Zamani ilikuwa raha

Hapa naahidi mbele ya chama-
cha mapinduzi nitakulinda mpaka kufa,
tumeachiwa jukumu la kukulea wewe.

Kumbuka mapinduzi bado mdogo,
wazazi wako wamefariki toka zamani......
............................................

Dah! unaimba kwa hisia zote za uzalendo. tehe tehe.....hakukuwa na tofauti kati ya chama na serikali
 
Four years!! Mkuu watu wame-date toka shule ya msingi hadi chuo kikuu na hawaoni ndani. Mchezo wanakuja kupewa siku ya ndoa (of coz hizi ni zile extreme cases lakini zilikuwepo za kutosha tu)

umenifurahisha
w
 

lakini hapo kwenye ndoa ilikuwa poa ndio maana baba na mama zetu mpaka leo wako pamoja
 

Mkuu hapa tunakelewa wachache, wengi ni St Emmy wanaona mauzauza tu, Asante kwa kutukumbusha.
 
Enzi hizo mipira ya Shule (za msingi) ilikuwa ikihifadhiwa kwa Mwalimu Mkuu. Watoto wake weekend wanajichukulia mpira nakucheza. Watoto wa wakulima wanawaogopa watoto wa walimu hata kugusa vitu vyao ilikuwa ni vigumu.
 
Reactions: awp
Imani ya TANU binadamu sawa, kila mtu aheshimiwe, ashiriki sawa katika taifa, Tanganyika ni nchi yetu. Siasa ya TANU hujenga Ujamaaa, nakusitiwisha raia, Usipojiunga na siasa hiyo wewe hujengi Tanganyika
 
tuliapishwa bila kujua ule wimbo wa-naapa naahidi mbele ya chama;pinduzi nitakulinda mpaka kufa najuta sana leo
mapinduzi nitakulinda ungali mdogooo
na wazazi wakoo wotee wamekuzaa wewee
 
Kumbukumbu zangu:

1. Disco Twiga, ghorofa ya tano, mtaa wa Samora.

2. DJ Kalikali (RIP) na nyimbo za breakdancing Rungwe Beach.

3. Kuogelea wakati wa sikukuu Afrikana. Tunawahonga Askari wa geti na kuingia na sufuria za pilau na chupa za mirinda moto. Nani anunue chakula bei za wazungu! Nakumbuka maandazi katika menu yao waliita " African cake".

4. Kuvaa Kaunda Suti na raizoni ya Bora ya ghorofa tatu.

5. Sinema za Bruce Lee pale Empire. Makarate yake yanakufanya usimame kitini na kushangilia.

6. Picha za kihindi Avalon. Picha refu sana lakini kuna intermission katikati. Tunatoka nje na kununua mishikaki na soda na kuendelea kuona katili amjad khan anavyopigwa na amita bachan.

7. Kutembea na gari jumapili kwa kubali. Barabara yote yetu!

8. Kuangalia picha nyumbani katika mkanda wa Betamax pamoja na majirani WOTE.

9. Kula chokleti ya "cadbury" kutoka Kenya na "Big G" na "orbit". Tunatafuna pole pole isiishe utamu.

10. Kuuza vyakula kwa "ration". Sabuni ya kuogea ni mbuni au ya misaada. Mafuta ni ya nazi. Peremende ni " pipi ya kifua ya bluu".

11. Kutumia simu ya Nokia ya "mkate".

12. Kujifunza kuendesha gari katika uwanja wa Lugalo, upanga.
 
yaani very interesting.......nakumbuka Chidya boys Masasi walikuwa wanaitwa mbwa mwitu coz shule yao ipo milimani
 
Duh asante sana mkuu umenifanya niione 1979 live nilipoenda kuandikishwa darasa la kwanza, wakati huo vita vya Kagera vinanguruma kuelekea mwisho. Yaani unapenda shule kwa moyo wote.
Wakati wa sikukuu za kitaifa chakula kinapikwa mnakula shuleni, duh those were the sweet days.
 

Mchakamchaka mnakimbizwa na mgambo huku mnaimba:

Jua lilee literemke mama; aiyaiya iya iya mama ...

Na ule wimbo mwingine wa Kambona ameolewa na Mwingereza mnaukumbuka?
Those days bwana, ilikuwa safi sana.
 

Miaka 50 ya uhuru::
Tumethubutu, tumejaribu, tumeshindwa, tujipange upya.
 

Carlos enzi zake na biashara ya unga. Nimesahau jina la kwanza.
 

Shule za Private zilikuwa za kanisa au jumuiya ya wazazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…