Zain yapunguza bei - 1Tsh per minute

Zain yapunguza bei - 1Tsh per minute
Mkuu usisite kunitumia nikuongeze kwenye list ya contacts :)

Aaah Maxence mbona unatuchanganya hapo kwenye red? Kumbe ni 1Tsh kwa sekunde nilidhani kwa dakika mbona hiyo ingekuwa bomba zaidi

Haya sasa ni mashindano ya kuwavuta wateja kutoka mtandao fulani kwenda mwingine
Tigo 1Tsh kwa sekunde wakati wote
Zain 1Tsh kwa sekunde wakati wote
Zantel 1Tsh kwa sekunde wakati wote
Voda 1Tsh kwa sekunde wakati wote isipokuwa saa 11:00 jioni hadi saa 3:00 usiku. Halafu hawa VODACOM bado wagumu kwanini na wenyewe isiwe wakati wote kama hao wenzao?
 
ha ha ha hommie kwani ya Kichina line nne huna?
Hivi simu ya line nne shilingi ngapi? Maana hawa jamaa wameweka 1Tsh kwa sekunde kwa mtandao wenyewe kwa wenyewe yaani voda kwa voda, zain kwa zain, tigo kwa tigo, zantel kwa zantel, Ukichepuka kidogo tu utashashangaa sh. 500 hata dakika moja haimalizi.
 
network.jpg


Wapunguze bei pia waboreshe coverage maana tometoka mbali jamaa hajali maisha yake rather than kutafuta network kazi kwelikweli!!
 
haah!!! kama imefikia hapa basi leo nanunua line ya zain ni ongee kwa uhuru, ila mbio za sakafuni huishia ukingoni kamwe hawawezi kuta tigo xpress ur self
 
haah!!! kama imefikia hapa basi leo nanunua line ya zain ni ongee kwa uhuru, ila mbio za sakafuni huishia ukingoni kamwe hawawezi kuta tigo xpress ur self


Kweli kabisa. Ingawa ni hatua nzuri, lakini Voda na Zain wamechelewa sana. Hata hivyo hapo tulipofikia siyo pabaya. Tunaweza kuongea kwa simu sasa bila kuweka kidole kwenye kitufe chekundu tayari kwa kukata simu. Ama kweli tumetoka mbali sana!!
 
Inaonyesha walikua wanawaibia wateja pesa nyingi, talk time ni
rahisi dunia nzima, kama kwa shilingi au nusu shillingi au robo shillingi wanaweza
kupata faida kwa nini walikuwa wanawalipisha pesa nyingi hapo awali kama siyo wizi?
 
Nimeshaanza kutumia line yangu ya Zain. Nadhani ni best alternative kwa sababu sometimes tiGo inazidiwa na unakuta siku 2 mawasiliano yanakuwa sio mazuri. Sitegemei kitu kama hiki kwa Zain............
 
sisi hatuitaki zain, wala togo, wala voda, ataekuwa cheap na reliable ndo mtandao wetu, afterall wote hao ni wachumaji tuu!
 
Hawa Zain walikuwa wamelala fofofo kuja kushituka wako very late sasa wana hasira kiasi cha kutoa dk 60 kwa shilingi moja. Nilikuwa nimeiweka kando chip yangu ya Zain kwa siku mbili hivi! Wahindi waliouziwa Zain wamekula hasara itawachukua muda sana kuja kurudisha gharama zao za uwekezaji hadi kupata faida. Tunawasubiria Voda nao maana wanajifanya kubana ifikapo saa 11 jioni hadi saa 3 usiku najua muda si mrefu watanyoosha mikono.

Kuna wakati TCRA waliwataka Makampni ya simu yashushe gharama hadi shilingi 17 kwa dk wakajifanya kukomaa sasa wameanza kushusha wenyewe taratibu. Asante sana TiGO maana bila ninyi hawa jamaa wangeeendelea kutuchuna na kutiunyonya damu.
 
Sasa ndio tunajua hawa jamaa wametengeneza hela kiasi gani kipindi cha nyuma coz hapakua na watch dogs. Hivi isn't profiteering by a company against the law in TZ?
I'm not happy, I think we should sue these companies!!!
 
Wameamua kushuka baada ya kuona wateja wao wamewakimbia wamehamia Tigo, Voda na Zantel......siye twatesa na thumni

Ustake ncheke mie Voda nako kwa kukimbilia kunani - kwa mafisadi ili wazidi kukupurura -pole ndugu

................................

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
wakati tunasherehekea hili tusisahau kuna watu wanapunguzwa kazini kupunguza gharama za undeshaji wa mitandao hii. Badala ya kulipia gharama zile kwa kuongea na simu sasa utaanza kumsaidia nduguyo chakula cha mchana na nauli ya kufuatilai ajira mpya. Gharama pale pale

hahaaaa !! Yaani huo ndio upande wa pili wa shilingi ama kwa maneno mengine kinachoendelea nyuma ya pazia - ama kweli MSIBA NA NYEMI.

................................

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
  • Ongea kwa Tsh 1 kwa sekunde siku nzima.
  • Ongea kwa Tsh 1 kwa dakika usiku kucha.
  • Hakuna Kujisajili, Hakuna Kikomo cha Muda, Hakuna Malipo Yaliyofichwa, Hakuna kukatika Simu Ovyo, Hakuna Msongamano wa Simu.

ZAIN_1Sh.JPG


Zain, kampuni inayoheshimika zaidi Tanzania na inayoongoza kwa ubunifu wa bidhaa na huduma, leo imedhidi kudhihirisha umahiri wake katika soko kwa kuzindua mpango mpya wa malipo ya kupiga simu wenye viwango vya chini kuliko vyote nchini wa Tshs 1 unaojulikana kama; "Uhuru wa kuongea".

''Ninayo furaha kubwa kuwatangazia kwamba kuanzia leo wateja wetu waliopo na wapya katika mpango wa malipo kabla, moja kwa moja watajiunga na mpango wa Tsh 1 kwa sekunde saa 24 ikiwa ni pamoja na kuweza kupiga simu kwa kiwango nafuu kuliko vyote cha Tsh1 kwa dakika baada dakika ya kwanza ya Uhuru wa Kuongea wakati wa usiku. Mbali na kutoa ubunifu wa kisasa wa kiteknolojia pamoja na kuwa na huduma bora zenye kuambatana na mtandao kuenea nchi nzima, Zain imejidhatiti kuongoza katika sekta ya mawasiliano kwa kuzidi kutoa viwango nafuu zaidi kwa wateja wetu, na ndio maana tumezindua Uhuru wa Kuongea ikiwa ni kutambua mahitaji ya soko la huduma ya simu na kuzingatia unafuu. Hakuna kujisajili, wala gharama za kuhama kutoka mpango mmoja kwenda mwingine, tunaposema ‘Uhuru wa Kuongea', tunamaanisha hicho hicho,'' alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi.

Zain imeamua kuwa wazi na bayana, hakuna haja ya kujiunga, wasiwasi wa muda, malipo yaliyofichwa wala simu kukatika katika kutokana na msongamano. Wateja wetu wataweza kujivunia Uhuru wa Kuongea kwa urahisi kabisa saa 24 siku zote za wiki wakiwa na uhakika wa mtandao madhubuti na ulioenea nchi nzima.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo mpya wa malipo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania Ahsan Syed alisema, ''Zain imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 500 katika miundombinu ya mawasiliano katika kipindi cha miaka mitano ilipopita kuhakikisha tunawapa wateja wetu huduma bora ya viwango nafuu popote pale walipo nchini. Mpango wetu wa malipo ya Tshs 1 ni rahisi na hauna mkanganyiko wowote na ni kwa Saa 24 kwa siku. Muda wa usiku kati ya saa tano usiku hadi saa moja alfajiri, wateja wa Zain watapiga simu vya viwango vya chini kabisa vya Tshs 1 kwa dakika baada ya dakika moja ya kwanza. Wateja wa Zain hawatalazimika kuangalia saa zao za mkononi au ukutani kujua kama wako katika muda wa viwango vya Malipo ya Tsh 1, na hii ndio inatutofautisha na makampuni mengine.''

''Tunatambua kwamba kufanikisha kupatikana mawasiliano ni eneo ambalo tunatoa mchango mkubwa kwa jamii na kuchangia kushamiri kwa uchumi wa Tanzania. Simu za mkononi zina mchango mkubwa katika uchumi wetu na ndio sababu sio tu kwamba tunaleta bidhaa zenye ubunifu mkubwa lakini pia tunahakikisha mtandao wetu ni wa kutegemewa na uliosambaa maeneo mengi zaidi nchini Tanzania. Pia tumesambaza mtandao wetu na bidhaa zetu maeneo mengi vijijini ili kuwawezesha mamilioni ya watu wanaoishi maeneo ya vijijini kuwasiliana na ndugu zao wanaoishi mijini na kuwapunguzia adha mbalimbali zinazosababishwa na umbali. Kupitia Uhuru wa Kuongea, Zain inazidi kuwathibitishia watanzania maana halisi ya Ulimwengu Maridhawa'' Mkurugenzi wa Mtandao wa Zain Tanzania Thierry Diasonama alisema.

Chanzo: Zain Press Release



ZAIN_1Sh.JPG

Jamaa wa kati huyo na kidole chake, imagine kingekuwa cha kati ? au tuseme yeye hajaridhika na punguzo ?

......................................

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
jamani kweli vita ya panzi furaha ya kunguru nimeamini sasa tigo hudumu maana kama si ww watanzania wangepata wapi unafuu ivi tigo awawezi kuanzisha kampuni ya kuzalisha umeme mana ndo lilobaki alina ushindani cjui sasatel watapumulia wapi kwani wao ndo wamedandia fuso kwa mbele bei juu
 
Back
Top Bottom