Yuko wapi Emmanuel Nchimbi?

Yuko wapi Emmanuel Nchimbi?

Nadhani kuna watu hawajui maana ya unafiki. Unafiki ni mtu kufanya vitu kwa siri. Lakini Nchimbi hakuwa mnafiki alisimamia anachokiamini.
kwani polepole kwenye katba mpya nafasi ya ukuu wa wilaya alikuwa hasimamii anachoamini? mbona amekuwa mkuu wa wilaya na si huyu leo tunamwita mnafiki? au unafiki ni cheo kwamba kinachagua watu na watu?
 
Nchimbi na Sofia hawakua wanafiki maana waliweka wazi msimamo wao, maana hawezi kufanya hivo. Na wala hawakua na kosa Lolote maana kile kilikua kipindi cha uchaguzi na kuwa na makundi haikua tatizo
kosa ni kutoka katka kikao cha kamati kuu.
 
eti kada maarufu mnyika yupo wapi hata mimi simsikii kabisa,kijana alikuwa machachari sana kuhamasisha vijana nchini kupambana dhidi ya ufisadi ndani ya nchi,lakini baada ya uchaguzi hatumuoni tena na makeke yake kimempata kipi??
 
Habari za leo wana jamii,

Napenda kujua huyu kada nguli kabisa toka enzi za umoja wa vijana mpaka kuja kuwa waziri na sasa amepotea kama upepo uvumao. Namuulizia Emmanuel Nchimbi maana naona wengine wanaukwaa ukuu wa mikoa, ubalozi.

Yeye nini hasa kimempata mpaka kuwa kimya hivi. Hata kwenye vyombo vya habari haonekani. Napenda tu kujua maana ni makada waliongoza harakati za kuitetea CCM iwe mvua iwe jua walikua tayari hata kufa chama kibaki.

Nawasilisha.
Swali hili muulize Mheshimiwa Lowassa. Atakujibu kwa ufasaha sana.
Hii ndo si hasa.
 
Wengine wameachana na siasa kimyakimya.
Iko siku Nchimbi nae atakuja kuwa Rais, sasa hapo itakuwa kazi! Kwanza atengue woote walio teuliwa kimagumashi halafu achunguze kama serikali iliyo mtangulia ilifanya mambo kwa kuzingatia Katiba ya JMT!
 
Hivi huu utoto huku JF utaisha lini? Nchimbi, sofia simba na wale wengine hawakuwa wanafiki wao walitamka hadharani hawakukubaliana na kilichotokea, unajua maana ya unafiki? utoto utoto utoto utoto.
tunamwita ni mnafiki kwa sababu alitoka kwenye kikao cha kamati ya maadili kwa kutokukubaliana na kilichokuwa kinafanyika, lakin baadae akamwunga mkono yule aliyeptishwa "kwa njia isiyohalali". sasa hapo huoni hiyo ni ishara ya mtu mwenye ndimi mbili?. mnamwita POLEPOLE ni mnafiki kwa sababu kile alichokuwa anahubir na anachokitenda kwa sasa ni vitu viwil vinavyotofautiana the same to nchimbi.
 
Mh!!na Lazaro nyalandu nae yuko wapi muleta mada!!au bado yuko nchi za wenzetu?
 
Nadhani kuna watu hawajui maana ya unafiki. Unafiki ni mtu kufanya vitu kwa siri. Lakini Nchimbi hakuwa mnafiki alisimamia anachokiamini.

Kusimama na kusema Hukubaliani kwa Uamuzi wa CC kukata majina ya watu wanaokubalika na kuchagua wasiokubalika halafu Mwisho wa Siku unabaki kumkampenia mmoja wa watu uliopinga kupitishwa kwake na kuacha kwenda kumkampenia uliesema anakubalika kunaitwaje kama si Unafiki?
 
Dr Nchimbi hakuwa mnafiki,ipo siku chama chake kitamtendea haki,kama walivyomkumbuka Philipo Malmo makamu mwenyekiti wa CCM bara
Philip Marmo hajawahi kuwa Makamu Mwenyekiti wetu labda ulimaanisha Philip Japhet Mangula.
 
Jembe la kupitisha madawa ya kulevya JNIA na kina Kinje.. Hapa kazi tu unafiki tupa kule.

Basi kama alikua anapitisha dawa za kulevya na wewe unajua. Basi tuna matatizo kuliko tunavyofikiri.
 
Nasisitizia hiyo namba3 Inasemekana MTU aliekuwa anampa Homa kwenye UVCCM alikuwa Kijana wa Mzee MALECELA simkumbuki Vzr jina lake Bahati Mbaya alifariki wakiti minyukano ya kuusaka ukuu ikiwa inaendelea
Anaitwa Ipyana Malecela.
 
Iko siku Nchimbi nae atakuja kuwa Rais, sasa hapo itakuwa kazi! Kwanza atengue woote walio teuliwa kimagumashi halafu achunguze kama serikali iliyo mtangulia ilifanya mambo kwa kuzingatia Katiba ya JMT!
Jamaa amepotea kabisa katika medani za kisiasa!
 
Collective responsible kivipi? Kila mtu si ana maamuzi yake hizi siyo enzi za chama kimoja we vipi?
Kumbuja Dr Nchimbu na wenzake Kimbisa na Sophia Simba walikuwapo ndani kwenye Kikao cha maamuzi, kama kulikuwa na jambo halikuwa sawa walikuwa na nafasi ya kulikataa ndani ya vikao na ndiyo utaratibu huo unaokubalika, ukifanya kitu tofauti na mlichokubaliana kwenye vikao vyenu huo ni UNAFIKI na ndicho walichokifanya sasa ww hauelewi nini?
 
Back
Top Bottom