Zakhia Meghji, Shamsa Mwangunga, Anne Makinda.....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zakhia Meghji, Shamsa Mwangunga, Anne Makinda.....!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by The Kop, Apr 15, 2011.

 1. The Kop

  The Kop JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 208
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  wasalaam wana JF...!
  Baada ya kufuatilia kwa umakini mkubwa mwenendo wa bunge la 10, tangu kikao cha kwanza hadi hiki kinachoendelea sasa hivi, imenifanya kurudisha fikra nyuma na kuwakumbuka wanawake walo shika nyadhifa za juu katika utawala wa JK. Tukianza na Zakhia Meghji, aliyepata kuwa waziri wa fedha na uchumi, tulishuhudia alivyokuwa "rubber stamp" ya kuidhisha wizi wa fedha katika akaunti ya EPA...alipohojiwa na waandishi wa habari kwanza, alikana kuhusika, alipobanwa kwa kupewa vielelezo alivyo sain alisema "wasaidizi wangu walinidanganya". Tukimgeukia Shamsa Mwangunga aliyekabidhiwa wizara ya maliasili na utalii, tulishuhudia jinsi shehena ya magogo na ilivyokuwa ikinaswa bandarini kwa kupitishwa isivyo halali. Yote tisa, funga kazi ni huyu ms Anne Makinda ambaye habari zinadai "alitongozwa" na RA ili agombee uspika wa bunge. Mama huyu analiendesha bunge kama familia yake na kuwabwekea wabunge hususan wa CHADEMA kama wajukuu zake, naogopa kama jamii za kimataifa wanaoliona bunge hili wakichukua taswira kwa kupitia spika huyu na wabunge wa "ndiyo mzee" wa CCM kuwa Wa TZ ndo tulivyo, unaweza kuona aibu kujitambulisha kuwa ni MTZ. Sasa swali la kujiuliza ni hili, hawa wa mama wanadhiirisha kwamba wanawake hawawezi...au wanatumikia mafisadi...? Je kuna haja ya kuwaamini na kuendelea kuwapa madaraka makubwa ikiwa ni pamoja na urais.....?
   
Loading...