Zaidi ya 1000 wajiunga CHADEMA

Zaidi ya 1000 wajiunga CHADEMA

sodeely

Senior Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
190
Reaction score
120
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kikosi kazi chake cha Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Kanda ya Ziwa, kimefanikiwa kuzoa zaidi ya wanachama wapya 1,000, wengi wakitokea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wakizungumza na Tanzania Daima jana wilayani hapa, viongozi waandamizi wa M4C Kanda ya Ziwa, Husina Amri Saidi, na Alfonce Mawazo, walisema M4C imedhamiria kujikita zaidi maeneo ya vijijini.

Walisema baadhi ya wananchi hao walipatikana katika mikutano yao iliyofanyika kisiwa cha Bumbile, kata ya Bumbile, jimbo hilo la Muleba Kaskazini ambao ni zaidi ya 200 waliojiunga na CHADEMA.

Mbali na hilo alisema zaidi ya wanachama 100 wa CCM walilazimika kurudisha kadi zao na kujiunga CHADEMA.

“Kwa kweli CHADEMA kupitia M4C tumeweza kuzoa wanachama wengi katika visiwa vya Muleba Kaskazini.

“Kisiwa cha Bumbile, kata ya Bumbile, zaidi ya wananchi 200 wamejiunga na CHADEMA kwa kununua kadi kwa hela zao.

“Lakini, wapo zaidi ya wana CCM 100 wamerudisha kadi za ‘magamba’ kisha kuvaa ‘kombati’,” alisema Husina.

Walisema wakiwa katika visiwa vya Lushonga na Mchangani zaidi ya wananchi 438 walijiunga na CHADEMA.

Akizungumzia harakati za CHADEMA katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015, Kamanda wa M4C Kanda ya Ziwa, Mawazo, aliwasihi wananchi wote wa Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa jumla kutumia nguvu ya umma kuiondoa CCM madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao.
 
wahaya inabidi waamke,wanawakumbatia sana magamba hawa nshomile.
 
Mbona magamba yameanza kuanguka mapema coz mambo bado, ndio kwanza 2013

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kamanda Mawazo ana mawazo chanya ya kuleta mabadiliko katika fikra za watu.
 
ok..ahsante kwa taarifa
tunataka kujua pia idadi ya waliohama cdm na kwenda vyama vingine..tusije tukawa tunaingiza 10 lakini wanatoka 100 tukadhani tunaendelea vizuri while tukawa tunajidanganya wenyewe..tiririka tafadhali
si kitu kizuri kusikika masikioni mwa mashabiki wenzangu wa cdm lakin tunapaswa kufanya tathmini vizuri
 
uhuru mpya ni kitu cha thamani sana kwetu! M4C ndiyo njia kueleke uhuru wa mawazo na fikra
 
u can have fewer resources but at the end of the day game plan matters!!. Move on M4C - deep down to finish them off before 2014.
 
Huyu Jamaa alipona kweli?

attachment.php
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kikosi kazi chake cha Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Kanda ya Ziwa, kimefanikiwa kuzoa zaidi ya wanachama wapya 1,000, wengi wakitokea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wakizungumza na Tanzania Daima jana wilayani hapa, viongozi waandamizi wa M4C Kanda ya Ziwa, Husina Amri Saidi, na Alfonce Mawazo, walisema M4C imedhamiria kujikita zaidi maeneo ya vijijini.

Walisema baadhi ya wananchi hao walipatikana katika mikutano yao iliyofanyika kisiwa cha Bumbile, kata ya Bumbile, jimbo hilo la Muleba Kaskazini ambao ni zaidi ya 200 waliojiunga na CHADEMA.

Mbali na hilo alisema zaidi ya wanachama 100 wa CCM walilazimika kurudisha kadi zao na kujiunga CHADEMA.

"Kwa kweli CHADEMA kupitia M4C tumeweza kuzoa wanachama wengi katika visiwa vya Muleba Kaskazini.

"Kisiwa cha Bumbile, kata ya Bumbile, zaidi ya wananchi 200 wamejiunga na CHADEMA kwa kununua kadi kwa hela zao.

"Lakini, wapo zaidi ya wana CCM 100 wamerudisha kadi za ‘magamba' kisha kuvaa ‘kombati'," alisema Husina.

Walisema wakiwa katika visiwa vya Lushonga na Mchangani zaidi ya wananchi 438 walijiunga na CHADEMA.

Akizungumzia harakati za CHADEMA katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015, Kamanda wa M4C Kanda ya Ziwa, Mawazo, aliwasihi wananchi wote wa Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa jumla kutumia nguvu ya umma kuiondoa CCM madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Mkuu mbona hueleweki haukujipanga vizuri kuongopa nini? mara zaidi ya watu 1000 wamejiunga CDM wengi kutoka CCM , mara waliotoka CCM ni 100, hao ndiyo wengi?

Hii dhana ya kwamba M4C imeaundwa kuiondoa CCM madarakani ndiyo itakayowamaliza CDM, ina maana hiyo ndiyo sababu ya msingi?
 
Hongera sana Kamanda Mawazo na kikosi chako, kazi yenu tunaiona........HADI KIELEWEKE
 
Unazungumzia ngombe 1000 kujiunga Chadema au mbuzi
 
Viva CDM.....hakuna kulala!!!! Magamba kifo cha mende.

Sidhani kama maneno matupu vila vitendo yanaweza kuiondoa CCM madarakani, huwezi kuanzisha vuguvugu kwa sababu tu unataka kukiondoa chama tawala madarakani bila sbabu ya msingi.
 
eti ripoti kutoka tanzania daima.....ni sawa na kesi ya kitimoto kapelekewa padri mushi
 
Back
Top Bottom