Mama Ana Makinda asema Nyerere alitaka self made opposition. Aongelea hali mbaya ya uchumi 1983 na uenyekiti wake mali za wahujumu uchumi

Gebreyesus

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,585
2,000
Kwenye kipindi Cha TBC muda huu mdahalo wa uongozi mama Anna Makinda anasema yeye alikuwa na wenzake 20 ambao ni wapinzani bungeni na anasema walikuwa ni self made opposition. Na walikuwa wakali mpaka Nyerere aliahirisha Safari yake ya Ruvuma akafika bungeni akamwambia Cleopa David Msuya hawa wabunge wa mrengo wa upinzani ndio tunaoutaka, kwahiyo Nyerere aliona umuhimu wa upinzani. Vipi nyie CCM wa Leo kwanini mmeuwa upinzani? Kwa maoni ya mwalimu nyie CCM Leo mnafanya vibaya.

=========

Mama Anna Makinda: Mshahara wa Bunge ulikuwa 345, mshahara wa auditors kama sisi ulikuwa 1600. Nilipata tabu kufanya maamuzi, ikabidi nikubali kubaki Bunge na mshahara wa 345. Watu wakashangaa zaidi, huyu nae kichaa! Ameenda huko, Auditors hawaendagi huko! Lakini nilipata fahari kwa sababu nilikuwa naweza ile kamati yetu ya Bunge, wajumbe 12 na mtoto mdogo nilikuwa mimi na ninayejua masomo hayo kwahiyo nilifanya kazi very actively katika ile kamati.

Siku Mwalimu anamtuma mheshimiwa Butiku aje wanifate mimi niende kwa Mwalimu, mimi namwambia Butiku, mimi sijui Mwalimu anakaaga wapi! Huyu ananiuliza hujui Mwalimu anakaaga Msasani! Ikabidi anipe gari kutoka Ikulu yeye mwenyewe kunipeleka Msasani.

Kufika kule, Mwalimu anafika, eeeh Anna nataka utusaidie serikalini, kama nilivyosema Mwalimu hazoeleki lakini rahisi kumuelewa. Nikasema mbona mimi nafanya kazi kubwa sana, wakati ule decentralization ndio imeanza, watu walikuwa hawawezi kuweka vitabu vizuri, kwahiyo tukasema hao hatuwezi kuwapeleka kusoma lakini unaweza kuwafundisha on the field nini kilichokuwa kinatakiwa, kwahiyo tulikuwa na kaprogram. Nasema mbona nafanya, nakusaidia, mwalimu hakunielewa.

Nimerudi naendelea na mambo yangu, baada ya saa mbili naitwa tena, Anna umeshafanya uamuzi? Akasema mimi ni Rais, nenda tu. Usiku natangazwa kwenye redio eti mimi ni waziri.

Wakati wa Ubunge wetu, mimi nilikuwa 'notorious'. Katika wabunge waliotengeneza upinzani wa kujifanyia wenyewe, sisi tulifanya. Tulikuwa tunasema 'Self made opposition'. Tulikuwa wakali kweli kuliko hata wabunge hawa. Mimi nilikuwa nawaambia nyie hamna lolote, sisi tulikuwa tunafanya kazi ya opposition kwelikweli wala hatukutumwa na mtu.

Mpaka Mwalimu alikuwa na ziara yake Ruvuma, akafika mpaka bungeni, waziri mkuu alikuwa mheshimiwa Msuya, anasema 'Cleopa we want self made opposition'

Tukiwa chama kimoja mtabweteka, sasa hivi inakuja ile point hawa wako chama kimoja, anasema msipokuwa na kitu kama hiki, nyinyi mnabweteka. We need that group ya self, tulikuwa watu kama 20 hivi, sasa sisi ndio tunazinduka, kumbe kulikuwa kuna tatizo!

Tumewanyanyasa kwelikweli na ile sugar scandal, nikasema hapa shughuli kweli, waziri mkuu akawa Sokoine. Mimi niliingia uwaziri wakati hali ya uchumi mwaka 83 ilikuwa ni mbaya sana.

Kwahiyo kazi moja mimi ilikuwa kuratibu upatikanaji wa vitu mbalimbali na kuangalia upungufu maana ulikuwa upungufu wa everything almost.

Siku moja niko kanisani usiku ikaletwa gari, Sokoine alikuwa anakuita saa yoyote, ukienda unawakuta kina Butiku wako kikao full na majenerali wote hapohapo, naingia pale usiku hata sijaelewa.

Waziri mkuu ananiambia utakuwa mwenyekiti wa mali za wahujumu uchumi, kwanza zimetoka wapi hizo mali? (Anacheka).

Kwahiyo tumemsaidia sana Mwalimu, ilikuwa kipindi kigumu kwasababu kulikuwa na upungufu wa bidhaa karibu zote, walioweza kohodhi mali walihodhi, nchi ilikuwa hali ngumu, ukitaka sukari lazima foleni, unga hakuna, chochote hamna, mafuta hakuna, hela za kigeni hakuna. Tulishiriki mpaka kugawa hela za benki kuu.
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,653
2,000
Sikio la kufa halisikii dawa.

Hii nchi bora iuzwe kila mtu achukue chake, yaishe. Maana nchi imejaaliwa wendawazimu kuanzia viongozi mpaka raia. Raia wakiambiwa tanzania imeingia uchumi wa kati wanashangilia kwa vigelegele na vifijo kweli, haya sasa mmepandishiwa na "VIFURUSHI VYA SIMU KWA LEVEL YA UCHUMI WA KATI", mmepandishiwa na "BEI YA MAFUTA LITA ELF 5" mwende sawa na watu wa uchumi wa kati, shangilieni na hilo la uchumi wa kati wa vifurushi vya simu!!!!
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,291
2,000
Kwenye kipindi Cha TBC muda huu mdahalo wa uongozi mama Anna Makinda anasema yeye alikuwa na wenzake 20 ambao ni wapinzani bungeni na anasema walikuwa ni self made opposition. Na walikuwa wakali mpaka Nyerere aliahirisha Safari yake ya Ruvuma akafika bungeni akamwambia Cleopa David Msuya hawa wabunge wa mrengo wa upinzani ndio tunaoutaka, kwahiyo Nyerere aliona umuhimu wa upinzani. Vipi nyie CCM wa Leo kwanini mmeuwa upinzani? Kwa maoni ya mwalimu nyie CCM Leo mnafanya vibaya.
Sema kwa mujibu wako wewe unaona yeye kaiumbua CCM lakini yeye wala hakukusudia kuumbua.

Tafsiri kwa wewe uonavyo, hii tabia ndio inakuwa kubwa mpaka mtu anakuja kuwa mfitinishaji mkubwa katika jamii.

Sema kwa uono wako sio unatafsiri maneno ya watu kwa uono wako alafu unafanya huo muono wako ndio nia yake ya kuzungumza hivyo.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,111
2,000
Kwenye kipindi Cha TBC muda huu mdahalo wa uongozi mama Anna Makinda anasema yeye alikuwa na wenzake 20 ambao ni wapinzani bungeni na anasema walikuwa ni self made opposition. Na walikuwa wakali mpaka Nyerere aliahirisha Safari yake ya Ruvuma akafika bungeni akamwambia Cleopa David Msuya hawa wabunge wa mrengo wa upinzani ndio tunaoutaka, kwahiyo Nyerere aliona umuhimu wa upinzani. Vipi nyie CCM wa Leo kwanini mmeuwa upinzani? Kwa maoni ya mwalimu nyie CCM Leo mnafanya vibaya.
Nyerere aliupenda upinzani ambao unatumia right channel yaani kama kuongelea hivyo bungeni ndio maana aliunga mkono

Sio huu wetu wa kijinga wa kuhamasisha watu sijui kuandamana nje ya bunge au kupinga maendeleo kwenye majimbo na kuitisha mikutano ya vurugu mitaani

Huo wa bungeni mbona ruksa hakuna anayezuia mbunge asiongee
 
kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
4,134
2,000
Mtu ataambiwa anawashwawashwa sasa hivi ... Ndo next time tuchague mtu muungwana hicho ni kigezo muhimu sana hasa nchi za kiafrika ambamo utu ni kitu adimu mmmno!!
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,636
2,000
Huyu mama anaongea hivi kwa sababu yuko nje ya system tu. Laiti angekuwa kwenye system angefanya haya haya. Shida ni kwamba kuna machaguo mawili tu sasa hivi
1. CCM na serekali wakiruhusu upinzani na kuupa uhuru na kuwe na haki, CCM inaanguka na serekali inakwenda upinzani. Na wao wanajua hili
2. Kuua upinzani na kutokuwa huru wala haki ili CCM iendelee kuunda serekali.

Sasa mama yangu Makinda atuambie angekuwa yeye ndio kwanzaa kachaguliwa kaingia madarakani kaonja utamu wa kutembea na ving'ora, mapolisi na majeshi yote yako chini yake angechagua nini hapo?

Lakini pia hebu ajiulize ndani ya nafsi yake akiwa yeye na Mungu wake tu, ajiulize kimya kimya tu wakati yeye yuko kiongozi alikuwa fair kabisa kwa wapinzani? Au anapenda upinzani uwepo uminywe ila usiuliwe.
 
myoyambendi

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
101,012
2,000
Nyerere aliupenda upinzani ambao unatumia right channel yaani kama kuongelea hivyo bungeni ndio maana aliunga mkono

Sio huu wetu wa kijinga wa kuhamasisha watu sijui kuandamana nje ya bunge au kupinga maendeleo kwenye majimbo na kuitisha mikutano ya vurugu mitaani

Huo wa bungemni mbona ruksa hakuna anayezuia mbunge asiongee
Sidhani kama UK sahihi...
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
49,862
2,000
1612619543420.png
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
10,236
2,000
Hata wakiwa CCM wote sio kwamba wote watakuabaliana kila jambo.
Kila mbunge ana akili zake na kupinzana katika kujenga kupo palepale
 
Mapank

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
1,721
2,000
Kwenye kipindi Cha TBC muda huu mdahalo wa uongozi mama Anna Makinda anasema yeye alikuwa na wenzake 20 ambao ni wapinzani bungeni na anasema walikuwa ni self made opposition. Na walikuwa wakali mpaka Nyerere aliahirisha Safari yake ya Ruvuma akafika bungeni akamwambia Cleopa David Msuya hawa wabunge wa mrengo wa upinzani ndio tunaoutaka, kwahiyo Nyerere aliona umuhimu wa upinzani. Vipi nyie CCM wa Leo kwanini mmeuwa upinzani? Kwa maoni ya mwalimu nyie CCM Leo mnafanya vibaya.
Na bado tumecheleweshwa saanaaaa
 
mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,917
2,000
Kwenye kipindi Cha TBC muda huu mdahalo wa uongozi mama Anna Makinda anasema yeye alikuwa na wenzake 20 ambao ni wapinzani bungeni na anasema walikuwa ni self made opposition. Na walikuwa wakali mpaka Nyerere aliahirisha Safari yake ya Ruvuma akafika bungeni akamwambia Cleopa David Msuya hawa wabunge wa mrengo wa upinzani ndio tunaoutaka, kwahiyo Nyerere aliona umuhimu wa upinzani. Vipi nyie CCM wa Leo kwanini mmeuwa upinzani? Kwa maoni ya mwalimu nyie CCM Leo mnafanya vibaya.

Weka na kideo tuone!
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
10,992
2,000
Kwenye kipindi Cha TBC muda huu mdahalo wa uongozi mama Anna Makinda anasema yeye alikuwa na wenzake 20 ambao ni wapinzani bungeni na anasema walikuwa ni self made opposition. Na walikuwa wakali mpaka Nyerere aliahirisha Safari yake ya Ruvuma akafika bungeni akamwambia Cleopa David Msuya hawa wabunge wa mrengo wa upinzani ndio tunaoutaka, kwahiyo Nyerere aliona umuhimu wa upinzani. Vipi nyie CCM wa Leo kwanini mmeuwa upinzani? Kwa maoni ya mwalimu nyie CCM Leo mnafanya vibaya.
Bibi ameona asife moyo ukiwa unamsuta

Afadhali hizi voice of reason zinatoka kwa hawa wazee....

Kuna jitu linaitwa Pius Msekwa,aiseee...shame on me!
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
4,130
2,000
Nyerere aliupenda upinzani ambao unatumia right channel yaani kama kuongelea hivyo bungeni ndio maana aliunga mkono

Sio huu wetu wa kijinga wa kuhamasisha watu sijui kuandamana nje ya bunge au kupinga maendeleo kwenye majimbo na kuitisha mikutano ya vurugu mitaani

Huo wa bungemni mbona ruksa hakuna anayezuia mbunge asiongee
Israel kuna maandamano leo sijui mwaka wa ngapi hakuna maendeleo?
Marekani juzi waliandamana Je, hakuna maendeleo?
Acha kuchanganya watu na viroja vyako vya kuokoteza
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,111
2,000
Israel kuna maandamano leo sijui mwaka wa ngapi hakuna maendeleo?
Marekani juzi waliandamana he hakuna maendeleo?
Acha kuchanganya watu na viroja vyako vya kuokoteza
Wale wanajielewa huwezi ukaona wakiandamana wanapora maduka ya watu na kupora watu na huandamana kistaarabu hawazuii watu wengine kuendelea na shughuli zao !!

Huku mijitu ikiandamana barabara zinafungwa na kuleta usumbufu kwa watu wengine kule kwa wenzetu miundombinu iko vizuri haileti incoviniance kwa wengine wasio na mpango na maandamano

Huku kwetu hakuna waandamanaji wa maana ni vichaa wavuta bangi wanaoingia barabarani
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
4,130
2,000
Wale wanajielewa huwezi ukaona wakiandamana wanapora maduka ya watu na kupora watu na huandamana kistaarabu hawazuii watu wengine kuendelea na shughuli zao !!

Huku mijitu ikiandamana barabara zinafungwa na kuleta usumbufu kwa watu wengine kule kwa wenzetu miundombinu iko vizuri haileti incoviniance kwa wengine wasio na mpango na maandamano

Huku kwetu hakuna waandamanaji wa maana ni vichaa wavuta bangi wanaoingia barabarani
Maandamano ni nini?? Muandamanaji wa maana ni yupi??
Kazi za polisi ni kulinda watu na Mali zao? Kwann police wasiende Badala ya kufyatua magumu?
Unasema miundombinu??? Kwahiyo tusubir mpaka miundombinu iwe kama USA ndo tusi haki zetu?
Hakika wewe unaita huruma kweli
Lowasa alisindikizwa toka buguruni mpaka ufipa nano aliporwa japo sahani?
Ruge mwili wake ulisindikizwa na maelfu kwa maandamano kuna shughuli ilisimama pale?
Mengine muwe mnatafakari kwanza
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
9,494
2,000
Huyu Anna Makinda amelelewa na TANU na CCM na ametumikia katika siasa toka ukigoli wake mpaka hivi leo amestaafu; je anaweza kusema kwa haki ya MUNGU kuwa hii ccm ya JIWE ni sawa na CCM ya enzi ya Nyerere? Nyerere alikuwa anakosolewa ndani ya chama lakini hivi leo hiyo ni dhambi kubwa ambayo inapelekea wanachama kufukuzwa. Nyerere alikuwa anapenda watu wajisahihishe kwani alijua kuwa binadamu hukosea lakini sio Jiwe , yeye hajui maana ya kujisahihisha. CCm enzi ya Mwalimu kilikuwa chama cha demokrasia lakini hivi leo ni chama cha dikteta ambae anachoamua yeye ndio hicho hicho hata pale anapovunja katiba!!!

CCm ya Nyerere imetekwa na Watu ambao sera zao ni za ukabila na upendeleo na ndio maana kila kitu siku hizi ni Chato; simply because kiongozi wa chama kwao ni Chato!!! Kwa bahati mbaya sana watu wa hadhi ya Mzee Rajab Diwani, Kaaya na Mwangoka hawapo tena duniani kuweza kukinyoosha chama kirudi kwenye maadili ya kupinga ukabila , rushwa na kuheshimu katiba ya nchi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom