SoC03 Zamu yako sasa, fanya kwa moyo wako wote na kwa upendo mwingi bila malipo yoyote

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Ilikuwa usiku wa manane nikiwa nimelala ghafla nikapokea simu kutoka kwa mfanyakazi wa taasisi moja isiyo ya kiserikali ambayo mimi nilikuwa nikifanya kazi ya kujitolea akanambia”nipo mbali na wagonjwa wanapaswa kufanyiwa upasuaji katika kituo cha afya kwa haraka hatutaweza kupata damu usiku huu,kwani huu uvimbe wa mgonjwa kwenye mdomo itahitajika walau chupa sita O- na huu uvimbe wa kutoa manyama yaliyoota sehemu za mwili zitahitajika kama chupa nane za damu O+”

Kiusingizi nikaanza kutafuta taxify kwa njia ya mtandao kutokea nilipo mpaka kituo cha afya ni kama km 50, baada ya taxi kuja nikaanzia kwanza kumuamsha mkurugenzi kusudi anipatie nauli na namba za simu za watu wa damu salama kanda ,watu hao walinipa ushirikiano wa hali ya juu nikaenda kwenye benki ya damu nikiwa na manesi wawili wakiwa na deli la kutunzia damu, tukiwa damu salama kanda ya ziwa kwa idadi ya chupa tulizokuwa tunazihitaji ilikuwa ni vigumu kupewa zote kutoka kwenye kituo kimoja kwani grup hili la damu la O- ni grup adimu sana, akatupatia damu chupa mbili na akatuunganisha na watu wa Bugando kitengo cha damu nao walikuwa na wagonjwa ambao wanahitaji damu usiku huo na walibakisha chupa mbili tu za grup hilo la damu ,hivyo hatukufanikisha.

Tukaondoka hospitali ya Bugando kuelekea hospitali ya Sekoutoure, kwa bahati nzuri grup lile la damu walikuwa wanazo chupa sita na wenyewe wakatugaia chupa mbili na kuwasiliana na watu wa hospitali ya Nyamagana wenyewe wakawa hawana kabisa hilo grup la damu ila Ilemela walikuwa wanazo chupa nne za grup hilo wakatupatia chupa mbili za grup O- na za yule mgonjwa mwingine chupa mbili .Hivyo wagonjwa wawili zilikuwa zinahitajika chupa 14 za damu na sisi tulifanikiwa kupata damu salama chupa nane hivyo kupungukiwa chupa sita.

Ilikuwa karibuni saa 11 alfajiri tukiwa tunarudi kituo cha afya cha binafsi ambapo wale wagonjwa walikuwa wamelazwa wakisubiri kufanyiwa upasuaji na madaktari bingwa.

Usiku ule niliitumikisha akili yangu sana, nikifikiria namna nafsi yangu tu ambavyo huwa ni bishi katika kujihusisha na kuchangia damu, niliwaza sehemu ambapo miudombinu ni duni watu wakiishiwa damu kule huwa inakuwaje kwa haraka, au kama mtu mmoja anaongezewa chupa nyingi hivyo je ikikosekana hata kidogo si mtu anakufa.

MUNGU SI ATHUMANI, mgonjwa mmoja alipona hasa yule mwenye upasuaji mkubwa na mpaka leo bado yupo hai lakini yule aliyefanyiwa upasuaji sehemu za taya hakuweza kuishi si kwakukosa damu ila alifariki kwa njaa na kukosa hewa kwani baada ya kuwekewa mrija wa kupitisha chakula kwenye koo uliwahi kuziba na aliyekuwa akimuhudumia alipaswa autoe lakini kwa kutokuwa na taaluma hiyo aliendelea kuuchomeka ule mrija na mgonjwa akafariki kwa kukosa hewa.

Yule mgonjwa aliacha ujumbe kwa njia ya simu akimkabidhi mgonjwa mwenzie kwani wote walikuwa chumba kimoja na wote walifanyiwa upasuaji siku moja,ujumbe ulisema’’unavyobembelezwa kula halafu unakataa,mwenzio hapa naumwa njaa na hata sioni sehemu ya kukipitishia hicho chakula’’

Baada ya usiku ule kupita na asubui yote kushinda nimelala kwa uchovu ,ndipo nilipata wasaa Kwenda damu salama ten ana kuomba kujua nawezaje kuchangia damu na kuhamasisha wengine waweze kuchangia

MPANGO WA TAIFA KANDA tulikuwa na mazungumzo kama ifuatavyo:-

Apheresis ni nini?
Apheresis ni tekenolojia ya kuchangia aina moja au zaidi ya mazao ya damu kutoka kwa mchangia damu. Mazao haya ni kama: Chembe sahani (Platelets), chembechembe nyekundu za damu (RBCs) na Plasma. Teknolojia hii huruhusu kukusanywa kile ambacho wagonjwa wanahitaji na kurudisha damu iliyobaki kwa wachangia damu.

Usalama wa wachangia damu ndio kipaumbele. Mashine ya Apheresis huchakata damu ili kuitenganisha, huvuna mazaodamu yanayokusudiwa na kurejesha damu iliyobaki kwa mtu anayechangia damu.
Je, apheresis ni salama kwangu?

Ndiyo, uchangiaji kwa njia ya apheresis ni salama sana. Kila mchangiaji anaangaliwa kwa karibu na wafanyakazi waliofunzwa ambao huhudumia wachangia damu wakati wote wa zoezi la uchangiaji.

Je, kuna madhara yoyote wakati wa kuchangia damu kwa njia ya Apheresis?

Wengi wa wachangia damu kwa njia ya apheresis hawapati madhara wakati wa zoezi la uchangiaji damu. Wengine huhisi baridi kidogo au jambo ambalo si madhara makubwa na linaweza kudhibitiwa vyema na wataalamu waliofunzwa.

Vigezo vya uchangiaji wa apheresis
Vigezo vya uchangiaji kwa njia ya apheresis ni sawa na uchangiaji wa damu kwa niia ya kawaida. Mchaangia damu wa Apheresis lazima:

 Awe na umri wa miaka 18. hadi 65
 Kuwa na afya njema.
 Uzito usiopungua kilo 50.
 Kwa mchangiaji wa chembe sahani kwa njia ya apheresis, jumla ya chembe sahani kwa mchangiaji inapaswa kuwa zaidi ya 150 × 109/L.
 Kwa mchangiaji wa plasma ya apheresis, jumla ya kiwango cha protini cha mtoaji kinapaswa kuwa zaidi ya 60 g/L.
 Kwa apheresis ya seli nyekundu mbili, mchangia damu wa jinsia yoyote wanahitaji kuwa na kiwango cha chini cha himoglobini cha 14.0 g/dl (68% HCT)

Hali ya kiafya: Mchangiaji damu anapaswa kuwa na afya njema, asiwe na magonjwa kama vile kisukari, Shinikizo la juu la damu n.k, asiwe mgonjwa anayejulikana kuwa na VVU, Homa ya Ini B&C, Kaswende au maambukizi mengine yoyote yanayoweza kusambazwa njia ya damu kuongezewa damu.

Muda wa kusubiri kabla ya kuchanga tena: Mchangia damu anatakiwa awe ametoa awali kutoka miezi 3 au zaidi kwa wanaume na miezi 4 au zaidi kwa wanawake

Baada ya kujifunza kile nilichokuwa nakihitaji nikaanza kuwa mchangiaji damu mzuri na mhamasishajji mzuri juu ya masuala haya ya kuokoa Maisha, sikuishi hapo nikaanzisha clubs za damu.

TUNAWEZA KULETA MABADILIKO,
Juzi usiku nilienda duka la madawa kwa dharura,Mama wa makamo akaja akihitaji dawa ,niliona hakuwa na kiasi cha kutosha kununua dawa zile.

Pia alionekana masikini.Nikasema nitalipia kiasi cha elfu kumi kilichobakia.Lakini alikataa akasema yeye sio ombaomba. Nikamwambia huo sio msaada ila ni malipo ambayo atapaswa alipie kwa mtu muhitaji mwingine kwa baadae. Alitoa machozi kwani mumewe alikuwa hoi kitandani na hakujua angewezaje kukamilisha dawa zote.

Tafadhali nenda kabadilishe stori ya muhitaji ,inaweza ikawa wewe unafuatia au mtu wako wa karibu. SOTE TUNAUNGANISHWA NA DAMU,CHANGIA LEO ,CHANGIA MARA KWA MARA ,KWANI HAKUNA KIWANDA KINACHOZALISHA DAMU NI BINADAMU KWA BINADAMU MWENZIE ...NENDA KAOKOE MAISHA,KUWA SHUJAA.

DAMU HAINA CHEO, KABILA ,RANGI WALA JINSIA...

20230607_203907-BlendCollage.jpg
 
Back
Top Bottom