Yu wapi Dkt. Masumbuko Lamwai?

Laswai huwezi acha kumtaja kwenye historia ya mageuzi....alikuwa machachari Kama Tundu Lisu .....CCM wabaya ...wakamfanyia visa ...kumfukuza kazi UD,akafungiwa uwakili ...ubunge wakambana akapoteza ...Hii mbinu inaitwa starving
Mwisho akarudi ccm.....wakampa kazi mbili Tatu...baadaye walipohakikisha Hana Tena nguvu mitaaani wakamtupa......alikuwa na nguvu Sana kwa vijana ...lakini ikifikia anapita mitaaani vijana wanamnunnia na ccm ndicho walichotaka

Ni Kama nguvu alikuwa nayo Kabourou Kigoma ..nadhani hata Zitto hajaaifikia ,,watu walikuwa wanalaala train station kumsubiri Kama anakuwa ..lakini HUYO Leo Zitto kamagragaza vibaya ..wananchi wanamuadhibu kwa kuwasaliti
 
Wakuu,

Naomba anayejua habari za Dkt. Masumbuko Lamwai, mwanasiasa na mwana harakati kwenye miaka ya nyuma alikua kivutio kikubwa kwa vyombo va habari na wananchi hapa Tanzania.
 
Mwasheria ambaye hakuwa na msimamo, akadanganywa akawa ni wa kuhama hama na mwisho akapotea kwenye nyanja zote za siasa na sheria
 
Mwasheria ambaye hakuwa na msimamo, akadanganywa akawa ni wa kuhama hama na mwisho akapotea kwenye nyanja zote za siasa na sheria
Aisee yawezakuwa maana alikuwa alikuwa mchezaji mzuri sana kwenye siasa na sheria.
 
Nilimkuta mahakamani amechoka amevaa koti kubwa akiwatetea wahalifu wa kuku sikuamini ni yeye !!!! ilikuwa 2009 kule Moshi
 
Wakuu,

Naomba anayejua habari za Dkt. Masumbuko Lamwai, mwanasiasa na mwana harakati kwenye miaka ya nyuma alikua kivutio kikubwa kwa vyombo va habari na wananchi hapa Tanzania.
Alikua miongoni mwa wanasiasa niliowapenda miaka ya
90
 
Ukiwa mwanasiasa mnafiki hufikwa na mwisho kama alio nao bwana masumbuko lamwai
Ndivyo utakavyo kuwa mwisho wa Lipumba pia
 
Yupo anaungaunga maisha tu. Kwa sasa ni mwanasheria wa Ghullam Dewji na bado ni mhadhiri.
 
[HASHTAG]#Omojubi[/HASHTAG]

Utabiri wako wa Feb 20/2013 na leo hii ni disembar 27/2016, Utabiri wako umetimia, ahsante sana
 
Mbona Lamwai amekuwa maarufu hata kabla ajachaguliwa Diwani wa Manzese, Kwenye Corridor za Mahakama za Tanzania jina lake si Dogo, Ni Mwalimu mzuri wa Sheria, kwamba UKIMWI unamtaiti, sina uhakika sana na hilo, mara nyingi nimetokea kufanya naye kazi kwa karibu sijaona tofauti ya Afya yake. Naona yuko fit.Kila mtu anahitaji kuombewa aliye na ........., na asiye na .............., unless kama mtu ameamua kuwa Towashi , vinginevyo huwezi kujua kesho yako.
Umeongea kama kiongozi wa kiroho, nimeipenda
 
Huyu jamaa alikuwa tegemeo la kambi ya upinzani kabla hajaamua kulinda maslahi ya familia yake.Angeamua kusimamia anachoamini kama alivyofanya prof Baregu leo hii angrkuwa mtu mwenye heshima kubwa upande wa wanamageuzi,pia angekuwa hazina kubwa ya mabadiliko kama Lisu
 
Mwaka 1994 akiwa NCCR Mageuzi tulimchagua kuwa Diwani kata ya Manzese, na hapo ndipo alianza kujulikana zaidi mitaani. Mwaka 1995 akiwa aligombea ubunge jimbo la Ubungo na alikuwa ameshinda pamoja na wenzake wa NCCR katika majimbo yote ya DSM lakini uchaguzi huo ulifutwa saa nane ya usiku baada ya tume kuona kuwa dsm yote imechukuliwa na upinzani.
Kwa kuwa NCCR haikuridhika na uchaguzi tanzania nzima, iliamua kujitoa, ila kisheria haikuwezekana. Wagombea wengine wote wa NCCR walitangaza kususia uchaguzi wa marudio dsm, lakini Lamwai alikataa na kushiriki; na tulimchagua kuwa mbunge wa jimbo la ubungo. Matokeo hayo yalipingwa mahakamani na Lamwai akashindwa kesi; na huo ukawa mwanzo wa mporomoko wake.
Baada ya hapo alifutiwa ualimu wa udsm na pia serikali ilimfutia leseni yake ya uwakili wa kujitegemea. Lamwai akadhoofu na akawa hana budi kujisalimisha kwa CCM. Ndipo Mkapa alimteua kuwa mbunge.
Kitendo cha Lamwai kurudi CCM na kuteuliwa na mkapa, kilimshushia heshima katika jamii - kama mchangiaji mmoja alivyosema 'siamini kama mtu aliyekuwa anaikandia sana ccm angeweza kurudi huko'. Wengi tulimwona kama mtu aliyekosa uvumilivu na ujasiri wa kundelea kuwa upinzani - alitusaliti. Kwa kuwa JK hakumteua tena kuwa mbunge; ikawa ndio mwisho wake katika siasa. Hana tofauti na Kabourou wa Kigoma
Kwahiyo haya ya akina Masha leo hii sio mambo mapya kabisa.
 
Back
Top Bottom