Hata magumu yana sababu; soma kisa cha Selena Gomes na rafiki yake Francia

longi mapexa

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
3,197
3,994
Siku ya 22 katika mwezi wa July mwaka 1992 maeneo ya Grand Prairie katika jimbo la Texas nchini Marekani binti mwenye umri wa miaka 16 aliyejulikana kwa jina la Amanda Dawn Cornet anafanikiwa kumleta kiumbe mpya katika ulimwengu huu huku akiwa na furaha kubwa ya kumzalia mume wake Bwana Ricardo Joel Gomez mtoto wa kike ambaye kwa pamoja walikubaliana kumuita Selena.

Basi kama ujuavyo kuwa siku hazigandi, nayo miaka ikasogea mtoto Selena akazidi kukua na kwa wakati huo familia yao ilikua na hali mbaya kiuchumi. Tofauti na ilivyozoeleka katika familia nyingi baba kuwa tegemeo. Familia hii mama ndiye aliyekua tegemeo kuu katika maswala yote pale nyumbani.

Miaka 5 baada ya Selena kuzaliwa baba na mama yake walitengana hivyo Jukumu la malezi ya Selena Yakabakia kwa Mama yake Amanda na kwa kipindi hicho walikuwa katika umaskini uliokithiri. Amanda alikua akijishughulisha na maswala Ya uandaaji wa maigizo kama kazi pekee Iliyosababisha maisha yake na binti yake Selena yaendelee.

Kwa kuwa Mungu si mwanasiasa mnamo mwaka 2000 nyota ya Selena ilianza kung’aa akiwa bado ni binti mdogo wa miaka 8 Alianza kupata fursa za kuigiza katika vipindi vya runinga vya Disney Channel. Hapo ndipo umaarufu wake ulipoanza kukua kwa kasi na kwa wakati huo huo aligundulika kuwa na kipaji kingine cha uimbaji. Huo Ukawa mwanzo wa safari rasmi Ya kuingia katika ulimwengu wa burudani.

Maisha yake Yakaanza kubadilika kwa kiwango kikubwa. Kutoka kwenye umaskini mpaka kuanza kuingiza mamilioni ya fedha. Naam neema ikamshukia akazidi kukubalika na ulimwengu haswaa katika tasnia ya muziki matamasha mbalimbali ya kimuziki yakazidi kumyookea na hakika Selena akazidi kuuteka ulimwengu wa burudani kwa mafanikio makubwa. Akaanza kupokea tuzo mbalimbali kudhihirisha ubora wake.

Kwenye mahusiano pia hakuwa nyuma akabahatika kuzama katika penzi zito na kijana mdogo Mwenye mvuto na ushawishi mkubwa miongoni mwa nyota wa muziki kule marekani naye si mwingine bali ni sukari ya warembo anayejulikana kama Justin Bieber uhusiano wao ukawa kama alama muhimu ya mapenzi kwa vijana wengi duniani huku wakituburudisha kwa utunzi wa nyimbo zao za kimahaba,kila aliyekuwa katika mahusiano alitamani kuwa kama wao kiukweli walipendeza sana. Kwa hakika hilo nalo likazidisha umaarufu wake maradufu.


Kijamii akazidi kuwa na ushawishi mkubwa hali iliyopelekea jicho la umoja wa mataifa kumtazama na hatimaye kumpa ubalozi katika shirika la watoto duniani. Akiwa na miaka 17 tu akafanikiwa kuwa balozi wa UNICEF huku akiweka rekodi ya Kuwa balozi mwenye umri mdogo zaidi kwa wakati huo .

Kwenye mitandao ya kijamiii akazidi kuwaburuza nyota wenzake. Ni Selena Gomez ndiye aliyekuwa anaongoza kwa kuwa na Followers wengi ulimwenguni katika mtandao wa Instagram kabla ya kuja kupitwa na mwanasoka nguli asiyehishiwa na maajabu katika dunia ya mpira anayeichezea Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo.

Lakini mbali na umaarufu pamoja na utajiri aliokua nao Ipo siri aliyokuwa akiificha kwa muda mrefu.
Akiwa nyota maarufu katika kizazi chake Selena Gomez alikua na kila kitu kuanzia utajiri kipaji kinachozalisha ushawishi mkubwa katika jamii pamoja na uhusiano wa kimapenzi ulioonekana wenye furaha zaidi duniani.
Siku moja alipokea taarifa mbaya iliyo badilisha maisha yake daima. Alipimwa na madaktari akagundulika kuwa na ugonjwa usio na tiba ni ugonjwa unaosababisha kinga ya mwili kushambulia Tishu na organ mwilini. Ugonjwa huo unajulikana Kwa jina la LUPUS.

Madhara ya Lupus.
Katika hali ya kushangaza Selena Gomez alikataa matokeo ya uchunguzi wa madaktari Na akaamua kuweka usiri mkubwa katika maswala ya afya yake. Bila kukata tamaa aliendelea kutumbuiza katika matamasha mbalimbali Na hata akafikia uamuzi wa kufanya Ziara katika nchi mbalimbali Duniani wenyewe wanaita “world tour” Alifanya hivyo mpaka pale hali yake kiafya ilipoanza kuzorota na hatimaye ikawa ngumu kupuuzia ugonjwa huo .

Akajikuta akiwa katika msongo wa mawazo sonona pamoja na kuchanganyikiwa yote hayo yakisababishwa Na madhara ya ugonjwa wa Lupus ambao tayari ulishaanza kumdhuru kwa kiwango kikubwa. Kuna wakati alishindwa hata kufungua chupa ya maji kutokana na kuishiwa na nguvu aliishia kutupa chupa sakafuni na kuanza kulia kwa uchungu.

Kwa kujihisi kushindwa kusonga mbele kwenye shughuli zake aliamua kuacha shughuli za muziki na uigizaji kwa muda ili kupata muda wa kujitibu maradhi yaliyokua yakimuandama

Majanga juu ya majanga.
Wakati akiwa anahangaikia ugonjwa wa Lupus na madhara yake madaktari wakamjulisha kuwa anatatizo lingine la Figo hivyo anahitajika kufanyiwa upasuaji wa haraka ili kuwekewa itakayoweza kuendeleza maisha yake vinginevyo atapoteza uhai. Kwa taarifa hiyo Alijikuta anarudi nyumbani bila kuwa na matumaini tena huku hofu ikiutawala Moyo wake. Kibaya zaidi katika orodha ya Watakao weza kunufaika na mpandikizo wa figo yeye huwenda ingemchukua kuanzia miaka Saba mpaka Kumi jambo ambalo lisingeruhusu yaye kuishi kutokana na tatizo lake kuhitaji uharaka wa matibabu. Hakika hiki kilikua kipindi kugumu sana katika maisha ya mrembo huyo.

Uhai zawadi pekee yenye thamani.
Siku moja alitembelewa na rafiki ya anayeitwa Francia binti huyu ni muigizaji pia. Kutokana na hali aliyokua nayo Selena, Francia Alimuuliza rafiki yake ni nini kinachomsibu. Huku akibubujikwa na machozi Selena alimpa habari ya mambo yaliyojiri pindi alipokwenda hospitali. Kama muujiza Francia aliamua kwenda kupimwa kama anaweza kumpatia Selena figo yake moja licha ya mama yake kumshauri kutokutoa figo yake. Safari hii ikiwa ni zaidi ya muujiza vipimo vilithibitisha uwezekano wa Selena kuweza kupandikiziwa figo ya Francia. NURU IKARUDI TENA Katika uso wa mwanadada Selena Gomez.

Muda wa upasuaji uliwadia ikiwa ni siku moja kabla ya upasuaji marafiki wawili walikaa pamoja wakisubiri tukio kubwa liliopo mbele yao. Francia aliamua kuandika wosia ili endapo akishindwa kupona wakati wa upasuaji awe amewaachia ujumbe aliokuwa akitaka kuwapa wale watakao bakia duniani. Siku ya upasuaji ilipofika Francia alikua wakwanza na mambo yalikwenda vizuri kisha ikawa ni zamu Ya Selena Gomez.

Mshumaa katika upepo mkali.
Wakati wa upasuaji wa Selena jambo baya likatokea na kufanya mambo kuwa magumu zaidi mshipa wa atery uliharibika ikabidi ahamishiwe kwenye upasuaji Mwingine wa Dharura ambapo madaktari walifanikiwa kutegeneza atery mpya kwa kutumia vein waliyochukua kutoka katika mguu wake.
Baada ya hapo taratibu zingine ziliendelea na hatimaye akafanikiwa kupandikiziwa figo baada ya siku kadhaa hali yake ikawa nzuri akazidi kukua vizuri kiafya hatimaye akapona. Furaha ikatawala akapata tumaini jipya ndani ya maisha yake ni tumaini Lililomfanya arudi tena katika ulimwengu wa burudani safari hii akaanzisha na mifuko mbalimbali iliyojikita katika kutoa misaada Kwa wasiojiweza na kwa wanaougua ugonjwa wa Lupus bila kuwasahau wenye madhara katika afya ya akili.
Anatunukiwa tuzo.

Billboard ambao ni wadau wakubwa wa muziki duniani walimtunuku tuzo ya Billboard Women In Music Awards Kama mwanamke mwenye mafanikio makubwa katika muziki. Ni usiku ambao ulimwengu wa muziki uliamua kutambua mchango wake katika kiwanda cha muziki duniani lakini Selena Gomez aliamua kuiambia dunia ni vyema wakamtambua aliyeokoa maisha yake kama yeye anavyomthamini na kumshukuru kila siku.


Huku akibubujikwa na machozi alimsifu rafiki yake akisema “Nafikiri tuzo hii alipaswa kupewa Francia kwani ni yeye ndiye aliyeokoa maisha yangu”. Changamoto zilizomkumba Selena Gomez zimemfanya kuwa na mtazamo tofauti katika maisha na siku zote amekua akinukuliwa akisema “Tunaishi mara moja na maisha yana thamani kubwa tuna mengi ya kufanya”
Fundisho;

Hata magumu yana sababu. Kuna wakati tunakuwa katika kiwango cha chini kabisa katika maisha ila ni vyema tukajipa tumaini kuwa yanayotupata ni sehemu tu ya Mpango wa sisi kusimama tukiwa imara na kuwa na mitazamo chanya kuhusu zawadi ya thamani tuliyo nayo ambayo ni UHAI.

El Artista.
 

Attachments

  • 077befd24bc0ee305f413a192a1aac2e.jpg
    077befd24bc0ee305f413a192a1aac2e.jpg
    40 KB · Views: 57
  • 91d5e7be4a2fbf5e03f16c8ed6995cb7.jpg
    91d5e7be4a2fbf5e03f16c8ed6995cb7.jpg
    21.8 KB · Views: 49
  • 8b5ee10c183d8300df7572d10261bf02.jpg
    8b5ee10c183d8300df7572d10261bf02.jpg
    32.8 KB · Views: 52
  • 7cb40370d0a5ecabda5903b522c4564f.jpg
    7cb40370d0a5ecabda5903b522c4564f.jpg
    52.3 KB · Views: 57
  • dcbcad181189e1544f5b5ee9f394e4f0.jpg
    dcbcad181189e1544f5b5ee9f394e4f0.jpg
    74.7 KB · Views: 55
  • de8948a38f764a49736bcfeb6f58a753.jpg
    de8948a38f764a49736bcfeb6f58a753.jpg
    7.8 KB · Views: 55
  • 01d1ec1ce22b8f1c53363ff91cd6a9ea.jpg
    01d1ec1ce22b8f1c53363ff91cd6a9ea.jpg
    68.4 KB · Views: 60
First to reply..... very interesting story, cha muhimu ni kutokukata tamaa katika maisha.
Ni Kweli mkuu mara nyingi tukiyumbishwa tunapoteza malengo kitu ambacho tunapaswa kubadilisha. Pia ni muhimu kujipa matumaini na mawazo chanya siku zote.
 
kwahiyo after seven years anafariki au na hyo lupus inasababishwa na nn naomba kutambua tafadhal
Mkuu japokua mimi sio mtaalam sana wa maswala ya afya kwa nlivyosoma wanasema ugonjwa huu unatokana na kinga ya mwili kuanza kushambulia tishu na organ za mwili.
 
Hawa wasanii wa bongo nawashangaa Sanaa.
unakuta jitu linaimba et
"Zawadi kubwa Ni kubarikiwa wowowo"

Hapo akipigwa homa na kuwa kitandani nadhani ndipo atajua zawadi kubwa Ni kubarikiwa "UHAI NA PUMZI"

Gomez alikuwa kitandani,pesa na umaarufu haukuwa kitu kwqke zaidi ya kupambania UHAI.



Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu wakishaumwa ndipo wanapokumbuka haya
 
Hawa wasanii wa bongo nawashangaa Sanaa.
unakuta jitu linaimba et
"Zawadi kubwa Ni kubarikiwa wowowo"

Hapo akipigwa homa na kuwa kitandani nadhani ndipo atajua zawadi kubwa Ni kubarikiwa "UHAI NA PUMZI"

Gomez alikuwa kitandani,pesa na umaarufu haukuwa kitu kwqke zaidi ya kupambania UHAI.



Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha ishu ya steve Jobs!! Daaah maisha haya hela tunaitafua ila kuna kipindi haina thamani kabisa maishani
 
Back
Top Bottom