Young cartoonist. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Young cartoonist.

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Jaguar, Apr 16, 2011.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mwalimu aliwaambia wanafunzi wake wachore picha ya mnyama tembo.Wanafunzi walijitahidi kuchora hiyo picha kwa ustadi tofauti isipokuwa john alichora nukta tu.Mwalimu alipomfikia kukagua picha yake akahoji picha aliyochora iko wapi?John akamwonyesha ile nukta huku akisema,'huyu ndo tembo niliyemchora sema tu yuko mbali balaa,ndo maana anaonekana mdogo kama nukta'.
   
 2. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  (b)Wiki ya pili,mwalimu yule yule aliwaambia wanafunzi wake wachore picha inayoonyesha kazi wanayopendelea kufanya baadaye.Wengine walijichora madereva,wengine madokta,wengine mafundi waashi,wengine walimu n.k.Mwalimu alipokuwa anakagua,alimkuta mtoto Asia hajachora picha yoyote.Mwalimu akahoji kulikoni,Asia akajibu,'mwalimu mimi baadaye nataka kuolewa lakini sielewi nitajichoraje kuonyesha hiyo kazi yangu ya baadaye!
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ahahahah!
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Tehe tehe tehe teeeeh!!!
  Hii ndio kama ile wanafunzi waliambiwa wachore treni, John yeye hakuchora na mwalimu wake alipokuja kukagua akamwambia kuwa "umechelewa treni imeondoka"
   
 5. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Very creative!
   
 6. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Au refu sana halitoshi kwenye daftari!
   
 7. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,265
  Trophy Points: 280
  (c) Wiki ya tatu mwalimu akwaambia wachore ng'ombe amakula majani...wengine wakachora mgo'mbe wazuri wakubwa, wakapaka rangi, wengine wakaongeza na vindama...ila John..alichora kwato tu na vimajani vidogooooo...
  Mwalimu alipokuja kukagua akamkasirikia John kwanini hajamchora ng'ombe. John akahamaki, "Ha! mwalimu nimemchora mwalimu, atakuwa ameenda pengine kuatfuta majani..si unaona alitembea hapa (akimwonyesha footsteps) na majani hapa ni madogo sana!"
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,265
  Trophy Points: 280
  (d)Wiki ya nne mwalimu akaona isiwe nongwa, akawaambia waandike insha inayoanza na, "Tulipofika kambini..." Aliwataka wa-assume wako kwenye vita vya Tanzania na Uganda (enzi za Idi Amin). Na wao ni wanajeshi wamepelekwa kambini kule Kagera....then waendelee! wawe creative as they wanted..
  Basi wanafunzi wakaandika wengine pages nne, tano, kumi..yaani walijimwaga alimradi wapate maksi zote..
  siku ya kukagua kazi Mwalimu alifurahishwa sana na wanafunzi wake walivyojituma, alipofika kwa John akashtuka kukuta John kaisha mstari wa kwanza, yaani, "Tulipofika kambini..."
  Akamuuliza kwa hasira kwa nini hakuandika insha yake kama wengine!?? John akamjibu, "..lakini mwalimu tulipofika tu kambini, maadui wa Idi Amini walituvamia wakatuua, sasa ningeandika je zaidi!??"
   
 9. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  (e)Mwalimu yule yule alihamishiwa mtwara.siku moja aliwaambia wanafunzi wachore chochote wanachopenda,akaenda ofisini,akaahidi kurudi baadaye kukagua.Aliporudi baadaye hakumkuta hata mwanafunzi mmoja darasani,wote waliondoka kwa sababu kwa kimakonde KUCHORA ni KUONDOKA!
   
 10. m

  magneto Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  (e)Mwalimu yule yule
  alihamishiwa mtwara.siku moja
  aliwaambia wanafunzi wachore
  chochote wanachopenda,akaenda
  ofisini,akaahidi kurudi baadaye
  kukagua.Aliporudi baadaye
  hakumkuta hata mwanafunzi
  mmoja darasani,wote waliondoka
  kwa sababu kwa kimakonde
  KUCHORA ni KUONDOKA!

  Kesho yake sasa mwalimu kaingia akiwa na ghadhab,'jana mlifaid eh,sasa na leo muondoke....' akageuka kumbe mwalimu mkuu alikuwa mlangoni akamwita kwa ishara kuelekea ofisini bila kumalizia sentensi yake.aliporudi sasa! wanafunzi wamesepa kitambo!
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Mtoto Genius.
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ahahahaaah!!
   
Loading...