Mwanahabari kuna mengi ambayo wewe huyafahamu, siasa ni mchezo mchafu usizikurupukie njiani ukadhani unazijua siasa, huyo Naeem Gire ambaye ni mshiriki wa Lowassa kwenye richmond, mimi nimesoma naye pale shaaban robert sec school, namjua vizuri sana yeye na biashara zinazomuweka mjini. Usipende kudanganywa na majibizano ya kisiasa ana then ukaamua kuchukua upande fulani kirahisi tu, utadanganyika na siku ukigundua kuwa umeongopewa utaumia sana moyo wako, kwani utajiona mjinga. Lowassa kutashitakiwa na kutopelekwa mahakamani sio kigezo cha usafi wake. Huyo mzee alishakataliwa na waasisi wa nchi hii, alishakosa radhi ya wakuu kabisa waliolianzisha taifa hili. Naeem Gire kushirikiana na Lowassa kwenye kampuni ya kuzalisha umeme wakati wa Gire ni mmiliki wa stationery, kilikuwa ni kitu kibaya sana kwa uongozi wa Kikwete, na Kikwete alikuwa very diplomat katika kumshughulikia mmeru. Kama mmeru angekutana na aina ya viongozi wenye vichwa vibovu, angekuwa kwenye nafasi mbaya sana kwa sasa. Itoshe kukushauri tu ndugu yangu mwanahabari, usiwaamini sana wanasiasa wenye nia za miaka mingi za kuwa marais, wako tayari kufanya lolote lile ili mradi lengo lifanikiwe.