kwenye suala la kuharibika wakati wa safari, yutong hazina guarantee mkuu, afadhali uharibikiwe na skania! Nimewahi kuharibikiwa na basi la Green star kuja mwanza, hapo shinyanga, tulilala hapo hapo! Na kwa taarifa, yutong za green star kuja mwanza zimechoka sana! zinalaza watu njiani mara kibao...wameleta mpya chache ku-backup ila hali sio nzuri, yutong ni janga mzee...hazina maana! zikikorofisha hamuondoki...systems zake ni electrified, haiwezekana kufanya utundu wa kienyeji kama kwa scania.Na kwa taarifa tu, mabasi ya sumry yanayokufa njiani siku zote ni nissan ud na hino na wala si yutong, maana sumry hana yutong hata moja, na mabasi yanayokufa njiani mengi ni scania na kama kuna yutong utakuta ni chache na hata hayo machache utakuta wakati wa utengenezaji wamiliki au mafundi wao wametumia vipuli fake.
kibaya zaidi wamiliki wa mabsi aina ya scania walio wengi wanashindwa kulipa madeni yao tofauti na wanaotumia Yutong,
Huo ni ushauri wa dhati wenye nia ya kuruzindua wabongo,
Simba
Nasikia kiwanda cha Scania kimechukuliwa na wachina tayari na wanachofanya ni kuendeleza pale wenyewe walipoachia.Katika hayo magari kila kitu bora kipo Scania, ila jamaa zako hata akili zao zishakuwa za kichina.
Yutong speedmeter yake mwisho 140, lakini we njo na speed yako 180 huikamati.
Aidha
1. Speedometer ni MBOVU
au
2. HUJUI maana ya Speed
Hahaha mkuu pole, naona kama umechukia, nilikuwa nakutania kuwataja wafanya wa scania na wala sipajui hapo scania kibaha.
Ila mimi ni researcher ndugu yangu na ninazo statistics na si vema kuzitaja ila hata hao uliowataja nina uhakika watakubaliana nami, maana ni kweli wanazo scania na wanajitahidi tu, lakini nina wasiwasi ikiwa wakiongeza wataongeza kwa kununua scania.
Ningependa nikaishia hapo isije kuonekana nina ugomvi na scania ili hali hata kuwajua siwajui ila ninajua mbinu za ndugu zetu za hizi nchi za uaya wanavopenda kuponda chochote kisichotoka kwao. Wanangangania sifa walizokuwa nazo enzi hizo ambazo hawana. Na tukubali era yao kibiashara ishapita hii ni era ya wachina na ili mradi tuhakiki tunachonunua ni kizuri basi tuende na mfuo kwa kuangalia maslhi yetu na sio ya kuiga,
Smba
wadau kuna kaubishi kapo hapa kijiweni kwetu kuhusu efficiency ya haya magari especially mabasi. Ubishi ume-base sana kwenye
1) speed ya mabasi, wengi wanaSema yutong ni funiko kuliko scania na ud.
2) ubovu- wamerate kuwa ubovu mchina anaongoza na relate kipindi yalipoingia Yalilaza watu njian nikiwemo na mimi. Ud wanatolea mfano sumry anavoPotea kwenye ushindan.
3)oil consumption. Mchina consumption yake iko chini kuliko wote. je ni kweli
NaOmba wadau na wajuzi wanisaisidie kwasabab nahitaJi kujua ubora wa haya Magar na hata wadau wengine ambao wanaweza kutaKa kuinvest kwenye biashaRa ya magari itawasaidia
ile ya buffalo ni ZONDA na sio YUTONG mkuu!hizi tutong zipo za matumizi ya mjini kama ile ya buffallo na zipo nyingine kwa matumizi ya barabara na mazingira magumu na scania hivyo hivyo .unapotaka kufanya uamuzi wa kununua usivutiwe na muundo ,utaelezwa .pili mafuta .ulaji wa mafuta ni kitu cha kuzinagatia ,engine oil inatumia kiasi gani ,formula iko hivi kama bodi ni nyepesi hutumia mafuta kidogo ,kama bodi ni nzito hutumia mafuta mengi hadi kuchanganya .mfumo wa gea pia huchangia gari kutumia mafuta mengi ,scania ina gea 8-12.yutong model zk3..ina gear 6.injini ni piston 6 ,scania ina piston 8 hivyo uwiano wa mgandamizo hadi kutokea muwako ni mkubwa ,yaani mafuta yanakandamizwa na piston yatatumika mengi .mambo ya transmission haya ni matatizo ya kiufundi yanarekebishika .
we ndugu inaonekana kuwa umetumwa na wachina na hata hoja yako haina mashiko. hebu nenda Iringa panda Yutong halafu mbele yenu ikae scania yeyote au hata nyie mtanglie wakati wa kupanda kitonga halafu uone mziki wa turbo ya scania na ule mluzi wake(turbo) hapo ndio utasema kuwa scania ni noma. acha kudangaya watu lakini. nimepanda new force,green star(zote hizo ni yutong) na hakuna kitu when it comes to Kitonga but scania ooh yeah kama kushuka vile cause pia nimepada scandinavia by then,hood,happy nation na Nganga. wacha kabisa.Wandugu yutng engine zake ni madhubuti asikudanganye mtu. ni za kimarekani toka magari ya MAN. MBIO NDO NYUMBANI KWAKE HAKUNA CHA MARCOPOLO WALA UD.