Ndugu Bruce Lee acha hasira zisizokuwa na msingi, naomba uisome mada tena ndiyo uanze kujadili na pia utambue kuwa si lazima kila mtu afikiri kama unavyofikiri wewe. Kwa mtazamo wangu mwanzilishi wa mada ana nia njema sana ujue kama mchakato wa Slaa 2010 ungeanza mapema Slaa lazima angechukua nchi. Mwanzisha mada anatambua wazi kuwa Dr. Slaa ndiye anayefaa lakini ikitokea hayupo? ikitokea hataki kugombea tena kama alivyokua akihubiri katika kampeni zake za urais 2010? je mbowe akiendeleza nia yake ya kugombea urais tutafanyaje? Lazima tujiulize mapema na ndio mada imekuja tuijadili. Kuwa makini sana hasa unapowatukana watu usiowajua kuwa wanafiki, nchi hii ni ya kila mmoja.
Kwangu mimi Mnyika ni wa 2020/25, Zito 2020, Lisu anaweza kuwa mzuri kama tu akipunguza jazba ambayo anaipata kwa kuwa tu ni mwanaharakati na harakati haziendani na uongozi wa kisiasa. Naamini mpaka amalize muda wake wa ubunge 2015 atakuwa amesharekebishika. Kwa upande Mwingine tuombee Dr. Slaa asifanyiwe uhuni ninaouhisi kutoka kwa Mbowe ili agombee tena 2015 hata kama hatashinda lakini ataleta mabadiliko makubwa sana yaani kuongeza viti vya upinzani bungeni na kuitikisa CCM ijue kuwa watu tunataka mabadiliko siyo ya kidhana tu au ya kubadili chama bali kubadili hali halisi ya mtanzania.