Zabron Singers - Mkono wa bwana

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
KIKUNDI cha Uimbaji cha Zabron Singers wamevunja rekodi kwa Afrika Mashariki kutazamwa na watu zaidi ya milioni 10, jambo ambalo halijawahi kutokea kwa wimbo wowote ya dini.

Kikundi hicho chenye makazi yake mkoani Shinyanga, kimepata umaarufu na wimbo wake ‘Mkono wa Bwana’ ambao ndio umewatambulisha zaidi duniani kote.

Wamevunja rekodi kwa kuwa haijawahi kutokea kikundi au wimbo wa dini kutazamwa na watu kiasi hicho sambamba na kushika nafasi ya kwanza kwa Afrika Mashariki kutazamwa na kupakuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mbali na wimbo huo, mtindo wa uimbaji umechangia pia kuwafurahisha watazamaji wengi kwani wamekuwa wakiimba mithili ya simulizi za kupokezana.

Kikundi hicho ambacho ni muunganiko wa familia tofauti ndani ya ukoo moja, ni waumini wa Kanisa la Wasabato, ambapo kwenye nafasi ya Youtube wanashika nafasi ya kwanza kwenye nyimbo bora ambapo imedumu kwa zaidi ya mwaka, wakiwa na wimbo mmoja tu.

Pia wamewahi kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya video bora na wameshika nafasi ya 37 kupitia wimbo wao uitwao Sikuachi tena na wameshika nafasi ya 99 kupitia wimbo uitwao Sio bure ambao umebeba albamu yao ya tatu iliyotoka mwaka jana.

Wanamuziki wengine walioshika chati katika Youtube ni pamoja na Aniseti Butati, Angel Benard,William Yirima, Walter Chilambo na Martha Baraka.

Kundi la Zabron Singers lilianzishwa mwaka 2006 katika mkoa wa Shinyanga, wilayani Kahama wakiwa chini ya Kanisa la Wasabato linaloitwa Kahama Central SDA na mlezi wao ni Benedict Burash.

WAZO LA MKONO WA BWANA

Zabron Singers walisema Mkono wa Bwana umetokana na mambo ambayo Mungu amewatendea katika kila jambo hata kuona kuwa pasipo Mungu wao sio kitu.

Kiongozi wa kundi hilo, Japhet Zabron alisema wakati wa Bwana ukifika hakuna anayeweza kuuzuia kwa kuwa wimbo ulitungwa mwaka 2013 ukarekodiwa mwaka 2014, tukauachia mwaka 2015 lakini kupokelewa ni 2016.

“Haikuwa kazi rahisi kwa kuwa wengi walikuwa hawaamini kama wanaweza kufanya kitu kikubwa kulingana na jinsi wao walivyo na ndio maana mpaka sasa wimbo umekuwa mkubwamkubwa kuliko sisi tulivyo.”

Credit: Innocent Ndayanse

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zabron Singers alisema Mkono wa Bwana umetokana na mambo ambayo Mungu amewatendea katika kila jambo hata kuona kuwa pasipo Mungu wao sio kitu.
Kiongozi wa kundi hilo, Japhet Zabron alisema wakati wa Bwana ukifika hakuna anayeweza kuuzuia kwa kuwa wimbo ulitungwa mwaka 2013 ukarekodiwa mwaka 2014, tukauachia mwaka 2015 lakini kupokelewa ni 2016.
“Haikuwa kazi rahisi kwa kuwa wengi walikuwa hawaamini kama wanaweza kufanya kitu kikubwa kulingana na jinsi wao walivyo na ndio maana mpaka sasa wimbo umekuwa mkubwamkubwa kuliko sisi tulivyo.”

Credit: Innocent Ndayanse

Sent using Jamii Forums mobile app
kumbe ni wasabato?..ndio maana watu wasabato wengi hawawakubali..kisa wanacheza wakiwa wanaimba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Views zinakimbia utadhani ni mpya
Screenshot_20200424-064810.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom