Yupi ni baba bora kati ya hawa?

Yupi ni baba bora kati ya hawa?

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,033
Nimesoma kitabu cha mwanafalsafa anaelezea familia mbili zinazolelewa katika mazingira tofauti ila wanaishi katika changamoto za maisha zinazofanana.

Familia ya kwanza watoto wanaambiwa na baba yao waache starehe,dhambi na anasa,wamtii na kumwabudu yeye wakifanikiwa kutii amri atawajengea jumba kubwa ambalo watakuta wanawake/waume wazuri na kila aina ya starehe,huko hakuna kufa,kuumwa wala kulala.,wawe wavumilivu na wenye subira watakuta mambo mazuri sana na wasiotii amri atawaadhibu kwa kuwachoma moto.

Upande wa pili wa familia baba yao amewasii watoto wasiwe na dhambi,wafuate amri zake na wamsifu yeye na kumwabudu yeye, na ametoa ahadi wale watakaofanikiwa atawajengea jumba la kifahari ila huko ni kuimba na kumsifu baba yao milele na milele kwa Mara nyingine.,wale wasiofuata atawaadhibu kwa moto.

Mwana jf UPI mtazamo wako unadhani yupi ni baba bora hapo na anawapenda watoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna baba bora hapo.
Baba bora hawez kuwa centralized
Sifa zote apewe yy
Yeye tu ndo wakuabudiwa
Yeye tu ndo atukuzwe
Huyo baba sio bora na hatokaa kuwa bora


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa ubinadamu wangu, Baba wa mwanzo ni Bora. Kwani Nani asingependa kwenda kukutana na starehe za kila aina na mabinti wazuri wa kumwaga mpaka kusaza? Besides, hata kwa maisha ya sasa tu kusifu na kuabudu 24/7 sio KAZI rahisi jamani, mi concentration yangu ni <2 hours.
 
Nimesoma kitabu cha mwanafalsafa anaelezea familia mbili zinazolelewa katika mazingira tofauti ila wanaishi katika changamoto za maisha zinazofanana.

Familia ya kwanza watoto wanaambiwa na baba yao waache starehe,dhambi na anasa,wamtii na kumwabudu yeye wakifanikiwa kutii amri atawajengea jumba kubwa ambalo watakuta wanawake/waume wazuri na kila aina ya starehe,huko hakuna kufa,kuumwa wala kulala.,wawe wavumilivu na wenye subira watakuta mambo mazuri sana na wasiotii amri atawaadhibu kwa kuwachoma moto.

Upande wa pili wa familia baba yao amewasii watoto wasiwe na dhambi,wafuate amri zake na wamsifu yeye na kumwabudu yeye, na ametoa ahadi wale watakaofanikiwa atawajengea jumba la kifahari ila huko ni kuimba na kumsifu baba yao milele na milele kwa Mara nyingine.,wale wasiofuata atawaadhibu kwa moto.

Mwana jf UPI mtazamo wako unadhani yupi ni baba bora hapo na anawapenda watoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa tatizo hiyo nyumba itakua na WI-FI?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo hapa...[emoji30][emoji30][emoji30]
tapatalk_1547552950903.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom