Yule daktari akaniharibia kwa wife…..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yule daktari akaniharibia kwa wife…..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 6, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hatukuwa na vita kali sana na mke wangu, isipokuwa tatizo lake lilikuwa tukikorofishana kidogo zinaweza zikapita wiki mbili hadi tano anazira kuzungumza nami. kwa kweli hii tabia yake ilinichochea kuanza kuwa na uhusiano wa nje ili kupata ‘kampani.'

  Hata hivyo hakuwa na uhakika kwamba, nina uhusiano wa nje ingawa alikuwa akihisi kwa kiasi cha kutosha. Kiasi cha miaka minane iliyopita tabia yake ya kuzira na yangu ya kutoka nje ya ndoa ilizua la kuzua.

  Ilikuwa hivi: siku moja niligombana kidogo na mke wangu na nikamtolea lugha chafu. Kitendo hicho kilichukua wiki tatu bila kuzungumza nami. kwenye ile wiki ya pili tangu kufungiwa milango ya mazungumzo, nikapata tatizo. Kwenye hangaika yangu, nilikwaa maradhi ya zinaa.

  Ilibidi nipige hesabu ya hospitali. Mke wangu alikuwa ni muuguzi kwenye hospitali moja ya serikali ambayo ndiyo niliyokuwa nikitibiwa. (Naomba nisiitaje). Niliogopa ningeweza kukutana naye na hata kama hataniuliza mimi, angewauliza madaktari tatizo langu.

  Hivyo niliamua kwenda hospitali nyingine ya binafsi. Nilipofika niliingia kwa daktari ambaye alinichangamkia sana. (Nawashauri kwamba, siku ukienda mahali ambapo unajua hujuani na mtu halafu akatokea mtu akakuchangamkia sana, jiulize mara mbili).

  Huyu daktari aliniuliza kama nimeoa, ambapo nilimdanganya kwamba sijaoa. Akaniuliza kama naweza kumkumbuka mtu aliyeniambukiza ili nije naye pale apate huduma. Nilidanganya kuwa amesafiri.

  Yule daktari aliniandikia dawa na kabla hajamaliza kuandika alitoka nje akiniomba radhi kwamba, anarejea punde.

  Nilikaa kusubiri daktari arejee. Kama dakika kumi baadaye, nikiwa nimeboreka, niliona mlango ukifunguliwa. Halafu nilimuona daktari. Lakini nyuma ya daktari kulikuwa na utata. Nilimwona mke wangu akiwa katika sare zake za uuguzi. ‘samahani. Nimetaka uje uone jinsi watu wanavyofanana. Mimi nilidhani ni shemeji mumeo.' Alisema daktari akimwambia mke wangu.

  Halafu alinigeukia, 'samahani, yaani nmnafanana na mume wa huyu muuguzi wetu, yaani basi tu.'

  ‘Anaumwa kitu gani?' Mke wangu alimuuliza daktari.
  Yule daktari akamjibu, 'ni siri yangu na mgonjwa. Nilitaka tu uone maajabu ya kufanana yalivyo. Nilimwona mumeo ile siku ya harusi tu, lakini sura naikumbka bado. Wanafanana sana kwa kweli….'

  Mke wangu alimkata kalima daktari. ‘Ni yeye kweli. Nashangaa anajifanya hanijui mkewe. Na ndio maana nakuuliza anaumwa kitu gani? Mke si ana haki ya kujua mumewe anaumwa nini?' Yule daktari akijifanya hakuwa anajua hilo alisema, ‘aisee ni jambo la kusikitisha. Mumeo ana matatizo ya gonorea……'

  Mke wangu aliruka kwa hamaki na kusema, ‘ati nini, ana kitu gani?' Yule daktari alimwambia mke wangu atulie. Nilisimama nikiwa na hasira hasa dhidi ya yule daktari.

  Inakuwaje akamwite mke wangu na kumpa taarifa ile! Sura ya daktari yule kwa mbali niliikumbuka sasa, ni kweli alikuja kwenye harusi yetu. Alikuwa ni rafiki wa kaka wa mke wangu.Wakati nataka kutoka, yule daktari alisema, ‘usikasirike, ni vyema tuyazungumze yaishe. Ni jambo la kusikitisha, mkeo kuniambia kwamba tangu ahamie kwenye hospitali yetu kwa takriban siku kumi sasa, wewe hujui, eti kwa sababu hamzungumzi.'

  Yule daktari alijitahidi kuwa na diplomasia akijaribu kututaka tujadili jambo lile likiwemo la gonorea ili tuyamalize. Mke wangu alikuwa mkali kama pilipili na hakutaka kumpa yule daktari nafasi ya kusuluhisha ugomvi wetu.

  Hata hivyo baada ya daktari yule kutumia busara ya hali ya juu, hatimaye mke wangu alitulia na tukayazungumza na kuyamaliza na sasa ndoa yangu ni imara kuliko kawaida.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Jamani hii kitu ni ya kitambo sana, msije mkadhani ni ya hivi karibuni.....LOL
   
 3. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .. ameshaacha kabisa kununa?
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Najua kuna watu humu watai - treat hii maneno kama vile imetokea jana.... Acheni hizo....LOL
   
 5. awp

  awp JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  pole na mshukuru daktari kwa kuwaweka sawa, japo ulitaka kumalaumu.
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  yeah lile lilikuwa ni soma tosha, siku hizi tunakwenda sawa.......
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  aliharibu bana, kulikuwa na haja gani kutangaza kwa wife kama nina gonorea...
   
 8. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  MTAMBUZI sasa hio gonorea uli-ipatia wapi :biggrin:
   
 9. awp

  awp JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Una mke HAPANA, una rafiki KASAFIRI, daktari akafanya umbea wa kufananisha ikabidi aweke mambo hadharani baada ya kubaini kuwa wewe ndiye shemejie wa ukweeeeeeeeeee. naona ulikuwa mdogo kama piritoni
   
 10. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,964
  Likes Received: 6,738
  Trophy Points: 280
  Ee bwana nimeipenda hii stori, lakini usiombee ikutokee, maana unaweza ukanywea, ukawa mdogo kama kidonge cha piriton, Na ukajikuta unampigia magoti 'my wife' na kuomba chonde chonde ili akusamehe!!
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Uswazi madaktari hawana siri
  ndo maana wanaokwenda kuchukua arv wengi wanatoka dar
  wanaenda kibaha lol
   
 12. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ulipata kadi ya njano hivyo kuwa makiniunatotoka nje maana afadhali ya gono kuliko ungepata Hiv.
  Tunashukuru kwa somo maana kupitia kwako tunajifunza pia,ndoa zina mambo ili uyaone ni paka uingie.
   
 13. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mkuu hili ni neno la kiswahili au macho yanguuuuuuuu
   
 14. awp

  awp JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  typing error mkuu i mean KUMLAUMU
   
 15. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Siku zote migogoro ktk ndoa zina faida chanya na hasi, wakati mwingine hubomoa na wakati mwingine hujenga, ila migogoro ambayo haitafutiwi suluhu huwa ni sum ambayo inaweza kuua ndoa na hata uhai. Mgogoro huo umepelekea kuiimarisha ndoa baada ya suluhu
   
 16. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 994
  Trophy Points: 280
  Haya wale wa ku-copy na ku-paste ivitieni kasi na hii.
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hahahahahaha mtambuzi daktari alikukomeshaaa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Kila jambo linasababu yake,hilo tukio hapo hospitalini ilikua ndo njia ya kupatanishwa na mke wako mpaka leo mnaelewana
   
 19. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  njia ya mwongo ni fupi kama alikuwa anamdanganya mke anatoa nje ndio hayo matokeo na kama alikuwa anajificha Mungu alitaka kumudhihirishia yeye hafichwi chochote ninaimani kutoka na hili somo kunawengi watajifunnza maana tunajificha kwa binadamu. Je, kwa Mungu ionakuwaje?
   
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kazi kweli kweli.
   
Loading...