Yusuph Mlela amtolea mitusi Ney wa mitego kisa Bongo movies kuandamana

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela amemtusi
rapa Nay wa Mitego kwa kile anachodai kuwa
msanii huyo anapotosha jamii juu ya
maandamano waliofanya baadhi ya wasanii wa
filamu nchini.
Mlela%2520na%2520Nay.jpg

Yusuph Mlela ambaye kwenye post yake
ameonekana kushindwa kutumia lugha ya staha
huku akionesha kutokwa na povu jingi kutokana
na mapokeo ya mashabiki wa filamu ambao
walio wengi wamekuwa wakiwachana wasanii
hao na kuwataka kufanya kazi zenye ubora.
Rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa
baadhi ya wasanii wa filamu ambao
waliandamana ni matahira kwani kitendo cha
wao kutaka filamu za nje zizuiliwe hakina tija na
mantiki yoyote.
Kutokana na jambo hilo, ndipo hapo msanii huyo
alipoamua kushusha ujumbe kwa msanii Nay wa
Mitego

"Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa
wewe leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba
nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani
kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa....acha
kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi...
sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka
wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili
uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la
maandamano" alisema Mlela
Mbali na hapo msanii huyo pia ameomba
mpambano na Nay wazichape
"Nay wa Mitego acha kutafuta sifa... nakushangaa
kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo
msanii...halafu huwezi kufananisha filamu na
muziki..... Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya
unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing
kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie
adabu..... This is serous coz we mtoto mdogo tu
kwangu nakupa dole la kati kuongea sana tabia za kike
wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani
chagua popote pale" Yusuph Mlela
Mlela%25201.jpg
 
hili movie ya ney vs mlela lingekuwa uwanja wa taifa na kiingilio nazani uwanja ungefulika
 
Back
Top Bottom