Zanzibar Hakuna CCM, Kuna Wahafidhina Wanatapia Roho tu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Hakuna CCM, Kuna Wahafidhina Wanatapia Roho tu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Oct 8, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Jabir Idrissa
  WAHAFIDHINA wa Zanzibar wamechomwa miiba mioyoni. Hawataki kusikia madhambi ambayo kufanikiwa kwake kuna maslahi makubwa nao.
  Hawataki mjadala wa matatizo yanayokabili uandikishaji wapiga kura. Labda wanajua ukitendwa kwa haki wameumia. Wanaogopa chama chao – Chama cha Mapinduzi (CCM) – kitaanguka. Wanajua kinaangushika.
  Tulikuwa kwenye ukumbi wa Mlingotini, katika Hoteli ya Mazsons, ndani ya Mji Mkongwe. Waliotukutanisha ni Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Centre for Democracy (TCD) – ili kujadili matatizo hayo.
  Mada iliyoandaliwa, "Demokrasia, Uandikishaji wa Wapiga kura na Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi" nimeipenda. Ni nzuri iliyokuja kwa wakati muafaka.
  Uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) la Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 wa kuchagua rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani Zanzibar, umekumbwa na masahibu.
  Umekabiliwa na shutuma na lawama. Maelfu ya wananchi wanalalamika kunyimwa haki ya kuandikishwa. Maana yake watakosa kupiga kura.
  Wanalalamikia kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi. Kwamba ndiyo tatizo la wao kukosa haki yao. Wengi wao wamenyimwa licha ya jitihada zao za kukiomba kwa wanaohusika. Hakuna anayewajali bali wanalaumiwa ni wakorofi.
  Sheria ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 1985 inashurutisha mtu kuwa na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi ndipo aandikishwe kupiga kura.
  Kitambulisho hiki kinachomaliza muda wa kutumika Agosti mwakani, kinatolewa kibaguzi; wengi wanaostahili kupewa, hawapewi. Bali wapo wasiostahili wanafuatwa nyumbani kulazimishwa wasajiliwe ili wakipate.
  Wazanzibari wanaokataliwa kitambulisho wanaishia kudhalilishwa na kujeruhiwa kwa mabomu ya machozi yanayorushwa na askari polisi. Wakirudi makwao, wanakuta nyumba zao zimechomwa moto, mazao yao shambani yameteketezwa. Wanafunguliwa mashitaka mahakamani.
  Tatizo sugu la Zanzibar wakati wa uchaguzi ni wananchi wengi kuwa katika upande wa kukosa. Watahangaika kwa nguvu nyingi na kupoteza muda mwingi kutafuta haki yao, lakini wanaishia kudhalilishwa.
  Wakati Mkurugenzi wa Idara inayotoa vitambulisho, Mohamed Juma Ame anaendelea kusema ametoa vitambulisho kwa watu 503,895; maelfu ya wananchi wanakusanyika vituoni na kwenye ofisi za idara hiyo kuomba vitambulisho.
  Sasa kuna ushauri wa wadau kwamba mkurugenzi aende majimboni na orodha ya aliowapa vitambulisho, aite kimoja kimoja na kuangalia nani atajitokeza.
  Wadau wanasema kwa yule atakayebainika amepata kitambulisho na bado anadai kingine wakati hakuna taarifa kituo cha polisi kuwa amepoteza kitambulisho alichopewa awali, ashitakiwe mahakamani.
  Lakini kwa vile vitambulisho atakavyobaki navyo, basi watafutwe wenyewe kupitia taarifa za uongo walizotoa ili nao washitakiwe kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha kitambulisho. Kutoa taarifa za uongo ili mtu apate kitambulisho ni kosa la jinai.
  Angalau mkurugenzi amesema jambo moja zuri. Kwamba ofisi yake na hasa ofisi zilizoko wilayani, hazina uwezo wa kusajili watu kwa mkumbo. Vizuri.
  Kinachotakiwa siyo kuwapuuza watu wanaotaka kitambulisho, bali ni kuwaandalia utaratibu mwanana ili wasajiliwe na kupewa kitambulisho maana, ni haki yao kwa mujibu wa sheria. Kama kweli serikali ina nia njema, ihakikishe hakuna anayekosa kuandikishwa kupiga kura.
  Kwa jumla, uandikishaji wapiga kura unachechemea tangu ulipoanza 6 Agosti majimbo la Mkoa wa Kaskazini Pemba. Baada ya watu kuona hawaandikishwi kwa kukosa kitambulisho, wamehamasishana.
  Wamegoma. Wanafika vituoni kuzuia wachache wenye vitambulisho nao wasiandikishwe. Wanatuhumu kuwa baadhi yao wamo wanachama wa CCM ambao walipewa vitambulisho bila kikwazo chochote. Wapo pia wachache hawana sifa za kupatiwa kitambulisho, wamepewa. Wenyeji wanasema "Haiwezekani waje kuingizwa katika daftari."
  Katika jimbo la Tumbatu, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wananchi bila ya kujali vyama vyao, na wamegawika katika CCM na CUF tu, wamegoma hawaendi kuandikisha, ingawa wana sababu nyingine wakiilaumu serikali kwa kuwapuuza kwa muda mrefu.
  Haya ni mambo ambayo wahafidhina hawataki kuyasikia yanajadiliwa hadharani. Basi wakawa wamejipanga kuvuruga kongamano la TCD. Mwenyezi Mungu alililinda na lilimalizika salama.
  Hafidh Ali Tahir, mbunge wa Dimani, alianza. Kabla ya mjadala kuanza, aliomba kutoa taarifa. Alikubaliwa. Akasema haelewi TCD ina mamlaka gani ya kujadili masuala ya uandikishaji wapiga kura.
  Isitoshe, maazimio baada ya mjadala yatapelekwa wapi kwenye mamlaka ya kuyatafuatilia. Akaiponda mada, muwasilishaji wake na TCD wenyewe kwamba wamepotoka kwani majadiliano hayatakuwa na maana yoyote maana walioshutumiwa hawapo kujitetea.
  Akadai waitwe na kuruhusiwa kutoa mada yao, ndipo mjadala ufanyike. Hafidh, mwanasoka na mwamuzi wa kimataifa mstaafu, alimrukia muwasilishaji mada, Salim Said Salim, mwandishi wa habari mwandamizi nchini akiwa amefanyia kazi vyombo vya kimataifa, eti ameegemea upande mmoja wa kulaumu serikali.
  Akapata wenzake. Akaja Ussi Yahya Haji, mbunge wa zamani wa Chaani. Sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM. Akaunga mkono hoja hiyo na kumpa Salim majina.
  Wakaibuka wengine kama walishakubaliana kugomea mjadala na kujitahidi kuuvuruga si hivyo watoke. Akaja Ali Suleiman Ali (Shihata), mwakilishi aliyetoka Mikunguni na kuingia jimbo la Kwahani, ambalo katika uchaguzi uliopita, lilikuwa na kufuru katika uvurugaji kwani kura zilizopigwa zilipita idadi ya walioandikishwa.
  Akapinga mada na mtoa mada. Akadai viongozi wa CUF wanavunja sheria kwa kuhamasisha wananchi wasiende kujiandikisha. Alisema hilo lazima lisemwe hadharani.
  Akaja Yussuf Mohamed Yussuf, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, na mbunge wa zamani wa Mwembemakumbi. Akatoa ya kwake ya kuunga mkono hoja ya Hafidh. Alimbomoa Salim akimuita ni mtu wa upinzani.
  Akaja Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz akamkosoa mtoa mada; Ali Mzee Ali, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi na Mjumbe wa NEC hakubaki nyuma akasema kupinga mjadala kuanza.

  Akaja kijana wa CCM, Matogo Juma Matogo, akapinga naye na kuhimiza sheria zifuatwe katika kila jambo. Hao ni wanasiasa. Uvumilivu ulimshinda hata ofisa mwandamizi katika serikali, Mohamed Juma Ame. Akalalamika mada imepotosha ukweli wa mambo kuhusu vitambulisho. Akahofia mjadala wa mada utakuwa ni kupoteza muda.
  SOURCE: MWANAHALISI.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mbunge wa Dimani, Mh. Hafidh Ali Tahiri, Mwakilishi wa zamani wa jimbo la Miembeni "mtaa wa mateja", kashindwa hapo kufanya lolote na yupo bungeni hakuna linalofanyika kwa zanzibar wala kwa jimbo lake "jipya", Yeye na mwenzake Dr.Mwinyihaji, wapo kuganga njaa zao tu, Dimani ipo ipo tu, hawana wanalofanya yale mazuri wanayofanya wananchi kwa juhudi zao wenyewe baada ya kukata tamaa na viongozi wao, ambao hawapiti hata kuwajuulia hali mpaka uchaguzi, pia wanazifisidi nguvu zao, kuna asasi ya kirai ilianzishwa na vijana wasomi wa Dimani kwa kuchangishana senti zao wenyewe mifukoni kusaidia wananchi wenzao pale wanapoweza hasa maeneo ya elimu na afya, si Hafidh Ali wala Mwakilishi wake aliyewaunga mkono, kamwe Mh. Mwakilishi alifika mbali kutaka jumuia hiyo isisajiliwe eti ina mpango wa kutaka kum'ngoa katika "jimbo lake" kwa kuandaa mtu wa kumpinga uchaguzi ujao. Leo Hafidh Ali anapata wapi ujasiri wa kuitetea tume na idara ya vitambulisho isisemwe...wakati hawezi hata kusemea shida za wananchi wake...au walau kusaidia kwa hali kuwapa msukumo pale wanapojiinua kwa nguvu zao?
  Mwisho wao unakaribia wakitaka wasitake.
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huko Zanzibar ni vurugu tupu na CCM wala hawaoni aibu ya mambo wanayoyafanya!Hivi Wazanzibari hawachoki kunyimwa haki zao kila leo na kuwekwa nyuma ya pazia??????
  Zanzibari hamna wanamapinduzi wa kweli???Basi baadhi yenu wawe sacrificial lambs walete vurugu mmwage damu ili kuvuta world attention!
  probably ndio mtapewa haki zenu baaad ya dunia kuwatolea macho!
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hilo sio kubwa lakini watu hawataki wafike huko,watu weusi tutazidi kudharaulika.
  Soma hii habari halafu jiulize kisha utafakari kwa kituo.

  BLACK PEOPLE, PLEASE, READ & HEED. POIGNANT!!!
  The sad thing about this article is that the essence of it is true. The truth hurts. I just hope this sets more Black people in motion towards making real progress.. Chris Rock, a Black comedian, even joked that Blacks don't read.
  Help prove them wrong! Read and pass on.
  Please Note:
  For those of you who heard it, this is the article Dee Lee was reading this morning on a New York radio station. For those of you who didn't hear it, this is very deep. This is a heavy piece and a Caucasian wrote it.
  Dee Lee, CFP
  Harvard Financial Educators

  Dee Lee
  THEY ARE STILL OUR SLAVES
  We can continue to reap profits from the Blacks without the effort of physical slavery. Look at the current methods of containment that they use on themselves: IGNORANCE, GREED, and SELFISHNESS.
  Their IGNORANCE is the primary weapon of containment. A great man once said, 'The best way to hide something from Black people is to put it in a book.' We now live in the Information Age.. They have gained the opportunity to read any book on any subject through the efforts of their fight for freedom, yet they refuse to read. There are numerous books readily available at Borders, Barnes &Noble, and Amazon.com, not to mention their own Black Bookstores that provide solid blueprints to reach economic equality (which should have been their fight all along), but few read consistently, if at all..
  GREED is another powerful weapon of containment. Blacks, since the abolition of slavery, have had large amounts of money at their disposal. Last year they spent 10 billion dollars during Christmas, out of their 450 billion dollars in total yearly income (2.22%).
  Any of us can use them as our target market, for any business venture we care to dream up, no matter how outlandish, they will buy into it. Being primarily a consumer people, they function totally by greed. They continually want more, with little thought for saving or investing.
  They would rather buy some new sneaker than invest in starting a business. Some even neglect their children to have the latest Tommy or FUBU, And they still think that having a Mercedes, and a big house gives them 'Status' or that they have achieved their Dream.
  They are fools! The vast majority of their people are still in poverty because their greed holds them back from collectively making better communities.
  With the help of BET, and the rest of their black media that often broadcasts destructive images into their own homes, we will continue to see huge profits like those of Tommy and Nike. (Tommy Hilfiger has even jeered them, saying he doesn't want their money, and look at how the fools spend more with him than ever before!). They'll continue to show off to each other while we build solid communities with the profits from our businesses that we market to them.
  SELFISHNESS, ingrained in their minds through slavery, is one of the major ways we can continue to contain them. One of their own, Dubois said that there was an innate division in their culture.. A 'Talented Tenth' he called it. He was correct in his deduction that there are segments of their culture that has achieved some 'form' of success.
  However, that segment missed the fullness of his work. They didn't read that the 'Talented Tenth' was then responsible to aid The Non-Talented Ninety Percent in achieving a better life.. Instead, that segment has created another class, a Buppie class that looks down on their people or aids them in a condescending manner. They will never achieve what we have.. Their selfishness does not allow them to be able to work together on any project or endeavor of substance. When they do get together, their selfishness lets their egos get in the way of their goal Their so-called help organizations seem to only want to promote their name without making any real change in their community.
  They are content to sit in conferences and conventions in our hotels, and talk about what they will do, while they award plaques to the best speakers, not to the best doers. Is there no end to their selfishness? They steadfastly refuse to see that Together Each Achieves More (TEAM).
  They do not understand that they are no better than each other because of what they own, as a matter of fact, most of those Buppies are but one or two pay checks away from poverty. All of which is under the control of our pens in our offices and our rooms.

  Yes, we will continue to contain them as long as they refuse to read, continue to buy anything they want, and keep thinking they are 'helping' their communities by paying dues to organizations which do little other than hold lavish conventions in our hotels. By the way, don't worry about any of them reading this letter, remember, 'THEY DON'T READ!!!! (Hawajifunzi)
  (Prove them wrong. Please pass this on! After Reading
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hivi vibabu vinavyojiita "wanamapinduzi" vikitoweka vyooote Zanzibar itakuwa afadhali kidogo, watu hawapati kujinafasi kwa karaha zao, kwani vimebaki vingapi vile, mtu anikumbushe?
   
 6. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mwenyezi Mungu alisema aliyesoma na asiesoma jee ni sawa ?Ukweli hasa Hafidh ali hana Darasa na ukitaka kulijuwa hilo fuatilia hata maelezo yake kuhusiana na elimu ni mzushi na mzandiki mmoja .
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Junius ukisubiri eti unaowaita vibabu vya mapinduzi viondoke unakosea. Wakiondokahao wanakuja watoto wao na watafuata wajuu walioandaliwa. Dawa ni kuzidisha mapambano na CCM ing'olewe madarakani, uchaguzi wa Zanziba ukianyika kwa haki CCM inaanguka na kupotea kabisa, manake hata Unguja wataambulia Wawakilishi wachache.
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hakika dhulma na batili hazi wezi shind haki.

  jamani lazima viongozi wajue kuwa Mungu yupo na kesho siku ya hukma ipo Je mtasemaje.

  Tujue kuwa Allah amesema" Mtaulizwa neema zote mlizopewa mlizitumiaje"
   
 9. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi wewe hujui kuwa hivyo Vibabu-wajukuu zao pia ni wana-Mapinduzi. Na MAPINDUZI DAIMA. Wacha ndoto za Nchana hizo!!!!!!!!!!
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pakacha, najuwa lakini hawa wote i.e, vitoto na vijukuu vya wanamapinduzi, wameshajionyesha wazi kuwa hamna kitu kichwani, hawawezi kufikiri kwa vichwa vyao(lack of independent mind),wanategemea kubebwa bebwa tu, kusukumwa sukumwa tu,kudekezwa dekezwa tu...mpaka lini...watu weshajifunza kutoka kwa Amani Karume,unakumbuka alipotangaza kugombea urais siku zile...wananchi walikuwa na matumaini sana na yeye, wakaona alau huyu atakuwa kama baba yake na atafanya kama baba yake...lakini wapi...imekuwa yale yale...CCM wakisimamisha jiwe na wapinzani wakisimamisha mtu...ukhiyari kuchagua hilo kumbi la CCM kuliko wapinzani. Pakacha, haya hatuyataki tena, wakati unakuja ambapo vijana wa kizanzibari watakwenda kumpigia mtu kura on merit na si kwa kuwa baba yake alikuwa sijuwi...mwanamapinduzi...sijuwi nani...na hao wote unaowaita...wajukuu wa mapinduzi...wameshajionesha kuwa vichwa vyao vitupu...hakuna mwenye haja nao...labda washinde kwa ushindi wa 'kishindo' au 'tsunami'
   
 11. M

  MLEKWA Senior Member

  #11
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazanzibari inabidi wajifunze kwa Kitwana Kondo kwani uchaguzi ujao Wailsamu wa Tanganyika hawaangalii CUF au CCM au Chadema bali Mgombea ukitoka Kigamboni wanaharakati wanakuja Kigamboni kuuliza wewe na Uislamu wako na vipi utawasaidia Waislamu na hapo misikiti yote ya Kigamboni itaambiwa ichange pesa kukusaidia Muislamu Mwenzao na kuhakikisha Kampeni inafanyika ndani ya Misikiti na kuhakikisha Kura zote za Waisalmu zinakwenda Kwa Hassan au Hessein sio John , au Joseph, na nyinyi Wazanzibari si muna Jumiki tumieni hii kusimamisha wagombea wenu wenye ajenda zenu za siri ndani ya vyama vyote vya CCM na CUF mulete Mageuzi huko kwenu visiwani.
  Angalieni hawa Shura ya Maimamu wako chini ya Kitwana Kondo na wako Tanganyika yote kuanzia Kigoma mpaka Mtwara kuhakikisha Waisalmu na wao wanapata nguvu ya Dola.
  Waislamu wameivamia CCM ndio Wakristo wengine wakawa wanakimbilia Chadema kwa makundi.
  Wenu
  Mjomba Mloka , Gairo.
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Loh kwa hesabu ni wachache sana lakini wako wengi wanaojibatiza 'Uwana Mapiduzi' wanaodai wamerithi kwa wazee wao hata kama wamehamia visiwani miaka ya Karibuni.
  Tatizo ni kuwa Uwanamapinduzi bado ni ulaji wa bure bila jasho mradi tu uwe tayari kusahau utu na ubinaadamu ambao Wazanzibari wa kweli wamezaliwa nao. Hali inatisha!
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Hello Pakacha,
  Unapoainisha Mapinduzi Daima unakusudia kipi kimojawapo. jee ni matunda yaliyoletwa na Mapinduzi au mauwaji na ubaguzi ulioletwa na Mapinduzi hayo?
  Kama unazungumzia mema yaliyoletwa na Abedi Karume baada ya Mapinduzi basi umekosea kwani hivi sasa mema yote hayapo, elimu ni ya kibaguzi na ya malipo, maji ya kulipia, afya isiyoeleweka na umoja wa Wazanzibari uliokuwepo wakati wa Karume haupo, sasa Udaima unaousema upo wapi?

  Ama kwa kwa upande mwengine ni aibu kuwa nyie mnaodai Mapinduzi daima mnapotosha malengo ya Mapinduzi kwa kujifanya kuwa ni Masultani kwani hamko tayari kuona demokrasia inafanya kazi yake. Unyanyasaji. ubaguzi na kutumia nguvu kumwaga damu ndiko mnakokufanya kuwa ndio lengo la Mapinduzi.
  Mwisho wa siku Mola bado ni tegemeo la Wazanzibari kwani si waliweza kumuondowa Sultani wa Kiarabu kwa silaha dhaifu? Basi na nyie si tofauti kwa Mola na iko siku atasema basi na itakuwa hivyo si vyenginevyo.
   
Loading...