Zanzibar inajitenga kupitia michezo?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Kuna kila dalili kuwa wazanzibar kwa umoja wao wanashindwa kudai kujitoa kwenye Muungano kwa njia za uwazi. Kujitoa kwenye ligi ya Muungano (super league), kuomba na kupata uwanachama wa CECAFA na sasa CAF na baafaye FIFA ni uthibitisho kuwa huenda mawazo yao ni kuzidi kuwa huru zaidi huko siku za mbeleni kwa kuanzia na michezo kisha yale mengine magumu kutamkika.
 
Afadhari tuwe na Tanganyika yetu. Hii mizigo kujibebesha bila sababu ya nini!
 
Hivi watakapocheza mechi ya kimataifa watapigiwa wimbo gani wa taifa?
 
Ngoja tuone muda utaamua, ila mi naona sawa tu si wameambiwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe
 
Kuna kila dalili kuwa wazanzibar kwa umoja wao wanashindwa kudai kujitoa kwenye Muungano kwa njia za uwazi. Kujitoa kwenye ligi ya Muungano (super league), kuomba na kupata uwanachama wa CECAFA na sasa CAF na baafaye FIFA ni uthibitisho kuwa huenda mawazo yao ni kuzidi kuwa huru zaidi huko siku za mbeleni kwa kuanzia na michezo kisha yale mengine magumu kutamkika.
Mbona hats UK hii mambo ipo? Muwe mnafanya utafiti
 
Sio kweli kwamba Zanzibar kupata uwakilishi CAF ni kujitenga kupitia michezo, nchi ya Wales ipo kwenye muungano wa Great Britain pamoja na Scotland lkn zote zina uwakilishi FIFA na bado hazijajitenga, visiwa kama Samoa ni sehemu ya Marekani lkn kimichezo vinajitegemea, so katafute hoja nyingine ya maana
 
Nilivyoona furaha ya wajumbe wa ZNZ waliotoka CAF na kusikia maoni yao walipohojiwa na waandishi wa habari, bila shaka ndugu zetu wazanzibari muungano hawautaki ila wamebanwa na wapo katika muungano kwa kushurutishwa.

Kwa wazanzibari kwao kuwa mwanachama wa CAF na kisha FIFA wakifanikiwa itakua ni ushindi mkubwa sana katika kudai sovereignty yao.

Kutokana na mazingira na kauli mbalimbali za viongozi wao wa upinzani na chama tawala, bila shaka Tanganyika tunawahitaji zaidi Zanzibar kuliko wao wanavyotuhitaji. Nimetembelea ZNZ zaidi ya mara kumi, wazanzibari muungano hawautaki. wanaosema wanautaka muungano wanadhihirisha vinywani tu ili kuungamkono msimamo wa chama chao CCM ila na wao ndani ya mioyo yao msimamo wao ni tofauti, hawataki kuonekana wasaliti.

Naamini uhuru wa kutambulika ktk michezo kama nchi huru ni ushindi na hatua kubwa kwa wazanzibari. Sasa wanajipa moyo kupata uhuru wa kisiasa, kukiwa na tume huru ya kusimamia uchaguzi na demokrasia ya kweli bila kutumia nguvu za kijeshi, wakiulizwa kuhusu muungano bila shaka ndio utakua mwisho.
 
Usisahau utafutaji wa mafuta na OIC
 
Sio kweli kwamba Zanzibar kupata uwakilishi CAF ni kujitenga kupitia michezo, nchi ya Wales ipo kwenye muungano wa Great Britain pamoja na Scotland lkn zote zina uwakilishi FIFA na bado hazijajitenga, visiwa kama Samoa ni sehemu ya Marekani lkn kimichezo vinajitegemea, so katafute hoja nyingine ya maana
Wimbo, katiba, mafuta na....!?
 
Nilivyoona furaha ya wajumbe wa ZNZ waliotoka CAF na kusikia maoni yao walipohojiwa na waandishi wa habari, bila shaka ndugu zetu wazanzibari muungano hawautaki ila wamebanwa na wapo katika muungano kwa kushurutishwa.

Kwa wazanzibari kwao kuwa mwanachama wa CAF na kisha FIFA wakifanikiwa itakua ni ushindi mkubwa sana katika kudai sovereignty yao.

Kutokana na mazingira na kauli mbalimbali za viongozi wao wa upinzani na chama tawala, bila shaka Tanganyika tunawahitaji zaidi Zanzibar kuliko wao wanavyotuhitaji. Nimetembelea ZNZ zaidi ya mara kumi, wazanzibari muungano hawautaki. wanaosema wanautaka muungano wanadhihirisha vinywani tu ili kuungamkono msimamo wa chama chao CCM ila na wao ndani ya mioyo yao msimamo wao ni tofauti, hawataki kuonekana wasaliti.

Naamini uhuru wa kutambulika ktk michezo kama nchi huru ni ushindi na hatua kubwa kwa wazanzibari. Sasa wanajipa moyo kupata uhuru wa kisiasa, kukiwa na tume huru ya kusimamia uchaguzi na demokrasia ya kweli bila kutumia nguvu za kijeshi, wakiulizwa kuhusu muungano bila shaka ndio utakua mwisho.
Hata umeme hawalipi kwa makusudi ili wakatiwe wapate sababu ya...
 
Back
Top Bottom