Yuko wapi Roho 7?

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,410
8,806
'' Nakupenda sana hip hop,
Zaidi ya machizi wangu wa kitaa, acha wale naokesha nao Baa... ''

Hizo ni ladha katika moja ya kazi zake zilizowahi kubamba sana hapa Bongo in hip-hop community. ROHO 7, emcee mwenye 'flow' fulani hivi isiyochosha kusikiliza.

'Nakupenda HipoHop' , 'Waite Polisi' , ni kazi zake zilizowahi kutikisa sana masikio na mioyo ya wapenda michano.

Ni miaka kadhaa sasa galacha huyu yupo kimyaa sana.

Nini kilimpata Roho 7? Yupo wapi mkongwe huyu, au nae kasanda gemu?


- Kaveli -
 
Nilikuja kupata stori zake alikuwa anasoma Tumaini Iringa law department,kumbe ile stori ya waite polisi ni kweli ilitokea Iringa enzi zile dem kweli alikuwa na mshkaji chuo kumbe waarabu wa oman nao wanatunza,sijui yukwapi mh Jackob Kindole kama nipo sahihi sijui ila alikuwa iringa.
 
Last time nilionana naye Iringa,
Tulikuwa tuankutana naye sana kwa prodyuza moja anaitwa Amba,
Amba alivyomaliza jamaa sikumuona tena.
 
umenikumbusha mbali sana kuhusu huyu jamaa,nilisoma nae tumaini chuo pale. sasa hivi ni mwanajeshi hajishughulishi sana na music
 
umenikumbusha mbali sana kuhusu huyu jamaa,nilisoma nae tumaini chuo pale. sasa hivi ni mwanajeshi hajishughulishi sana na music
ana nyota tatu yani ni captain na jeshi limemkataza kuimba
 
Naskia jamaa amekuwa Mjeda..
ITABIDI TUSUBIRI MPAKA ATAKAPOSTAAFU JESHI,
HUENDA AKAENDELEZA HARAKATI ZA MUZIKI
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Jamaa Ni Mwanajeshi Kwa sasa Kama walivyosema Memba wengine Hapo Juu.. Nna Nyimbo Zake kAdhaa Kama 3 Hivi Nmeziweka soundclooud kwa atakaetaka kusikiliza

Hii Inaitwa Sikio Lakufa Ama Waite Police


Hii Inatwa Hip Hop

Video Yake hii Hapa

pia Nyimbo hii Aliirudia Yaki akaiita Bila wao
Video Yake Hii Hapa

Audio Yake Hii Hapa Chini


Hii inaitwa Crazy Aliifanya Kwa amba Akimshirikishaa Yule binti farida Wa Mwanza (Inasemekana alikua mpenzi wake)
 
Jamaa alikuwa anakuja vizuri kiwango chake hiki leo kuna vijana wengi wanakaa hawamuwezi wacha alinde mipaka yetu hapo ndo unapojua kuna watu muziki unawakimbilia na wengine unawakimbia.
 
Waite polisi ili wamchape punda mzigo uweze kwenda. Huyu jamaa anajua Waite polisi ni Bonge ya ngoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom