Habari za leo wana jamii,
Napenda kujua huyu kada nguli kabisa toka enzi za umoja wa vijana mpaka kuja kuwa waziri na sasa amepotea kama upepo uvumao. Namuulizia Emmanuel Nchimbi maana naona wengine wanaukwaa ukuu wa mikoa, ubalozi.
Yeye nini hasa kimempata mpaka kuwa kimya hivi. Hata kwenye vyombo vya habari haonekani. Napenda tu kujua maana ni makada waliongoza harakati za kuitetea CCM iwe mvua iwe jua walikua tayari hata kufa chama kibaki.
Nawasilisha.
Kwanza kwa wanaomfahamu Nchimbi siyo mtu anayeweza kuitwa mwanasiasa Nguli. Nchimbi alibebwa na mambo machache
1. Family background- anatokea kwenye familia iliyokuwa na uongozi wa kisiasa
2. Students politics za Mzumbe zilimwigiza UVCCM
3. Wakati anaingia UVCCM hapakuwepo strong character hivyo ikawa rahisi kupenya
ILa, Nchimbi siyo strong politician is very average character kwenye mambo mengi.
Kuhusu kutoteuliwa katika teuzi za Magufuli zinazoendelea, jibu ni jepesi sana- Emanuel Nchimbi ndiye aliyeitisha kikao na waandishi wa habari na kueleza kwamba Chama hakifuata utaratibu katika kukata jina la Lowasa