Zaidi ya wafungwa 300 bado hawajulikani walipo Afghanistan

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Msemaji wa gavana wa mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan anasema zaidi ya wafungwa 300 bado hawajulikani walipo baada ya shambulizi la kundi la kigaidi linalojiita dola la kiislamu katika gereza moja katika mji wa Jalalabad. Attaulah Khugyani amesema kuwa kati ya wafungwa 1,793, zaidi ya 1,025 walijaribu kutoroka ila wakakamatwa. Wafungwa wengine 430 walisalia ndani ya gereza hilo.

Shambulizi hilo lilianza jana usiku na mapigano kati ya watu waliojihami kwa bunduki na maafisa wa usalama yaliendelea hadi leo. Msemaji huyo Attaulah amesema watu 29 wamefariki dunia kutokana na makabiliano hayo na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Ripoti zinaarifu kwamba maafisa wa usalama wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa gereza hilo mchana wa leo.
 
Dah! Nawaza tu kuhusu bongo maana hali ya usalama wetu ni tulivu saana sijui siku hiyo nani atashinda.
 
Back
Top Bottom