Yuko wapi Job Ndugai Naibu Spika?

Yuko wapi Job Ndugai Naibu Spika?

Ngugai, alikuwa anasumbulia na Koo, pia kisukari , ila kwa sasa yupo mzima wa afya, yupo kwenye Jimbo lake kwenye shuhuli za ujenzi wa chama.

Ni kweli alikuwa na matatizo ya kiafya, ila kwa sasa ni Mzima wa afya.
 
Wakuu nafikiri tangu alipoacha kuliongoza bunge letu wakati wa sakata la escrow hajawahi kuonekana tena akiongoza vikao vya bunge naibu spika wa bunge mh Job Ndugai na sasa bunge hilo huwa linaongozwa na spika na asipokuwepo huwa likiongozwa na m/kiti Zungu, binafsi najiuliza tu yu wapi naibu spika wetu maana bunge lililoisha hakuonekana kabisa na la sasa pia hii ni wiki ya pili tangu bunge lilipoanza vikao vyake lakini hajaonekana hadi sasa je ni nini kimempata mh wetu ilihali ni juzi tu nimemuona kwenye ziara ya kinana katika jimbo lake la kongwa tena akiwa ni mzima wa afya tele.

Nawasilisha
 
Duuuuu umetukumbusha, alifukzwa na kupotezwa wakati wa escrow hadi kesho hapewi nafasi kabisaaaa, pole ndugai ushirika na wezi lazima uwe mwizi sugu, ukisita kidogo lazma kushughulikiwa
 
Duuuuu umetukumbusha, alifukzwa na kupotezwa wakati wa escrow hadi kesho hapewi nafasi kabisaaaa, pole ndugai ushirika na wezi lazima uwe mwizi sugu, ukisita kidogo lazma kushughulikiwa

Yaani hawa watu ni shida tangu aondolewe kwenye lile sakata hajapewa tena nafasi na sijui mwisho wake ni nini ngoja tuone
 
Kimepita kipindi kirefu sasa tangu mwanzo wa sakata la ESCROW Naibu spika huyu aliondoka kuelekea ng'ambo kwa matibabu.
Lakini tangu amerejea hajaonekana katika vikao mbalimbali vya Bunge hata hakuweza kuhudhuria mazishi ya rafiki yake Marehemu John Komba.
Alionekana tu katika ziara ya Kinana mkoani Dodoma lakini amepotea tena bila taarifa yoyote.
Je, zile tetesi kwamba anaumwa zaweza kuwa na ukweli?
Je, Serikali imemtenga kutokana na msimamo alioonesha awali katika kushughulikia mjadala wa Escrow?
Je, ameamua kujijenga zaidi katika jimbo lake kutokana na hofu ya uchaguzi wa Octoba?
Mwenye taarifa zaidi atujuze.
 
Nami nimeona kwanza kakaa kiwogawoga tu!! halafu si yule ambaye siku zote huwa makini katika utendaji wake....anyway time will tell.

Sio Makinda tuliyemzoea. Nadhani incompetency ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inamkwaza na anahofia hakuna mpangua hoja.
 
Nilikuanae ndege moja kutoka India kuja Mpaka Dubai Mpaka Dar lakini Sijui alienda kufanya nini wala hakuonyesha kua mgonjwa...
 
Back
Top Bottom