Suruali za jeans hazikuwepo kulikuwa na suruali za codrai na surual za mabuga luuu, ndo zilikuwa fashion.
Vijana mpooo....tupoooo ...tupo kabisa
jeuri ya chama...chini ya umoja wa vijana
yebaaa .....waaaa
mwenge huooo..mwenge...mbio...mbio
mwenge tunaukimbiza mbio..mbio
mpaka makao makuu mbio...mbio
ZAMANI KULIKUWA NA KAUZALENDO TOFAUTI NA SASA,
TULIKUWA TUNAJIPANGA BARABARANI KUMSUBIRI RAIS AKIPITA.
ILA SIKU HIZI WATU HAWANA UJINGA HUO.
Nondo mla watu, kibanga ampiga mkoloni, brown ashika tama
Kilimanjaro Hotel umenikumbusha zamani sana wakati bado nipo kinda tulikuwa tunapelekwa kuangalia mashindano ya magari Kilimanjaro Hotel ndio wanapomalizia mashindano yao kuna dereva mmoja anaitwa DUDU(Singasinga)Mnaikumbuka pool side kilimanjaro hotel
Ahante sana, miaka hiyoooo 80's.......
Kweli ilikuwa raha sana, hata vitabu tulivyokuwa tunasoma vya akina asha na rozi vilikuwa vizuri sana, yuo can't compare kwakweli...... "rafiki ni bora kuliko mwanasesere"
Somo la jiografia lilikuwa poa sana, by that time darasa la nne tu unaijua mikoa yote ya Tanzania, mkoa gani unalima mazao gani n.k sasa hivi sidhani kama watoto wanafundishwa hivi vitu.
Manjagata unakikukmbuka kitabu cha jiandae kumaliza elimu ya msingi, zile atlasi, ndani unakutana na Tanzania- sura ya nchi, yaakisha mambo ya tanzania, inafuata afrika mashariki, then afrika na mwisho dunia, mwanafunzi unaelewa kwa undani tanzania kuna nini, afrika mashariki kuna nini, afrika kuna vitu gani hadi dunia
Kwenye atlas umenikumbusha kitambo kweli kuna mchezo wa kutafuta miji tulikuwa tunacheza 'mtu anataja mji/sehemu wengine mnatafuta.'
ram usinikumbushe kabisa hizo enzi ilikuwa raha jamani! Vita tu ndo ilituharibia mambo kiasi kwamba maisha yakayumba, kabla ya hapo ilikuwa mteremko sana! Jiandae kumaliza ELIMU ya Msingi ilikuwa na maswali ya masomo yote! Ila wakuu darasa la kwanza miaka hiyo nilikuwa kilaza kweli, basi siku moja mwalimu akawa ameandika ubaoni "HILI NI CHANUO" na chanuo limechorwa hapo sasa ikawa ukitajwa unasoma hiyo sentensi. Ikafika zamu yangu bwana sasa kwa vile Mimi nilikuwa sijui kusoma, nikawa nimekariri, lakini katika kukariri kwangu nikawa nimejichanganya nikaongeza neno la kwangu nikasoma "CHANUO HILI HAPA" badala ya "HILI NI CHANUO" Weeeee nilioga viboko kama kibaka! Tangu siku hiyo haki ya nani nilikuwa moto chini ile mbaya!!Ahante sana, miaka hiyoooo 80's.......
Kweli ilikuwa raha sana, hata vitabu tulivyokuwa tunasoma vya akina asha na rozi vilikuwa vizuri sana, yuo can't compare kwakweli...... "rafiki ni bora kuliko mwanasesere"
Somo la jiografia lilikuwa poa sana, by that time darasa la nne tu unaijua mikoa yote ya Tanzania, mkoa gani unalima mazao gani n.k sasa hivi sidhani kama watoto wanafundishwa hivi vitu.
Manjagata unakikukmbuka kitabu cha jiandae kumaliza elimu ya msingi, zile atlasi, ndani unakutana na Tanzania- sura ya nchi, yaakisha mambo ya tanzania, inafuata afrika mashariki, then afrika na mwisho dunia, mwanafunzi unaelewa kwa undani tanzania kuna nini, afrika mashariki kuna nini, afrika kuna vitu gani hadi dunia
Wajanja wa mjini ilikuwa lazima ukariri zile aya za kitemi za Umsolopagaazi-Matibabu ilikuwa bure. Hospitali za binafsi hazikuwepo labda za misheni.
-Ukivaa chupi ilikuwa ni dili kubwa!
-Hakukuwa na skini taiti
-Viatu ilikuwa tunanunua Bora
-Nyumba 10 alikuwa anaheshimika kama hakimu. Ukigombana na mkeo anakwenda kushitaki na kulala kwa mjumbe
-Ukimwi ulikuwa hakuna zaidi ya kisonono na kaswende
-Wasichana wa kazi walikuwa bwerere siku hizi ni shida!
-Hakukuwa na magril kwenye milango na madirisha
-Nyerere alikuwa kama Mungu
-Kawawa alikuwa alionekana kama kichekesho kwa stori za "Kawawa funika kikombe"
-Tulifanywe tuamini kuwa Kambona ni adui wa nchi yetu na nyimbo tuliimba
-Wakati ule wanafunzi kwenda kufanya kazi za mwalimu nyumbani kwake ilikuwa ni heshima kubwa, sasa hivi ni kesi
-Mashairi ya "Karudi baba mmoja" na "Sizitaki mbichi hizi" yalikuwa kichwani kwa kila mwanafunzi
-Jioni zilikuwa ni nyakati za kupiga hadithi na vitendawili au michezo ya kujificha. Siku hizi ni kuangalia TV
Nitaendelea......
Sunday boogie pale Princess kila jpili lilkitumbuizwa na Safari Trippers wakiwa na Marijani Rajabu.Gateways palikuwa na The Sunburst.Zaman wale wa born town kucheki movie Avaron,Empress,New Chox au Drive Inn,wale wapenzi wa movie za kihindi Cameo ndio ilikuwa mpango mzima,kabla ya movie mangoma ya wanyamwezi yalikuwa yanapolomoshwa,wanyamwez kama wakina Billy Ocean,Cool n the Gang wengineo ndio ilikuwa stata kabla ya movie kuanza,da!miaka ile ilikuwa bomba kuwai kutokea katika maisha yangu na nina uhakika kwa wale vijana wa 90s na waliopitia viwanja vile,watakuwa wanamiss kipndi kile,da!kwa bahati mbaya vyote vimekufa.