Yu wapi Dkt. Masumbuko Lamwai?

Masumbuko Lamwai?Ohh yule mwanasheria wa Ikulu. Kwanini CCM waliogopa kumpambanisha na Tindu katika kesi ya Ubunge wa Lema?
 
Jamani hivi huyu mwasheria aliyewahi kuwa Mbunge siku za nyuma nadhani kupitia NCCR kama sikosei, yuko wapi siku hizi?mbona hasikiki ...
MWENYE HABARI ZAIDI JUU YAKE AZIMWAGE HAPAJAMVINI...
mimi nichofahamu ni Walid Kaburu, kutoka mbunge wa afrika mashariki mpaka mwenyekiti wa ccm kikoma
 
Lamwai anafundisha Tumaini University ndo dean faculty of law, pia anafundisha law school of tz na anafanya shughuli zake za uwakili maisha yanaenda. Alosoma kasoma tu

Alinyang'anywa leseni ya uwakili siku mingi jo.
 
Mkuu ni vyema utambue Dr. Masumbuko Lamwai alikuwa ni mhadhiri pale UDSM-school of Law; Swali la kujiuliza kwa nini Dr.Lamwai haendelei na kibarua chake pale UDSM?

hivi unajua law school imeanza lini Tz?
 
Masumbuko lamwai miaka michache iliyopita alikuwa ni miangoni mwa mawakili wazuri sana na hata alipokuwa mbunge alikuwa anajua sana kujenga hoja bungeni,na aliweza kuwafanya vijana wengi wa wakati ule wasome sheria wakienda chuo kikuu,swali langu hivi huyu jamaa yuko wapi?na nini kilimpata mpaka amepotea kiasi hiki,ninacho amini nikwamba bado yuko hai,na je akirudi kwenye siasa kwa sasa anaweza akafanya vizuri kama enzi hizo?na ni chama gani kinaweza kumfaa zaidi?Naomba mwenye majibu atupie
 
Jamani hivi huyu mwasheria aliyewahi kuwa Mbunge siku za nyuma nadhani kupitia NCCR kama sikosei, yuko wapi siku hizi?mbona hasikiki tena, nilisikia habari kuwa alijiengua kutoka NCCR na kujiunga na CCM, je ni kweli?

Yuko tumain university anafundisha sheria..
 

Masumbuko Lamwai
Joseph Selasini
Baba: Roman Shao (RIP)
Sielewi elewi...
 

cdm kitamfaa sana, ila kwa sasa nitamshauri awe katika kamati ya wazee wa chama.
 
Ndugu siasa hacha kupigana ngumi kumbe watu wanakula saani moja wapi mrema wapi maalim seif wapi mbati .
 
Kwa sasa amefulia tu, yuko nyumbani kwake Ubungo Kibangu na kazi yake sasa hivi ni kukagua daftari la bili ya maziwa, biashara ya mkewe.

Aliyeko CHADEMA ni mdogo wake Joseph Selasini, yule aliyemng'oa Mramba kule Rombo.

kumbe ni ndugu hawa watu?
 

kamanda huyu jamaa kwa sasa ni mwanasheria wa magamba
 
Poa sasa nimefahamu, lakini hawa jamaa sometimes wanatuchezea akili, siamini jinsi alivyokuwa anaikandia CCM, ati leo hii naye kesha kuwa mwanasheria wao. Kweli siasa ni MCHEZO MCHAFU!
Neither permanent friend nor permanent enemy in Politics.
 
Dr. Lamwai Masumbuko, Senior Lecturer - PhD (London), LLM 1978, UDSM, LLB 1976 UDSM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…