali yake na Muungano uwe wa nchi mbili zinazojitegemea kipekee.
   
 19. NDAMANDOO

  NDAMANDOO JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 250
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Natamani ngelikuwa Rais! maelekezo yote kuhusu Muungano nilipewa na mwl kabla ya kifo chake.
   
 20. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Ipotee tu ntafurahi kweli
   
Loading...