Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Hali ni tete sana ndani ya kambi ya CUF, wanatuhumiana tu. UHAI wake uko mashakani, unatembelewa na mauti, au wengi kuhamia ADC.
Ni kutokana na muelekeo wa chama baada ya kugomea uchaguzi wa marudio. Wengi wameona kuwa CUF kama ingeshiriki uchaguzi ingelikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuinyanyasa CCM ndani ya BLW na serikali ya SUK.
Kwa vile CUF wanaamini kuwa viti vyote vya PEMBA na viti visiopungua vitano UNGUJA vingeangukia CUF isipokuwa nafasi ya Urais tu ambayo CCM ingetumia nguvu za ziada ya kuitwaa nafasi hiyo.
Hivyo wanamwita Katibu wao Mkuu ni fisadi na mbinafsi anae fikiria maslahi yake tu na kuyaweka rehani ya wanasiasa wenzake. Maalim anajilabu kuwa yeye stahili zake zote anazipata. Wawakilishi wake wanakufa njaa! Wengine wana kwenda mbali zaidi wakimtuhumu kwa amenunuliwa.
Lakini wengi si kidogo wanasema ni radhi na mizimu ya Hamad Rashid ndio inayomtesa Maalim Seif kwa kumdhalilisha kisiasa na kumpangia njama za kumfukuza chama bila ya hatia.
CUF bara imeshtuka na kampeni za wazi zinafanywa kumrejesha Pro. Lipumba ili akiokoe chama kisiparaganyike bara. Wengi wanaamini kuwa Pr. Lipumba alijiweka pembeni baada ta kutalahifiana na Maalim Seif kuhusu kupatikana kwa mgombea wa uris UKAWA.
Mzozo huu pia unaathiri kwa kiasi fulani ngome ya CCM Zanzibar kwa kutomuamini Hamad Rashid na kujikumbusha na mithali ya KIPEMBA inayosema "mpemba fyoko ni sawa na kinyesi cha ngombe, utakiona kikavu juu lakini ndani ni kibichi"