Profesa Ludigo ni miongoni mwa watayarishaji wazuri wa muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva hapa nchini Tanzania, kazi nyingi nyingi za wasanii mwishoni mwa miaka ya 90 zilikua na mikono yake!
Aliganya kazi na P-Funk Majani ndani ya Bongo Record na Master Jay katika studio za Mj Records.
Asilimia 70 ya wasanii waliowika miaka ya 1990's mpaka miaka ya 2005 walifanya nae kazi, ndio maana wanamkumbuka sana, kwani kwa kiasi kikubwa alichangia mafanikio yao.