Zanzibar ipewe kipaumbele kwenye miundombinu

Tuacheni mihemuko, Kuengezeka kwa watalii na kukua kwa Utalii Zanzibar neema yake ni kwa wote na si kwa wazanzibari pekee, Ajira ni za wote, visa na permit fees zote hela inaingia direct kwenye jamhuri ya muungano. Na faida kiujumla ni nyingi sana.
 
Zanzibar ndio lango la utalii nchini. Nashauri pesa nyingi ipelekwe huko kuendeleza miundo mbinu ya barabara, airport na hotel

Tangu lini Zanzibar ikawa lango la utalii Tanzania?
Hivi vitu vinahitaji taaluma/reference sio kuandika tu kwa hisia
Watalii takriban 75% wanatokea bara kwenda Zanzibar kwahiyo kitwakimu (bara) hasa Kilimanjaro na Arusha ndio Lango la Utalii Tanzania.
Watalii huja kwa wingi kutembelea Mbuga za wanyama na Kupanda Mlima Kilimanjaro; baada ya hapo baadhi yao ndio hupenda kwenda Beach na hivyo kwenda zanzibar.

Ukumbuke utalii wa Beach (Sun, Sand & Sea) unaushindani sana, mfano; Anse Lazio hapo Seychelles ni the best beach; hapo kwa jiarani Kenya - malindi, Watamu nk, wanafanya vizuri sana, Lakini usisahau, Africa kusini, Msumbiji na hata visiwa vya Malta kule kskazini wana white sand beach nzuri sana duniani na watalii hupenda kufurika huko.
Namaanisha, beach zina mbadala wa Zanzibar ila hakuna mbadala wa mlima Kilimanjaro & Mbuga
 
Zanzibar ndio lango la utalii nchini. Nashauri pesa nyingi ipelekwe huko kuendeleza miundo mbinu ya barabara, airport na hotel
Kwani si wana serikali yao na mamlaka yao ya mapato wanashindwa nini kujenga hiyo miundo mbinu au ndiyo ile sera yenu ya changu changu chako changu.
 
Back
Top Bottom