Yu wapi Maunda Zoro?

Fredinho

JF-Expert Member
May 18, 2016
971
1,160
Staa huyo wa nyimbo kama niwe wako na mapenzi ni ya wawili amepotea sana kwenye tasnia ya muziki,sauti yake tamu na nyororo ilitakiwa iendelee kutuburudisha katika vipindi mbali mbali vya 'romantic time', macho yake yenye mvuto yalitakiwa yaendelee kutuliwaza katika tv zetu kwa video kali za marangirangi,lakini ghafla Maunda kapotea kama stori za katiba mpya! kitu gani kilimpata?au alishaacha muziki!!!
 
mkuu una uhakika gani...na hayo unayozungumza?
mwezi mmoja au zaidi baba yake alihojiwa na gazeti fulani na pamoja na mambo mengine ya uzazi aligusia kuwa Maund aliapata shida na sukari ya hudhurungi...........japo alidai kuwa kwa sasa anaendelea poa na amaeushinda uraibu wa madawa uliokuwa ikimshikilia mateka
 
Guys nimesoma na Maunda ktk Level ya secondary- kongowe mbagala, shule ya Dsm Christian Seminary

Kwa sasa Maunda ameolewa na yupo ktk ndoa yake
Anaishi Kurasini

So ndoa ina mambo mengi hatuwezijua anavyojipanga kurudi ktk tasnia ya music japo kwa sasa ni mama kijacho!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom