Yupo wapi mwanaharakati huyu wa UDSM?

Ha ha ha ha ha ha jamaa yangu sana huyu,Mkerewe wa Mwanza...huyu jamb anamwaga sumu kwa Wanafunzi huko Magu,jamaa ni Mwalimu wa History na GS...anamwaga sumu ni balaa kwa watoto,alikoswakoswa sana katika taflani ya Odwang Odor(?)
Me nimemkumbuka sana huyu Mganda Odwagi Odor.
Mwenye habari kumuhusu huyu jamaa atujuze.

Nilipewa simulizi take kwa ufupi na Dada yangu aliyepitia Udsm enzi hizo.

Mwenye kumjua huyu mganda atujuze zaidi.
 
Odwangi Odor hakuwa mtz ...nakumbuka aligombea urais udsm akapigwa chini
 
Aisee alshababu yuko wapi na yule mdada waliongoza mgomo 2010
 
Nakumbuka hata mie nilifunga geti pale mabibo. Na kandamana from mabibo to chuo na tukakaa mataa katikati
 
Uchaguzi uliofuata nikagombea urais wa DARUSO.......a.k.a Jembe, nilitingisha sana bahati mbaya nilikua CONAS na mpinzani wangu mkuu alikua CASS tena BAED unategemea nn hapo.....??? All in all bado harakati zinaendelea Mungu akituweka hai 2020 tutaunguruma mahali, nawasalimu wadau wote mlioko humu
 
Dah, sitaisahau UD katika maisha yangu 2006-009 ilikuwa ni Kama chuo cha nyota za medani jeshini. Kila mtu alikuwa fighter utake usitake nature inakufanya upambane.

Kila semester palikuwa na harufu ya mgomo na kufukuzwa chuo, watoto wa mama na mboga saba waliumia sana kipindi hiki hasa wale wa hall 7
 
Rich alianzia kazi Bukoba na nilikuwa nafundisha naye shule moja ila kwa sasa kahama yupo Mwanza Pamba sekondari....Jamaa ni mwanaharakati hadi leo....
Owawa pia yupo ofisi ya CAG Bukoba
 
 
Radical watoke wapi ,sasa hivi mashoga wengi.

Imagine hadi leo wanafunzi hawajapata field allowances.

Wanafunzi wa siku hizi wanadhani watapewa hela na haki zao na serikali kwa kukodisha matarumbeta na nyimbo za kuisifu


Poor them
 
Huyu alishababy yupo wapi na kabinti kamoja hivi kaa arusha pamoja na sokwe huyu kaemba nazani yupo uvinza halmashauri ila sijui yupo idara gani.
 
Ha ha ha ha ha ha jamaa yangu sana huyu,Mkerewe wa Mwanza...huyu jamb anamwaga sumu kwa Wanafunzi huko Magu,jamaa ni Mwalimu wa History na GS...anamwaga sumu ni balaa kwa watoto,alikoswakoswa sana katika taflani ya Odwang Odor(?)
Yeah alikoswa koswa .Alikuwa noma sana huyu jamaa.Nyakati za migomo mtatiro Alikuwaga anamtumia sana Ku mobilize man power
 
Kuna watu uharakati wao ulihamasishwa na mob psychology ya UDSM, nje ya UD! they are nothing!. Wako wapi kina Sikitiko Kapile , Emile Kivugo, kina Bazigiza baada ya UDSM?!.
P.
But sio Kwa Kaemba mkuu.He was something else
 
Hao kina Owawa and company, Kaemba alikuwa right hand man wao. Harakati zao zisingeweza kufanikiwa bila amsha amsha ya watu kama Kaemba
 
Tulikutakaga story zake nasikia alimchallenge sana kipara??

raisi msaliti aliyepita kwa kishindo
Wakati Kipara anakuwa Rais , Kaemba Alikuwa tayari amemaliza chuo coz Kaemba alimaliza 2009 na Kipara alikuwa Rais 2010/2011.

Ila walikuwa wanajuana coz wote watoto wa Mwanza, Kaemba mkerewe Kipara msukuma ..

And wakati Kipara anaanza first year alikuwa mwanaharakati mzuri sana. Alikuja kuchange baada ya kuingia madarakani
 
huyo odwang alikuwaga mtoto wa joseph koni wa lord resistance army??maana nilikuwaga bado sijajiunga hapo ila story zake nilipata juu juu
Hapana ulikuwa uzushi tu but his father alikuwa mpinzani wa M7 na inasemekana Alikuwa na mkwanja mrefu sana. Hata ishu ya Odong kufukuzwa chuo na.kurudishwa Uganda inasemekana kulikuwa na mkono wa M7 pia
 
Hivi kwann wana harakati wengi wanatokea collage nyingine na sio CoET, au huko kwa wenzetu shule yao nyepesi paka wanapata mda wa kutosha kufanya na uarakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…