Zantel Internet mmeanza ubabaishaji?

Zantel Internet mmeanza ubabaishaji?

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,767
Reaction score
20,869
Mi ni mshabiki mkubwa wa zantel hasa kwene upande wa internet. Kwa kipindi kirefu nimekua nikitumia modem yao ambayo kiukweli ilikuwa ikinifaa sana. Cha ajabu siku za hivi karibuni nimeanza kuona mabadiliko kwenye utendaje wa internet hii kwani mara nyingi hasa mchana napata spidi ndogo sana tofauti na mwanzo. Yaani napata around 2 - 30 Kbps na mara nyingi inakata kabisa. Zantel jirekebisheni au tutarudi kwenye cable sasa hivi!!
 
Kuna mdau kaniambia tangia jana mchana kuna matatizo mitandao karibia yote.., Mkonga kwenye maeneo ya Kibaha una matatizo ambayo wanayashughulikia.., Na hii ime-affect mitandao yote na sio Zantel peke yake

Hii ni kuanzia jana mchana ila kama issue yako imeanza kabla ya jana basi kuna tatizo (vipi umejaribu kuwapigia, dial 100) ingawa customer service yao huwa ni mbovu sitegemei jibu la kueleweka
 
Kweli kuna tatizo, juzi mimi nimeshindwa kabisa kutumia internet, hata kufungua e.mail inachukua muda mrefu sana zaidi ya dakika 12 na wakati mwingine inakataa kabisa.
 
ninatumia zantel ipo poa...labda inategemea na sehemu uliyopo.
 
hamieni vodacom
Hakuna cha mkongo kuharibika au "inategemeana na sehemu ulipo"
Voda mwendo mdundo tu.
 
mimi airtel cpati connection net siku ya tatu leo....
 
Hapa bongo kiukwel hakuna mtandao matata kila eneo ila kila mtandao unakuwa active na maeneo mengne huohuo unakuwa kilaza,mfan maeneo nilipo mimi mbabe wao ni airtel anafuata tigo,voda then zantel,bt unaweza tembea hatua chache unakuta mbabe anabadilika
 
Toka submarine cables zilipozingua kule baharini naona Zantel hawajarudi kwny kiwango chao,mimi pia ni mshabiki mzr wa Zantel cos hapa nilipo huwa ipo vzr lkn toka hayo matatizo yatokee leo siku ya 3 naona mambo si mambo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom