Zaeni watoto wengi kwa faraja ya uzee wako

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,397
Reaction score
64,618
  • Kama mtu atajaliwa kuishi miaka mingi,uzee hauepukiki.Ni kipindi ambacho mzee atahitaji furaha na faraja kutoka kwa ndugu na jamii inayomzunguka.Kunakuwepo na changamoto hasa pale jamii/ndugu wanaotakiwa kumpa faraja mzee...wanakuwa bize na miangaiko yao ya kimaisha,na kumuacha mzee akiwa na mawazo ya kwenda mbinguni.
  • Wazee wengi hujitahidi kuomba kuishi na wajukuu zao ili wajukuu waweze kuwafariji.Tatizo ni pale wajukuu wanakuwa wako bize kutafuta elimu,kutokana na maisha ya kisasa na wazee kubaki kama wakiwa.
  • Wazee wetu wa zamani walijitahidi sana kuwa na watoto wengi,ili watakapokuwa katika umri wa uzee wasiwe wapweke.Sasa kutokana na maisha ya kisasa, kuwa na mtoto mmoja au wawili,inapelekea wazee wengi hasa wanapofikia umri wa uzee kutokuwa na faraja ya uzao wao.
  • Nashauri ndugu zangu, fyatueni kama uwezo unao hao watakuwa faraja kwako.
 
ACHA UONGO wewe hujafikia Uzee wowote
toka lini Mzee akampenda Mjukuu?
Leo asikie Mjuukuu na mtoto wake wamefungwa unadhani atamlilia nani atoke?
wewe jizalie watoto halafu usiwasomeshe km hajaja kukumaliza humo ndani
fuatilia Kesi za mirathi uone ki,bembe cha watoto wanavyogombana wakati Sheria hairuhusu wajukuu ndipo utakapojua hasara ya kuzaa Timu ya mpira
 
Nimecheka sana....
 
Ukishindwa kujipa faraja mwenyewe, hata dunia nzima ikikupa faraja hutafarijika.
Chukulia mfano,una miaka 80,watoto wako wote wako nchi za mbali,na kwa bahati mbaya ulichagua staili ya kisasa kuishi;utakuwa unajisikiaje?
 
Kuna watu hawana hata mtoto, na wanaishi vizuri tu.

Na wengine wana watoto kibao, na hao watoto kibao ndiyo chanzo cha matatizo kila siku.

Usikariri kwamba kuwa na watoto wengi ndiyo kuwa na faraja.Uanweza kuwa na watoto wengi, halafu wote wakawa machangudoa na mateja. Kila siku wanakuletea kesi mpya.
 
Nakubaliana na wewe;pia kwa nini wahindi huwa wanapenda kuishi boma moja na uzao wao...utakuta bibi,mama,watoto,wajukuu n.k huwa ni kwa nini?
 
Sina uhakika, naweza ku speculate tu.

Wanabana matumizi.Wahindi wana tabia ya kubana matumizi sana.Kulikuwa na jamaa mmoja Singasinga ana kiwanda cha kutengeneza ma bodi ya mabasi Pugu Road, lakini ukimuona hata humjui, anavaa viraba vya DH, lakini watoto wake wanasoma International School of Tanganyika, enzi hizo.

Kiutamaduni kwao wako wengi, washazoea kujazana pamoja.

Kidini wanahimizwa kuwa na ukaribu wa familia.Na wanashikilia sana dini zao.

Kihistoria Tanzania wengi hizi nyumba za NHC/ Msajili walitaifishwa enzi za Azimio la Arusha, sasa wengine kwa mfano Upanga kule, wametaifishwa lakini wameachiwa apartments fulani zao wanakaa nafikiri bure, kwa sababu hizi ni nyumba zao wametaifishwa, sasa hapo wanapata sababu ya kujazana.

Wanapeana michongo ya kutoka, wanaitana kutoka India, mgeni akifika anafikia sehemu, akipata michongo yake anasepa mbele.Unaweza kuona wanajazana, lakini wanakuwa tofautitofauti wanapita hapo, na wengine wanarudi kusalimia wakishapata michongo yao poa.
 
Mbali tu na tamaduni,mi nadhani pia inaweza kuwa ni njia ya kutaka kuwa karibu na wazee wao na kuwafariji kwa sababu sisi wote tunaelekea huko.Inawezekana kuwa imesababisha na biashara za kifamilia,kuwa mzee anazeeka na anawachia vijana waziendeleze na wao wakiendelea kunufaika na mali walizozichuma.
 
Tamaduni za Kiafrika, Kihindi na Kichina, zile za asili, zinaweka mbele sana familia kwa namna ya kwamba watu kuishi pamoja ndiyo asili yenyewe.

Hata ukiangalia vijijini utaona familia zinavyokaa pamoja, sehemu nyingine mpaka leo.

Ila, kwetu sisi Waafrika tumevurugwa kirahisi sana kwa kuletewa dini za wageni na mifumo ya tamaduni ya jamii zenye viwanda ya kuishi mijini.

Kwa kiasi kikubwa mifumo hii inaathiri tamaduni za asili za watu wote, wakiwamo hao Wahindi na Wachina.

Ila, wenzetu wametuzidi kitu kimoja, wao bado wameshikilia dini zao za asili, na mafunzo ya kwenye dini zao za asili ya kuheshimu na kuenzi wazazi na wahenga wao wanayafuata bado.

Nimekutana na muhindi yuko Marekani anafanya kazi za IT, anafanya kazi na very sophisticated systems, lakini ukikaa naye anakwambia mimi siku fulani nilikuwa nafanya "puja", which is some Hindu ritual kwenye dini yao huko.

Wako Marekani lakini wengi bado wameshika tamaduni zao.

Sisi kidogo tumechepuka kutoka mafunzo ya asili na tunaenda kileoleo zaidi.
 
Kuwa na watoto wengi nayo inaweza kuongeza matatizo au kuwa chanzo cha matatizo mbalimbali ambayo yanaweza yakamfanya mtu asifikie hata huo 'Uzee' wenyewe.

Watoto wengine ni wakorofi sana na katika zama hizi za 'Utandawazi' na 'Ma-Smatifoni' yao makubwa makubwa hayo, siku hizi wanajua kila kitu na hawaambiliki.

Watakupa 'Presha' bure tu kwa kesi zisizoisha na mabalaa ya kila aina watakayokuwa wakiyafanya.
 
Nimekuelewa vizuri,kwa hiyo mkuu,unaamini haya maisha ya kuzeeka tukiwa mbali na uzao wetu au kutokuwa na uzao kabisa ni sahihi?
 
Sawa mkuu, nini sasa kifanyike ili uzee wetu uwe wa faraja,furaha na wenye matumaini hasa mtu anapofikia umri wa miaka 70+
 
Hakuna kilicho sahihi kwa watu wote, Waingereza wana msemo unasema "one man's meat is another man's poison".

Na hii ni kweli literally, kuna mtu ambaye hali nyama, akila nyama inamdhuru, kwa hiyo wewe unapoona mnofu wa nyama huu mzuri kwako, kwa mwenzako ni sumu.

Na maisha nayo ni hivyo hivyo, kila mtu inafaa ajitazame mwenyewe ajiamulie mwenyewe kwa kuangalia maisha yake.

Mtu anaweza kukuambia kwamba kuwa na watoto wengi ni vizuri, kwa kufikiri kila mtu ana uwezo wa kulea kama yeye, hilo si lazima liwe kweli kwa kila mtu.

Mtu anaweza kukuambia kwamba kuwa na watoto wengi ni vizuri, kwa kufikiri kwamba "kila mtoto anakuja na riziki yake". Hilo nalo si lazima liwe kweli, siku hizi watoto wanaandaliwa maisha mazuri na wazazi tangu wakiwa wadogo.

Sasa basi, kwa mtu ambaye ataona inafaa kuwa na watoto wengi, kuwa na watoto wengi ni haki ya kibinadamu, afanye hivyo ili asiishi kwa unyonge wa kukosa kufanya alichotaka.

Pia, kwa mtu ambaye anaona dunia ina matatizo mengi, mtu anayeona kwamba kuzaa watoto wengi kwa kila mtu kutaathiri mazingira, kutaongeza umasikini, kutawanyima watoto attention ya wazazi, kutawafanya wakose elimu, kutatengeneza matatizo ya uhalifu na ujinga, naye ni haki yake akiamua kukaa azae mtoto mmoja au hata asiwe na mtoto kabisa.

Muda ndio utaamua.

Mimi binafsi nipo kwenye upande wa kuwa na watoto, lakini wawe wachache. Wawili is around the replacement figure.

Yani, mkiwa baba na amama mnapata watoto wawili, mmemaliza deni lenu la kuletwa duniani na nyie mmeleta wawili, kikawaida mnawaacha nao waendeleze uzao.

Kwa msingi huu, kizazi kinaendelea, lakini hatujazani kwa namna itakayoielemea jamii kwa population issues.

Lakini huo ni msimamo wangu binafsi, sisemi kwamba ni bora zaidi ya msimamo mwingine wa mtu mwingine, kwa sababu masuala haya ni mapana na marefu na athari zake halisi hazijulikani kwa miaka miwili au kumi.
 
Sawa mkuu, nini sasa kifanyike ili uzee wetu uwe wa faraja,furaha na wenye matumaini hasa mtu anapofikia umri wa miaka 70+
Kuizungumzia 'Faraja' ama 'Furaha' katika kipindi cha uzee, inajengwa zaidi na mtu mwenyewe binafsi.

Mfano, huwezi kuwa na furaha ama faraja uzeeni kama hukutengeneza maisha yako ya baadaye wakati ukiwa kijana na nguvu zako.

Maana usipofanya hivyo, kuna uwezekano mkubwa ukaja kuwa na maisha mabovu sana na magumu kiasi ambacho hiyo faraja hutoweza kuipata hata kama una watoto mia.

Kwahiyo, msingi mkuu wa kuwa na furaha katika maisha ya baadaye ni kuanza kuitengeneza hiyo furaha sasa.

Jenga furaha yako ya baadaye wakati ukiwa na nguvu na uwezo wa kufanya mambo kabla uzee haujafika la sivyo itakuwa ngumu sana kuipata uzeeni.
 
Back
Top Bottom