Zanzibar ikijitenga Madeni ya Tril 23 yatalipwa na nani?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Najiuliza hili swali mwenye jibu atanisaidia.

Madeni yanayojopwa nje ya nchi yanakopwa kwa mgongo wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ushahidi mojawapo hata chenji ya rushwa ya rada wazenji wanaitaka kwa kuwa ni ya muungano.

Sasa ikitokea wakajitenga yaha madeni yaliyokopwa kwa miaka saba ya Jk yatalipwa kwa ushirikiano huo huo na Zanzibar na Tanganyika??
 
..madeni yatalipwa na Tanganyika.

..deni la tanesco tu linawashinda, sembuse hayo ya nje??

..nyinyi msitafute kisingizio cha kubakia kwenye muungano.

..hatutaki serikali 3, hatutaki mkataba, LET ZANZIBAR GO!!
 
No way, lazima Zanzibar wabebe mizigo yao.

Jambo la kwanza, siku viongozi watakapokaa kuandaa dondoo za mkataba wa kuvunja Muungano, Zanzibar wabebe madeni yao yote tangu 1964.
 
Zanzibar ina Population ndogo ambayo portion yake kwenye hili deni nayo ni ndogo sana.

Labda hata katika 22Tril, zanzibar ikawa ina < 100mil.
 
Najiuliza hili swali mwenye jibu atanisaidia.

Madeni yanayojopwa nje ya nchi yanakopwa kwa mgongo wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ushahidi mojawapo hata chenji ya rushwa ya rada wazenji wanaitaka kwa kuwa ni ya muungano.

Sasa ikitokea wakajitenga yaha madeni yaliyokopwa kwa miaka saba ya Jk yatalipwa kwa ushirikiano huo huo na Zanzibar na Tanganyika??

Watalipa 4.5% ya madeni, si ndio wanachopewa....!!!
 
Nisingependa Muungano uvunjike, lakini ikitokea hivyo cha kufanya ni kuangalia na kufanya mambo yafuatayo:
- Kuangalia madeni hayo yameanza lini mwaka hadi mwaka, bila ya kusahau kuwa mwaka 2006 TZ ilisamehewa madeni yote ya nje na IMF,
- Kujua ni deni gani la sekta ya umma (deni la sekta binafsi watajijua wenyewe),
- Kuangalia Zanzibar imekuwa ikichangia kiasi gani katika JMT,
- Kuangalia Zanzibar imekuwa ikipokea kiasi gani cha "Misaada"
- Kuangalia katika madeni hayo Zanzibar ilipewa kiasi gani (hapa ni kuepusha ile kuwa deni ni la Tanzania nzima lakini pesa zimetumika upande mmoja, iwe Makunduchi au Nachingwea, iwe kwa sherehe za mapinduzi au kwa famous sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Taznania bara.

Baada ya kujua yote hayo, kila mmoja "akitapike" alichokila.
 
Back
Top Bottom