Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Siku moja Yesu alimtuma Yuda akanunue kuku saba kwa ajili ya sherehe.Katika kuwaandaa wale kuku,Yuda aliiba mguu mmoja kwa kila kuku.Wakiwa mezani Yesu akahoji;Yuda,hapa kuna miguu 7 ya kuku,miguu mingine 7 iko wapi?Yuda akajibu,"yaani mkuu mpaka leo hujui kwamba kuku hutembea kwa mguu mmoja,kwa hiyo kuku 7 wana miguu 7 na sio 14!".Yesu hakutaka ubishi,wakaendelea kula.Wakiwa nje,Yuda alimwonesha Yesu Jogoo aliyesimama kwa mguu mmoja kama ushahidi kwamba kuku ana mguu mmoja.Yesu akamrushia jiwe yule jogoo na yule jogoo akachomoa mguu wa pili,akakimbia kwa miguu miwili.Yuda akasema,"mimi sishangai,umeshaanza miujiza yako,umemrushia jogoo jiwe kisha ameota mguu wa pili na kukimbia kwa miguu miwili!