Zaidi ya 1000 wajiunga CHADEMA

Zaidi ya 1000 wajiunga CHADEMA

Mkuu mbona hueleweki haukujipanga vizuri kuongopa nini? mara zaidi ya watu 1000 wamejiunga CDM wengi kutoka CCM , mara waliotoka CCM ni 100, hao ndiyo wengi?

Hii dhana ya kwamba M4C imeaundwa kuiondoa CCM madarakani ndiyo itakayowamaliza CDM, ina maana hiyo ndiyo sababu ya msingi?

Hebu jaribu kuwa na uwezo wa kufikiri, hayo ni majumlisho ya sehemu zote walizotembelea makamanda..
 
Huyu Jamaa alipona kweli?

attachment.php

Hao ni CDM ndo walimfanya hivyo?
 
Hebu jaribu kuwa na uwezo wa kufikiri, hayo ni majumlisho ya sehemu zote walizotembelea makamanda..

Naona kweli ulipania kutamka ulichoambiwa utamke, tufikiri tunachangia mada bila kusoma?
 
Sidhani kama maneno matupu vila vitendo yanaweza kuiondoa CCM madarakani, huwezi kuanzisha vuguvugu kwa sababu tu unataka kukiondoa chama tawala madarakani bila sbabu ya msingi.

We mburula unataka sababu gani?
 
ok..ahsante kwa taarifa
tunataka kujua pia idadi ya waliohama cdm na kwenda vyama vingine..tusije tukawa tunaingiza 10 lakini wanatoka 100 tukadhani tunaendelea vizuri while tukawa tunajidanganya wenyewe..tiririka tafadhali
si kitu kizuri kusikika masikioni mwa mashabiki wenzangu wa cdm lakin tunapaswa kufanya tathmini vizuri

Hizo takwimu kawaulize CCM, ndo wenye record ya waliohama chadema kwenda CCM! Otherwise wewe ni Gamba Original!
 
ahsante...chama kisichotaka changamoto mwisho wake mfupi,we unadhani kila anayetoa mawazo tofauti na yako ni gamba...r.i.p bro
Hizo takwimu kawaulize CCM, ndo wenye record ya waliohama chadema kwenda CCM! Otherwise wewe ni Gamba Original!
 
ok..ahsante kwa taarifa
tunataka kujua pia idadi ya waliohama cdm na kwenda vyama vingine..tusije tukawa tunaingiza 10 lakini wanatoka 100 tukadhani tunaendelea vizuri while tukawa tunajidanganya wenyewe..tiririka tafadhali
si kitu kizuri kusikika masikioni mwa mashabiki wenzangu wa cdm lakin tunapaswa kufanya tathmini vizuri

Uliza mhariri wa Uhuru
 
Chadema wasifurahie idadi ya watu bali kati ya hao waliowavuna ni wangapi wanamapenzi ya dhati na wako tayari kukitetea chama.Vinginevyo wataingia leo Chadema kesho watarudi CCM.
 
Makamanda kazi nzuri Bravoooo. ccm hakubaliki lazima itokomezwe kabisa
CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kupitia kikosi kazi chake cha Vuguvugu la Mabadiliko
(M4C), Kanda ya Ziwa, kimefanikiwa kuzoa zaidi ya wanachama wapya
1,000, wengi wakitokea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wakizungumza na Tanzania Daima jana wilayani hapa, viongozi waandamizi
wa M4C Kanda ya Ziwa, Husina Amri Saidi, na Alfonce Mawazo, walisema M4C
imedhamiria kujikita zaidi maeneo ya vijijini.

Walisema baadhi ya wananchi hao walipatikana katika mikutano yao
iliyofanyika kisiwa cha Bumbile, kata ya Bumbile, jimbo hilo la Muleba
Kaskazini ambao ni zaidi ya 200 waliojiunga na CHADEMA.

Mbali na hilo alisema zaidi ya wanachama 100 wa CCM walilazimika
kurudisha kadi zao na kujiunga CHADEMA.

“Kwa kweli CHADEMA kupitia M4C tumeweza kuzoa wanachama wengi katika
visiwa vya Muleba Kaskazini.

“Kisiwa cha Bumbile, kata ya Bumbile, zaidi ya wananchi 200 wamejiunga
na CHADEMA kwa kununua kadi kwa hela zao.

“Lakini, wapo zaidi ya wana CCM 100 wamerudisha kadi za ‘magamba’ kisha
kuvaa ‘kombati’,” alisema Husina.

Walisema wakiwa katika visiwa vya Lushonga na Mchangani zaidi ya
wananchi 438 walijiunga na CHADEMA.

Akizungumzia harakati za CHADEMA katika kuelekea kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015, Kamanda
wa M4C Kanda ya Ziwa, Mawazo, aliwasihi wananchi wote wa Kanda ya Ziwa
na Tanzania kwa jumla kutumia nguvu ya umma kuiondoa CCM madarakani
kwenye uchaguzi mkuu ujao.
 
Back
Top Bottom