Jangwani sec partners wao Azania sec, Zanaki Sec vs Tambaza, ngoja itokee mechi ya basketball pale viwanja vya Zanaki kati ya Azania vs Tambaza ndio utaona raha yake.....kule boarding mitaa ya kaskazini Weruweru vs Ilboru, Umbwe or Old moshi, Kiraeni vs Killimanjaro boys/old moshi, Kibosho Girls vs Ilboru. Sekondari za Lyamungo, kibohehe na Kolila ilikuwa shida kupata parters kwa sababu ya fujo zao! Mlikuwa mkialikwa na Moshi Technical mnajua mnaenda kukutana na wakulima, hata kucheza walikuwa wanacheza ngoma za kienyeji badala ya muziki......wananuka vikwapa hasa.....Nakumbuka kuna siku tulialikwa Old moshi sec disco liishe saa sita usiku nasi tupande basi turudi kwetu, lakini mijamaa ikamnunulia bia dereva ikamnywesha akalewa halafu wakaiba funguo ya gari.....hatukuondoka mpaka asubuhi saa kumi na mbili ndio tunafika kwetu....usiulize yaliyotukuta!!!!!!
Hapo kwenye red ulionjapo mtete wa Msukuma?
Siku hizi ndo hamna raha wakati huo kila kitu kilikuwa kinasisimua kwani havikuwa vinapatikana kila mahali kama leo. Wali wa maharage ulikuwa mtamu kuliko chipis mayai/kuku leo, hata uji usio na chochote ulikuwa mtamu kuliko uji wa asali leo
Hata sasa ni raha.....isipokuwa raha za sasa zinategemea na kiwango cha uchumi au uwezo wako wa kujipendekeza kwa wenye nazo.......
na baada ya miaka 20 sidhani kama dunia itakua salama tena kuishi........zaman watu walikua happy san
Tuliapishwa bila kujua ule wimbo wa-NAAPA NAAHIDI MBELE YA CHAMA;PINDUZI NITAKULINDA MPAKA KUFA najuta sana leo
Mkuu shairi la karudi baba mmoja nililiimba nikiwa darasa la 4 mwaka 2000 ila shairi la sizitaki hizi mbichi sikubahatika emu weka mistari yake!
Kwenda sekondari
ilikuwa ni heshima kwa jamii inayokuzunguka. Wakati wa kwenda shule
husindikizwa na kundi la watu huku umesaidiwa sanduku. Tulipanda treni.
Tiketi tulitunza kwani nauli tulirejeshewa baada ya safari. Makonda wa
treni (tt) walikuwa ni wahindi.
Mwl.alipohamishwa shule ilipikwa pilau, pia mashairi yaliimbwa.
Picha tulipiga studio tena baada ya kusevu kwa muda mrefu.... Tofauti na
siku hizi ''selfie''.
Tulisikiliza RTD, kwa miziki idhaa ya biashara.
Range rover haikuruhusiwa ku paki benki. Peugeot 504 iliaminika ni gari
ya wahuni/majambazi.
Namba za serikali ilikuwa stb, stc, std, stg. Za wahisani ilikuwa tx -
plate number nyekundu.
Sikukuu ya saba saba ilifana sana kitaifa ilifanyika. Na mikoa mingine
ilishiriki pia.
Vitabu madaftari shule za msingi ilikuwa bure. Daftari likijaa unapeleka
kwa mwl.wa darasa anakupa jipya
ole wako karatasi zikutwe pungufu, viboko vilitawala mashuleni na
nidhamu ilikuwepo pia.
Wanafunzi shule ya msingi baadhi walikuwa wananyoa ndevu.
Itaendelea.
hizi hadithi zilikuwa zina mafunzo makubwa
nimewakumbuka Mr & Mrs Daudi, Baraka na Neema na Neema atakuwa ameolewa sasa
waliofeli ndio walienda private schools, ilikuwa aibu mtu kusoma pte school. leo ni sifa kusoma au kusomesha pte schools.
Mmhh those were good days when life style was contrary to the current one..you could use centi and shilling to buy all the basic needs and still get an extra money ...
Those were the days when dating someone's daughter for Four years and yet you couldn't get sex...ha ha haa