Zali la mentali, ushauri tafadhali

Zali la mentali, ushauri tafadhali

Ni matapeli hao! Usithubutu kutuma hta senti moja! Huyo unayemtaja alishanitumia email km zako hata mimi. Ukihitaji nikuforwadie nitakuforwadia. Kuna rafiki yangu pia alitumiwa email na huyu huyu anayejiita Michel. Mi nilishawajua kitambo coz sio mara ya kwanza kutumiwa email za namna hiyo. Wapo pia wanaojifanyaga wanaishi Senegal Refugee camp. Baba zao waliuawa na wakaacha pesa nyingi. Wanatumia triki ya kuwa wamefall in love na wewe. Wanakuomba uwape full details zako za bank. Baada ya hapo wanakwambia utume kiasi fulani cha pesa ili jaji aidhinishe hizo pesa ziingie kwenye account yako! Ukishatuma hizo pesa ambazo wanadai zinahitajika na Attorney General ili aidhinishe hiyo transaction WANAKATA KABISA mawasiliano na wewe unakuwa ushaibiwa!
 
hapo unapigwa zairi kuzaliwa mjini university hata kama hijasoma hata picha hahahahahahaha we kilaza
 
Haya mambo yapo sana kwenye mtandao na watu wengi sana washalizwa na kuibiwa hela kibao kutoka kwa hawa matapeli. Kama hela yako haina kazi tuma uliwe. Shtuka, kimbia haraka unatapeliwa.
 
huenda sio matapeli.. lakini kama kweli kulikuwa na nia ya kukutumia zawadi.. kusingekuwa na cost kabisa..
 
Kwanza email yako kapataje? Jiulize nakwambia hao ni matapeli shukuru Mungu upo jf na unapata ushauri kuna wengine kama wewe hawana sehemu ya kuomba ushauri na wanakurupuka na kutuma pesa .mijamaa inapiga pesa sio mchezo kwa tamaa. Acha tamaa kijana

Nashukuru mkuu ushauri wako ni busara sana hiyo ndiyo intellectual advice
 
Haya mambo yapo sana kwenye mtandao na watu wengi sana washalizwa na kuibiwa hela kibao kutoka kwa hawa matapeli. Kama hela yako haina kazi tuma uliwe. Shtuka, kimbia haraka unatapeliwa.

Nashukuru mkuu kwa ushauri wako
 
Zali lenyewe ndo hilo!!! Ptuuuu. By the way umeanza kutumia mtandao wa internet lini?
 
Hivi mtu yupo UK dollar 98 zitampeleka wapi jamani? Au ndio mafreeemason wenyewe hawa lol
 
Mtumie tu, hiyo zawadi ni kubwa sana hailingani na hiyo pesa.
 
Juzi nilitumiwa email na watu kama hao.. wanasema wako marekani..wakaniambia nimeshinda sijui kwenye nini $800,000.00 so wakasema nitume details zangu ili niclaim payment kwa branch officer wao hapo southAfrica..... sikujibu kitu
 
Utapeli wa 1999, we bado unaingilika. Pole
 
Hahahaha...ndo maana kakwambia hana bank account...maana jamaa yupo bongo na wala sio mwanamke....

Lakini huu utapele wakizamani sanaa...yaani mtu anunue zawadi zote hizo akose nauli ya kukutumia..basi atakuwa mjinga...!
 
Back
Top Bottom