Changamoto ya kupost mara 8 (minimum) kwa siku 5 za wiki - JIUNGE!

Changamoto ya kupost mara 8 (minimum) kwa siku 5 za wiki - JIUNGE!

Mwezeshaji1

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2023
Posts
235
Reaction score
562
Hii ni kwa wajasiriamali vichwa moto, na wenye kutaka kukuza biashara zao mwaka huu.

Lengo: kufikia watu wengi zaidi na kuuza bidhaa/huduma

(hakuna ada ya ushiriki -(labda mbeleni), hivyo wewe tu na JITIHADA zako)

Utaratibu:

1. Anza kwa kuandaa vifaa (simu yenye camera yenye mwanga, hata kama si IPhone & mic ya kudaka sauti).
2. Sababu za watu kununua bidhaa zako.
3. Utanashati.

Ikifika tarehe 15/03/2026 TUNAANZA na uzi huu utapokea mrejesho wa siku, lengo tufike mwisho wa mwaka na:

Lengo dogo;
1. Double followers (kama una 100 wawe 200)

Lengo KUBWA
2. Mauzo ya kueleweka (utaandika lengo unalotaka, si lazima UTAJE)

Aina ya maudhui: VIDEO (reels/videos), picha hatuhesabu, ila endelea kuzipost kwa faida nyingine kama kuonesha wateja vitu ili wachague kwa utulivu.

Wapi upost: mitandao ya Instagram, Facebook, tiktok - utachagua wenye wateja unaowataka, (hapa JF utaweka FEEDBACK tu)

Utakuwepo ✋🏿?

(Maboresho ya hili YANAKARIBISHWA)
 
Back
Top Bottom