Yuko wapi huyu siku hizi?

zaratustra

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
849
225
Wakuu tangu wiki hii imeanza, nimemkumbuka sana bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Manase Muhaha a.k.a Mgogo (yaani ndo leo nimelikumbuka jina lake), alikuwa mchangiaji maarufu sana wa mada mbali mbali redioni, hasa redio one na redio tumaini (kipindi cha Jirani) hasa miaka ile ya mwishoni mwa '90. Inawezekana kutokana na majukumu sisikilizi sana redio siku hizi kwa hiyo siwezi kumsikia, lakini kwa vyovyote hata kwa bahati mbaya ningeweza tu kumsikia hasa ninapokuwa kwenye vyombo vya usafiri vya jamii! Kama kuna anayejua habari za huyu bwana aliyekuwa mahiri katika kujenga na kutetea hoja zake pia kujivunia kabila lake na hata kuongea lugha ya kwao ilikuwa burudani sana, (naamini kwa wasikilizaji wengi!), tafadhali anijuze!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom