Zanzibar bora ingeungana na Mombasa kwa kuwa tamaduni zinafanana sana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Khalifa Said mmoja ya waandishi huru ambaye amekuwa akindikia magazeti mbalimbali ya nje. Amekuwa na mtizamo tofauti kuhusiana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwa wengi nadhani mmekuwa na Ufahamu hasa wa tamaduni za Mombasa ikiwepo moja ya Ukarimu kwa wageni pasipo kujali jinsia zao.

Watu wa Bara kwa ukarimu kiukweli wana ubaguzi kiasi flani.mwanaume anaweza mkarimu mwanamke mgeni hata kama hajawahi mwona/ndo mara ya kwanza kumwona. Lakini kwa mwanahme mwenzie ikawa ngumu.

Mombasa mji ulioko Pwani ya Bahari ya Hindi si ajabu kwenda kula sehemu au kununua kitu na mtu akajiwa na hamu ya kukulipia.utakapotaka kulipa utaambiwa "yakhe ushalipiwa"

Huu ni utamaduni wa Ukarimu ambao pia upo sana Zanzibar.na kwa maelezo ya mwandishi huyu anasema ni mara 100 zanzibar wangejiunga na Mombasa.Si Tanganyika.

Lakini pia kwa utamaduni wa mapishi,mavazi na hata lugha. Mombasa na Zanzibar kuna mfanano mkubwa sana kuliko Bara. Nami naunga mkono maana nmeshafila sana Mombasa na Zanzibar pia.

Wanachakula kinachofanana.ni wajuzi wazuri wa mapishi.siku ya mwanzo kufika Mombasa nlidhani tumepitia Zanzibar kwanza.... Vyakula kama pilau,biriani,urojo n.k vilikuwepo kwa wingi sana.mapishi ya samaki mbalimbali na matumizi ya spices...nliburudika sana na vyakula vya huko tofauti na Nairobi.

Wapenzi wa Mombasa wanapenda Taarabu na ktk hili nikakumbuka waimbaji kama Maliki Star wa miaka ile ya nyuma. Nani asiyemfaham Siti na Bi kidude wa Zanzibar?ile taarabu asili acha hizi za akina Marehemu Nasma Kidogo au Khadija Kopa.

Lugha au kiswahili cha Mombasa ukimsikia mtu azungumza utapenda aendelee kuzungumza kwa nama ya matamshi yake na maneno ambayo ni tofauti na yanayotamkwa huku na wasukuma,wanyakyusa na wajita.

Mombasa wao watamka kwa ulaini sana na pasipo mikwaruzo au mgandamizo wa maneno.kama zanzibar tu... Wala hawatumii nguvu.utasikia "kufungwa tumefungwa lakini chenga twawala"

Ndio maana Khalifa Said anaona ni vyema Zanzibar ingeungana na Mombasa kuliko bara. Nami nasema nimefika kote huko. Yupo sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom