Yule changu akaniletea noma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yule changu akaniletea noma!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Dec 27, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumapili mwaka 2000, wakati huo ndio ujana wangu ulishika kasi na nilikuwa napenda kujirusha ile mbaya. Nilikuwa naishi maeneo ya Mwenge, lakini maeneo yangu ya kujirusha yalikuwa ni Mwananyamala, kwani ndiko nilikokulia. Siku hiyo ya tukio nilikuwa na marafiki zangu maeneo ya Kinondoni, tukipata moja moto moja baridi, mara wakajitokeza mabinti watatu, lakini mmoja alionekana kufahamiana na mwenzetu moja tuliyekaa naye, wale mabinti walikuja na kujumuika nasi. Tuliendelea kunywa na kupiga soga.

  Miongoni mwa wale mabinti, alikuwepo mmoja ambaye nilivutiwa naye, na nikawa napiga naye stori. Baada ya kufahamiana tuliendelea kupiga stori na kutokana na mihemko niliyokuwa nayo nilijikuta nikianza kumshika shika yule binti bila ya aibu, kwani pombe zilishakolea kichwani. Mara ghafla simu yangu iliita na nilipotaka kuipokea ile simu ikakatwa, niligundua kuna ujumbe kwenye simu yangu, niliufungua ili kuusoma, ujumbe ule ulitoka kwa mmoja wa wale marafiki zangu tuliyekaa naye pale kwenye meza. Alinitaka nimfuate akienda msalani ili tuongee, nilimjibu kwa kifupi tu kuwa nimemuelewa. Alipopata ujumbe wangu alinyanyuka na kuelekea msalani. Nilimfuata.

  Tulipofika msalani aliniuliza kama namjua yule binti niliye naye, nilimjibu kuwa simfahamu kwa kweli. Alinitahadharisha kwamba yule binti ni changu mwanafunzi (Yaani binti anayejiuza) na wale alioongozana nao ni magwiji wa tabia hiyo na inaonekana wale ndio waalimu wake. Alinitahadharisha kwamba kama nitaondoka naye niwe makini. Nilimkubalia kuwa nitakuwa makini na wala asihofu. Kwa kawaida nikiwa na mwanamke sikuwa na jeuri ya kumpeleka mahali ninapoishi kwa sababu mwenye nyumba wangu alikuwa anapangisha wapangaji waliooa na hakupenda mtu asiyekuwa na mke akae katika nyumba yake. Mimi nilifanya usanii wa kumpeleka binti mmoja kwa makubaliana ya kumlipa ili nimtambulishe kuwa ndiye mke wangu, lakini nilimjulisha mama mwenye nyumba kwamba mke wangu huyo anakwenda kusoma nje nchi na atarudi baada ya miaka miwili. Nilidanganya kuwa atasafiri kwenda kwao kuaga siku inayofuata na akirudi ndio ataondoka kwenda Ughaibuni kusoma. Nilikubaliwa kupanga katika nyumba ile, ikanilazimu kuishi kwa nidhamu ya hali ya juu ili nisije haribu.

  Tulikubaliana na yule binti kuondoka naye, na nililazimika kuchukua chumba katika nyumba moja ya wageni iliyopo maeneo hay ohayo ya Kinondoni. Tulipofika binti alikwenda kuoga akiniacha pale nikiangalia TV, nilitumia muda ule kuficha fedha zangu kwenye mfuko wa siri kwenye bukta yangu, aliporejea na mimi nilikwenda kuoga na niliporudi bafuni nilimkuta akijikwatua. Wakati najiandaa kupanda kitandani akataka kujua asubuhi ataondokaje. Nilimuuliza dau lake ni kiasi gani, akaniambia elfu ishirini, nikamwambia siwezi kulipa hiyo hela kwani ni ghali sana, akaniuliza nina kiasi gani, nikamjibu kuwa nina elfu kumi akaniambia labda kama itakuwa ni ile ya chapchap aondoke zake lakini siyo kulala. Tulivutana, kisha tukakubaliana nimlipe elfu kumi na tano. Kwa kuwa nilitakiwa kazini alfajiri, nilitega alam ya simu yangu ya mkononi iniamshe kisha tukalala. Alfajiri simu iliniamsha nikaamka na kujiandaa haraka haraka, nilipomaliza kujiandaa nikajaribu kumuamsha yule binti lakini alikuwa amelala fo fo fo. Niliondoka bila kumuaga wala kumuachia hela yake, nikijua nitakutana naye viwanja.

  Nilifika kazini na kuendelea na kazi kama kawaida, lakini ilipofika saa nne nikapata taaarifa kuwa naitwa kwa meneja muajiri, nilishtuka maana kuitwa kwa meneja muajiri ni jambo ambalo wakati mwingine haliashirii mema. Nilikwenda kwa meneja muajiri na nipofungua mlango nikakutana uso kwa uso na yule binti wa jana niliyemtelekeza pale nyumba ya wageni, nikajua mambo yameharibika. Meneja muajiri alikuwa ni mwanamke wa makamu na alikuwa na busara sana, aliniambia kwa kifupi. Huyu dada ameokota kitambulisho chako lakini angependa muongee kwanza hivyo nendeni chumba cha pili mkishamalizana muje munijulishe nijue yameisha. Tulienda chumba cha pili, huku nyuma yule meneja aliguna kwa kebehi, niligeuka kumuangalia akabinua midomo kwa dharau.
  Tulipofika pale nilimuomba kitambulisho changu na kumpa hela yake, alikataa kupokea ile hela akidai nimuongeze elfu tano za usumbufu, sikutaka kubishana naye kwa sababu sikutaka yawe makubwa nilimpa elfu ishirini kisha akanipa kitambulisho changu.

  Nilimuuliza sababu ya kunichomolea kitambulisho changu kwenye pochi, akanijibu kwamba alikuwa haniamini na alifanya hivyo ili kuepuka kudhulumiwa na wanaume wakware kama mimi. Nilipomuuliza kama alimweleza nini bosi wangu, hakutafuna maneno aliniambia dhahiri kwamba alimweleza yote kuhusu mkataba wetu wa kufanya ngono kwa malipo na mimi kumtoroka. Ni bahati nzuri tu alinichomolea kitambulisho changu kwenye pochi usiku wakati naoga. Nilifadhaika sana.
  Tulitoka pale na kwenda kwa meneja muajiri kumjulisha kwamba tumemalizana, alimruhusu yule binti na akaniomba nibaki ili tuzungumze. Nilikaa nikiwa nimetahayari kweli.

  Alinitazama kwa nukta kadhaa kisha akafungua droo yake na kutoa kijitabu kidogo na vipeperushi kadhaa vinavyozungumzia juu ya athari za ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa…………… Alinitaka nikasome kwa makini kisha tuonane wiki inayofuata kwa mazungumzo zaidi.
  Niliondoka pale ofisini kwa meneja mwajiri nikiwa nimefedheheka na tangu siku ile nikawa nikiwaona machangu nawaogopa kama ukoma.

  Hii inamuhusu rafiki yangu na wala sio mimi…………………………………LOL
   
 2. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  amekomaje mmh, ila umeielezea vzr kama inakuhusu ww lol.
   
 3. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  mkuu pole sana.... ...but ulitumia kinga aka ndom?
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280

  Aaaaaaaaaaaaaaaaaah Mtambuzi hiyo sentensi hapo juu imeharibu mkuu.........................
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haikutumika aisee, Ulevi........ Nooma
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ipotezee kiushkaji, nina wanangu na wajukuu humu...............LOL
   
 7. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Duh! hiyo ni noma mkuu!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa noma, lakini nime-survive...............!
   
 9. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  chonde chonde ulevi nomaa, bora we umeeleza ukweli wengine humu tuna wake lakini kila siku utasikia mi naenda kunywa buguruni sijui kinondoni kumbe wanachotafuta mh!
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Naenda kusema kwa mama, kuseeeeema!
  Kule nyumbani umamuachia bukuuuuuuu...<Singing happily>
   
 11. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  town hapa, aliyeuza cheni feki kalipwa fedha ya bandia! akili kumkichwa
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilishasema hii inamuhusu rafiki yangu wala siyo mimi......................LOL
  Nikisikia umemwambia mama yako, nitakutwanga makwenzi!
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mhh! Story kwa hisani ya mtambuzi.
  Compile bwana watu tupate ajira
   
 14. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hahaha unanichekesha mtambuz.
  kizaz cha jakaya hao wana mambo.
  na watakula bamia wk nzima, akienda kusema lol.
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nikachomekea kwamba hiki kisa kinamuhusu rafiki yangu............ Si umeona wanangu wameshaanza unoko! wako wengi hao.........
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Uzee dawa Kongosho, nimepambana na visa na mikasa mingi sana.............. Na ndio maana nikipata fursa naweka ushuhuda watu wajifunze.>>LOL
   
 17. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mtambuzi hata wewe? Loh
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Siyo mimi jamani, ni rafiki yangu, mbona mnanisingizia................ Ngoja niseme na Mods, aiondoe hii habari, maana naona inaniletea noma sasa..............................
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Inaniuma sanaaaa! Leo patachimbikaaaa! ( Unless zile nguo za xmas ukatukopee woolworths! Hehhee, blackmailing timely!)
   
 20. Darlingtone

  Darlingtone JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera...

  Sijui ungekuwa huna hiyo elfu 20 ingekuwaje
   
Loading...