Yuko wapi aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe?

Wakuu kama ilivyokuwa kwa Kinana, Balozi Membe hajaonekana kwenye matukio makubwa ya kitaifa kuanzia msiba wa Hayati mpaka shughuli za kitaifa zilizofuatia

Yuko wapi? Kama sikosei muda mchache kabla ya uchaguzi alienda zake Dubai na sina kumbukumbu kama alirudi tena nchini. Nadhani hisia zake za kijasusi kipindi kile zilimshawishi ulikuwa ni wakati sahihi yeye 'kukimbia'
Kasha maliza kazi yake ya kuchomoa betri.
 
Wakuu nimeona niulize jambo hili huyu mzee jasus na mwanadiplomasia nguli yupo wapi inasemekana kwamba zile dakika 89 za kufunga goli alitoka sare ikabidi apewe dakika za nyongeza akashinda mechi baada ya kushinda mechi aliamua kwenda ungaibuni
 
Ahaaa, unamsema joka la mdimu.....atakuwa karudi juu ya mdimu kuwadhibiti wale wanaotaka kuangua matunda ya mdimu.
 
Hakuna kazi yoyote aliyopewa Membe. Huyu mmakonde ali underestimate upepo wa siasa za kibongo.

Apumzike tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom