Zain yapunguza bei - 1Tsh per minute

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,196
13,186
  • Ongea kwa Tsh 1 kwa sekunde siku nzima.
  • Ongea kwa Tsh 1 kwa dakika usiku kucha.
  • Hakuna Kujisajili, Hakuna Kikomo cha Muda, Hakuna Malipo Yaliyofichwa, Hakuna kukatika Simu Ovyo, Hakuna Msongamano wa Simu.

ZAIN_1Sh.JPG


Zain, kampuni inayoheshimika zaidi Tanzania na inayoongoza kwa ubunifu wa bidhaa na huduma, leo imedhidi kudhihirisha umahiri wake katika soko kwa kuzindua mpango mpya wa malipo ya kupiga simu wenye viwango vya chini kuliko vyote nchini wa Tshs 1 unaojulikana kama; “Uhuru wa kuongea”.

‘’Ninayo furaha kubwa kuwatangazia kwamba kuanzia leo wateja wetu waliopo na wapya katika mpango wa malipo kabla, moja kwa moja watajiunga na mpango wa Tsh 1 kwa sekunde saa 24 ikiwa ni pamoja na kuweza kupiga simu kwa kiwango nafuu kuliko vyote cha Tsh1 kwa dakika baada dakika ya kwanza ya Uhuru wa Kuongea wakati wa usiku. Mbali na kutoa ubunifu wa kisasa wa kiteknolojia pamoja na kuwa na huduma bora zenye kuambatana na mtandao kuenea nchi nzima, Zain imejidhatiti kuongoza katika sekta ya mawasiliano kwa kuzidi kutoa viwango nafuu zaidi kwa wateja wetu, na ndio maana tumezindua Uhuru wa Kuongea ikiwa ni kutambua mahitaji ya soko la huduma ya simu na kuzingatia unafuu. Hakuna kujisajili, wala gharama za kuhama kutoka mpango mmoja kwenda mwingine, tunaposema ‘Uhuru wa Kuongea’, tunamaanisha hicho hicho,’’ alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi.

Zain imeamua kuwa wazi na bayana, hakuna haja ya kujiunga, wasiwasi wa muda, malipo yaliyofichwa wala simu kukatika katika kutokana na msongamano. Wateja wetu wataweza kujivunia Uhuru wa Kuongea kwa urahisi kabisa saa 24 siku zote za wiki wakiwa na uhakika wa mtandao madhubuti na ulioenea nchi nzima.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo mpya wa malipo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania Ahsan Syed alisema, ‘’Zain imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 500 katika miundombinu ya mawasiliano katika kipindi cha miaka mitano ilipopita kuhakikisha tunawapa wateja wetu huduma bora ya viwango nafuu popote pale walipo nchini. Mpango wetu wa malipo ya Tshs 1 ni rahisi na hauna mkanganyiko wowote na ni kwa Saa 24 kwa siku. Muda wa usiku kati ya saa tano usiku hadi saa moja alfajiri, wateja wa Zain watapiga simu vya viwango vya chini kabisa vya Tshs 1 kwa dakika baada ya dakika moja ya kwanza. Wateja wa Zain hawatalazimika kuangalia saa zao za mkononi au ukutani kujua kama wako katika muda wa viwango vya Malipo ya Tsh 1, na hii ndio inatutofautisha na makampuni mengine.’’

‘’Tunatambua kwamba kufanikisha kupatikana mawasiliano ni eneo ambalo tunatoa mchango mkubwa kwa jamii na kuchangia kushamiri kwa uchumi wa Tanzania. Simu za mkononi zina mchango mkubwa katika uchumi wetu na ndio sababu sio tu kwamba tunaleta bidhaa zenye ubunifu mkubwa lakini pia tunahakikisha mtandao wetu ni wa kutegemewa na uliosambaa maeneo mengi zaidi nchini Tanzania. Pia tumesambaza mtandao wetu na bidhaa zetu maeneo mengi vijijini ili kuwawezesha mamilioni ya watu wanaoishi maeneo ya vijijini kuwasiliana na ndugu zao wanaoishi mijini na kuwapunguzia adha mbalimbali zinazosababishwa na umbali. Kupitia Uhuru wa Kuongea, Zain inazidi kuwathibitishia watanzania maana halisi ya Ulimwengu Maridhawa’’ Mkurugenzi wa Mtandao wa Zain Tanzania Thierry Diasonama alisema.

Chanzo: Zain Press Release
 
What a news!
Njema sana hii Mkuu!
Wamechukua nyingi sana hawa, ngoja tufaidike na sisis kidogo.
Hata hivyo bado sana...wanatakiwa wamfuate tigo alivyofanya!
 
vita vya panzi furaha yetu sie kunguru......ama kweli mchuano ni mkali
 
Watashusha sana tu but ile congestion katika kupiga simu, jamani acheni tu. Situmii Tigo aka Buzz ukipenda Mobitel lakini nakubali kuwa wanafunika!
 
Wameamua kushuka baada ya kuona wateja wao wamewakimbia wamehamia Tigo, Voda na Zantel......siye twatesa na thumni
 
Wengi walikuwa wanaiona Zain kuwa expensive network, kwa sasa naona kwa mwendo huu line zetu za Zain zitakuwa active. Itabidi nianze kuwagawia marafiki namba yangu ya Zain :)
 
hapo sawa maana vinginevyo wangejikuta
wanaotumia zain ni wafanyakazi wao tu!!!!!!!

if u cant fight join them
 
hahaaaa wametunyonya zimetosha its time sasa waturudishie fadhila

asante ZAIN harakisheni tupitilize 'THUMNI' hadi senti TANO
 
hapo sawa maana vinginevyo wangejikuta
wanaotumia zain ni wafanyakazi wao tu!!!!!!!

if u cant fight join them
wafanyakazi wa ZAIN na VODA na TTCL mobile wenyewe wana line za TIGO
 
Safi sana. sasa itakuja ile ya 'wikienda bure' ! Soko Huria. Nani anakumbuka mbao ya 'ukipiga unalipa, Ukipokea unalipa' na hand set za shs Milioni na ushee? tena kubwa ka walk talkie!!
 
wafanyakazi wa ZAIN na VODA na TTCL mobile wenyewe wana line za TIGO

Hiyo Nyekundu hapo funika bovu nadhani mara ya mwisho kutumia hiyo mitandao mingine ilikua 2001!!
tigo Thumni ni nomaa!!
 
wakati tunasherehekea hili tusisahau kuna watu wanapunguzwa kazini kupunguza gharama za undeshaji wa mitandao hii. Badala ya kulipia gharama zile kwa kuongea na simu sasa utaanza kumsaidia nduguyo chakula cha mchana na nauli ya kufuatilai ajira mpya. Gharama pale pale
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom