Mwaka 1994 akiwa NCCR Mageuzi tulimchagua kuwa Diwani kata ya Manzese, na hapo ndipo alianza kujulikana zaidi mitaani. Mwaka 1995 akiwa aligombea ubunge jimbo la Ubungo na alikuwa ameshinda pamoja na wenzake wa NCCR katika majimbo yote ya DSM lakini uchaguzi huo ulifutwa saa nane ya usiku baada ya tume kuona kuwa dsm yote imechukuliwa na upinzani.
Kwa kuwa NCCR haikuridhika na uchaguzi tanzania nzima, iliamua kujitoa, ila kisheria haikuwezekana. Wagombea wengine wote wa NCCR walitangaza kususia uchaguzi wa marudio dsm, lakini Lamwai alikataa na kushiriki; na tulimchagua kuwa mbunge wa jimbo la ubungo. Matokeo hayo yalipingwa mahakamani na Lamwai akashindwa kesi; na huo ukawa mwanzo wa mporomoko wake.
Baada ya hapo alifutiwa ualimu wa udsm na pia serikali ilimfutia leseni yake ya uwakili wa kujitegemea. Lamwai akadhoofu na akawa hana budi kujisalimisha kwa CCM. Ndipo Mkapa alimteua kuwa mbunge.
Kitendo cha Lamwai kurudi CCM na kuteuliwa na mkapa, kilimshushia heshima katika jamii - kama mchangiaji mmoja alivyosema 'siamini kama mtu aliyekuwa anaikandia sana ccm angeweza kurudi huko'. Wengi tulimwona kama mtu aliyekosa uvumilivu na ujasiri wa kundelea kuwa upinzani - alitusaliti. Kwa kuwa JK hakumteua tena kuwa mbunge; ikawa ndio mwisho wake katika siasa. Hana tofauti na Kabourou wa Kigoma