ZANTEL WANATUIBIA KWA KISINGIZIO CHA UBOVU WA MTANDAO.

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
17,057
18,406
Mimi mteja wa kampuni ya simu ya Zantel nasikitishwa sana na hii mbinu ambayo hii kampuni ya mawasiliano wanayoitumia kuibia wateja. Ukituma hela kwa ezypesa wao hukata salio lako halafu hukwambia hela haikwenda kwa sababu ya tatizo la mtandao na watakurejeshea hela yako. Tatizo hawakwambii watarejesha lini na kukutaka uwe mstahimilivu.Sasa ni siku 15 toka nianze kustahimili na hakuna jibu lini watarejesha na hawataki kutoa ushirikiano kwa sisi tunaohoji tutarudishiwa lini fedha zetu. Naomba TCRA waangalie hii kampuni maana huu ni wizi. Kukaa na hela ya mteja hadi tatizo lake liishe ni wizi na nawaomba wale wanaotaka kujiunga na huu mtandao waachane na hayo mawazo.
Karibuni mliokumbwa na tatizo hili kwenye huu mtandao ovu wa ZANTEL.
NB: kama ZANTEL mnadaiwa msitumie ezypesa kulipa madeni yenu.
 
Hivi bado wapo? Hawa walikimbia Dodoma wakatuacha yatima na SIM card zao tukaishia kupata hasara za kimawasiliano. Hawafai kabisa
 
Mimi mteja wa kampuni ya simu ya Zantel nasikitishwa sana na hii mbinu ambayo hii kampuni ya mawasiliano wanayoitumia kuibia wateja. Ukituma hela kwa ezypesa wao hukata salio lako halafu hukwambia hela haikwenda kwa sababu ya tatizo la mtandao na watakurejeshea hela yako. Tatizo hawakwambii watarejesha lini na kukutaka uwe mstahimilivu.Sasa ni siku 15 toka nianze kustahimili na hakuna jibu lini watarejesha na hawataki kutoa ushirikiano kwa sisi tunaohoji tutarudishiwa lini fedha zetu. Naomba TCRA waangalie hii kampuni maana huu ni wizi. Kukaa na hela ya mteja hadi tatizo lake liishe ni wizi na nawaomba wale wanaotaka kujiunga na huu mtandao waachane na hayo mawazo.
Karibuni mliokumbwa na tatizo hili kwenye huu mtandao ovu wa ZANTEL.
NB: kama ZANTEL mnadaiwa msitumie ezypesa kulipa madeni yenu.
Achana na huo mtandao wa kishamba, karibu chamani AIRTEL
 
Back
Top Bottom