pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 262
- 522
Mwanzoni mwa mwaka wa elfu mbili kulikuwa na sijui nimuite tabibu ama shehe huyu alikuwa anapatikana maeneo ya kunduchi nadhani ni mbele kidogo na ilipo kambi ya jeshi alikuwa anatibu kwa dua kisha anakuchoma sindano fulani hivi ambayo imewekwa dawa za kienyeji binafsi huwa namkumbuka sana pia namuona ni mtu muhimu katika maisha yangu kwani aliweza kunifanya niachane na madawa ya kulevya, nilikuwa muathirika mkubwa sana kiasi cha kulala nje ukipita pale kinondoni American chips lazima unikute nasinzia siku moja ndugu zangu wakanishauri wanipeleke kwa huyo babu ila hakuwa babu kiumri bali ni jina tu nikaanza kwenda pale ambapo alikuwa nakumbuka tulikuwa watu weeeengi saana kila mmoja na shida yake ila kilichoni shangaza ni kwamba alikuwa anatutibu wote kwa dawa moja ni watu maelfu kwa maelfu halafu alikuwa hatozi chochote anasoma duwaa kisha tunaitikia amin kwa muda kama lisaa limoja kisha tunakwenda kuchoma sindano ambazo zilinifanya niwe nalala sana na kupiga chafya kwa nguvu mpaka nikaacha madawa kabisa badae nikashindwa hata kuvuta sigara tena nazungumzia miaka 13 iliyopita naamini kuna mwana jukwaa atakuwa anamfahamu huyu kaka je yuko wapi siku hizi? Nakumbuka tiba alikuwa anatolea kwenye kasri lake la ghorofa lililopo maeneo ya kunduchi ila kwa wingi wa watu tulikuwa tunaketi uwanjani....dah kitambo sana